Wapi ndugu zangu waweza uza madini ya Ruby?

Wapi ndugu zangu waweza uza madini ya Ruby?

Muwe makini pia mtakao enda kununua msije pigwa mkaja kulalamika huku jf

Ushauri kwa ambaye atavutiwa katika hilo dili hakikisha una servilance ya kutosha na hata uwe na tails kibao au ma sniper , hii biashara kwetu sisi haina tofauti na zile biashara za ngada.. Point ni kwamba hutakiwi kuamini hata kama utapewa pesa mpaka vyote vi balance.

Umemshauri vizuri sana Kiongozi maana hii biashara sitakagi kuisikia tena maishani mwangu!!
 
Lazima useme hivyo sababu hujawahi kuishika na wala hujui inapatikana katika mazingira gani kwa utaratibu upi yaani kwa ufupi You know nothing...... Tunazungumzia Ruby umeshaingiza na mambo ya rupia. Kuna mwingine ukikwambia mambo ya rupia anakuambia hivyo vitu havipo ni hadithi tu so tunatofautiana ufahamu katika mambo mengi. Jukumu la kuamini ama kutokuamini ni la kwako msomaji hujashikiwa bastola ukubaliane na hoja hii and vice versa

Huyu ndio Fixer.. Anakufix tu ukizubaa.. Mjini hapa.
 
Last edited by a moderator:
Umemshauri vizuri sana Kiongozi maana hii biashara sitakagi kuisikia tena maishani mwangu!!
Kwa dhana hii ni wazi nina kazi kubwa sana kuhakikisha kama madini haya ni yenyewe nayauza!!
 
Amani kwenu wadau wa biashara.

Ndugu zangu huko kijijini wamefanikiwa kuchimba madini ya ruby kwa walivyo niambia, yanakadiriwa kufikia robo tatu ya KG. Ila hawajui wapi wayauze na pia hawana vibali vya uchimbaji maana kwa uwezo wao hawawezi kuwa nao. Pia natambua utata wa kisheria uliopo juu ya umiliki wa madini. maana kwa sheria ya madini iliyopitishwa miaka michache iliyopita hata ukiokota madini uko kwenye kosa kisheria.

Naomba msaada wenu, ni wapi ndugu zangu hawa wanaweza kuuza madini yao kisheria na walipe kodi huku wakipata stahili zao bila kupunjwa??

Nimepitia mitandaoni na kupata bei za kimataifa na inaonesha madini haya yanathamani si haba.... Ila ni wapi wanapoweza kuuza na wasikutana na matatizo ya kisheria?? ni kipi wafanye??

Naweza kuwa nimechanganya madesa katika uandishi wa hoja yangu.... Nisameheni!! Ila dhamira yangu ni kuwasaidia ndugu zangu hawa wasije uza at black market au wakayauza kwa bei ya hovyo kama wazee wetu wakati wa ukoloni walipobadilisha kwa shanga!!

nategemea majibu yatayonisaidia.

Acha utapeli , nyie ndo mnatafuta wa kuwapiga unajua rubb wew , ngoja nimshtue mod . Maana mmezoea kutapeli watu kwenye JF
 
Acha utapeli , nyie ndo mnatafuta wa kuwapiga unajua rubb wew , ngoja nimshtue mod . Maana mmezoea kutapeli watu kwenye JF
Bro hivi akili zako zinafanya kazi?? Unatuhumu na kutoa hukumu. stu pid kabisa.... we umeona mimi nimeomba nini?? Ji.nga kweli wewe. Unanijua mimi na unahakika gani kuwa natapeli??
 
Kaka unadhani biashara hii inafanyikaje?? Unaamini kuwa madini haya yapo na yanafanyiwa biashara??

Ndugu wanajamii forum huyu jamaa ni tapeli kuweni makini na hawa matapeli kuna siku alikuja humu eti anauza Green tomalin eti akanieleza ana nusu kiroba kitu ambacho sio rahisi kupata hata gram 300 ni shida. baada ya kumbana jamaa akapotea maana mimi ni mtaalam wa hayo madude
 
Oop hayo ni madini au majini? Serikali itafute njia ya kuwanusuru hawa wachimbaji maskini wasijedhulumiwa. Wakubwa
mmeshaweka pesa nyingi huko Uswizi zinawatosha
 
Ndugu wanajamii forum huyu jamaa ni tapeli kuweni makini na hawa matapeli kuna siku alikuja humu eti anauza Green tomalin eti akanieleza ana nusu kiroba kitu ambacho sio rahisi kupata hata gram 300 ni shida. baada ya kumbana jamaa akapotea maana mimi ni mtaalam wa hayo madude

Hebu nakuomba usiharibu uzi huu kwa fikra zako hasi dhidi yangu.... Niko hapa naomba uulete uzi huo hapa nikielezea kuhusu Green Tomalin...kama ni mimi nitaomba ma admin wanipige life ban!! Watu wengine wa hovyo sana. Nimeuliza watu wenye ujuzi wa mambo haya na nimeeleza ukweli ulivyo... fuatilia comment zote ili uelewe sio kuja na judgement zako hapa.
 
Biashara ya madini haitaki kuambiwa kitu ambacho hujakiona. Jamaa wa vijijini wepesi sana kusema wana mawe ukija yaona unakuta ni uchafu.. Makapshon yaliyoziba kabsaa au hata sio ruby.

Kwa kiasi cha Ruby waliyosema wanayo 3/4 kgs bila kupepesa macho na utakuja nithibitishia hapa sio Gem quality.. Hzo wakijitahidi sana ni kapshon na sio high.

Pocket ya Ruby inaweza ikawa na kilo 100 lakini ukaotea kaGem quality 0.8grams tuu au usipate kabisa.

.......
 
Hicho ndicho nachotaka kusubiri nikione.... Na pia kwakuwa si mimi wala wao wanaojua ruby yenye quality ni ipi ndipo hapo ugumu unapokuja.

Kwa wingi wa walivyosema hata mimi ninapata wasiwasi though pia nasubiri kujionea... yakifika tu nitaweka picha ya madini hayo kwenye thread hii. Pia nitaendelea mbele zaidi kuhakikisha kuwa ni madini yenyewe na yanathamani gani mpaka yatakapouzwa. Kwa vyovyote vile itavyokuwa.. nasubiri mzigo uje kwanza.
 
tunduru utauza maana ndiko watu wanakochimba na kuuza.kuna wa sri lanka wengi sana wanao nunua
 
Halahala usiwekeza hata senti moja katika biashara hiyo.
Kama huna uzoefu nayo huku ukitegemea Wataalam wa JF.
Usije-sema hukuonywa!
 
Halahala usiwekeza hata senti moja katika biashara hiyo.
Kama huna uzoefu nayo huku ukitegemea Wataalam wa JF.
Usije-sema hukuonywa!
Sijawekeza hata senti... waliochimba ni ndugu zangu wa ukoo... wameniomba niwasaidie katika mchakato wa kuyauza na nitakuwa nao kila hatua mpaka watapoyauza.

Ahsante kwa caution yako.
 
Baadhi ya picha za madini hayo yaliyoagizwa kwangu kama sample!! Narudia kusema kuwa sijui ni madini gani!!
 
Attachments

  • IMG-20150903-WA0035.jpg
    IMG-20150903-WA0035.jpg
    51.9 KB · Views: 183
  • IMG-20150903-WA0031.jpg
    IMG-20150903-WA0031.jpg
    83.8 KB · Views: 154
  • IMG-20150903-WA0030.jpg
    IMG-20150903-WA0030.jpg
    47.8 KB · Views: 150
  • IMG-20150903-WA0028.jpg
    IMG-20150903-WA0028.jpg
    56.2 KB · Views: 166
  • IMG-20150903-WA0027.jpg
    IMG-20150903-WA0027.jpg
    66.2 KB · Views: 196
Picha zaidi.... wamenitumia vipande 15 tu.
 
Attachments

  • IMG-20150903-WA0025.jpg
    IMG-20150903-WA0025.jpg
    102.5 KB · Views: 171
  • IMG-20150903-WA0024.jpg
    IMG-20150903-WA0024.jpg
    91.3 KB · Views: 175
  • IMG-20150903-WA0023.jpg
    IMG-20150903-WA0023.jpg
    55 KB · Views: 136
Back
Top Bottom