Wapi nitapata mganga wa Kienyeji mzuri?

Wapi nitapata mganga wa Kienyeji mzuri?

Ukienda bila ramani na uulize kila mtu hasa Kwa kigoma umeisha,watu wa kigoma kila umuonaye ni wakala wa mganga fulani,hii naongea ilishanikuta kasulu Kijiji cha kasesa ambapo nilifika na kuulizia boda mmoja ambaye nilimuona ametulia.

Alinitoa hapo lusesa kwenda Kijiji kingine ndanindani,akikonipeleka sasa yaani nilitoa Hela na sikuona maajabu yoyote zaidi ya mikosi tu.

Mikosi kiaje?

Kwanza demu wangu alinikataaa baada tu ya kutoka huko...pili nilichukiwa Sana na watu kiasi hii iliniletea ugomvi Sana.

Kwahy waganga wa kigoma wengi ni matapeli.
Kwahiyo baadae ulimpata mwenye maajabu, vip kuhusu mikosi uliitoa Kwa namna gani?
 
Kwa uzoefu wangu ,Si kila mganga ana uwezo wa kumsaidia kila mtu ,mambo mengi ya kiroho au Tiba za asili hauwendana na mkono wa mtu na nyota yako ,
Mfano
1:naweza kukawa mganga anasifiwa ni mzuri na anasaidia wengi lkn ukaenda ww ukadunda ,

2😛ia matatizo ya watu huwa hayafanani ,kila mmoja ana yake na yenye uzito wake ,kwahiyo unaweza ww umeenda ukatatulika kwa haraka ,akaja mwenzio labda ana matatizo ya muda mrefu na mazito asione chochote ,
Kubwa nacho wambia Tiba zinahitaji umakini sana na utulivu kupata suluhu kwenye kila jambo

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Kama uko serious tafuta usafiri wa toka hapo ulipo uende mpaka simiyu(bariadi mjini),kama utakua unatokea upande wa mwanza utashuka stendi ya somanda ama bariadi mjini, utapanda boda mpaka lugulu kwa buku tano na kama unatokea shinyanga utawaambia wakushushe lugulu. Baada ya hapo kuna kama vijiji viwili sijavishika jina(kama uko serious)utanifata PM nitakupatia namba za wenyeji watakaokupokea na kukupeleka eneo husika..
Mtaalam sio mzee ni kijana mwenye weledi na hataki pesa yako zaidi ya elfu mbili(2000)kabla ya kukuganga.malipo yake ni ahadi tu baada ya kufanikiwa utarudi kutoa shukrani.

Mkuu mambo unayotaka kuyajaribu uwe na moyo.
Moyo kivipi tena mkuu
 
Kuna mmoja yupo tabora ni mzuri sana, yeye anakufanyia kazi majibu unayaona kesho, Kuna mjinga mmoja nilimkopesha mil 1.7 akaanza kunizungusha pamoja na kwamba tuliandikishana kwa mwanasheria but ilipofika tarehe ya kulipa ulikua 20/January this year jamaa anasema hana pesa, kwenda kwa mwanasheria akaniambia nimuandikie barua nikimkumbusha deni pia nimuambie kuwa Nina nia ya kumshtaki baada ya siku saba nikafungue kesi mahakamani ambapo Hutu huyu mwanasheria ndo awe mtetezi na wakili wangu sasa nikapiga hesabu kama kuandikisha mkataba wa kukopeshana wakili alilamba laki je akinisimamia kesi si atanitoboa patefu pia muda utapotea basi nikampigia Huyo Fundi nikamueleza shida anasema nimuandalie chakula( pombe ) niende nazo usiku akapiga kazi akaniambia kesho asubuhi atakuletea pesa, nikamtoa ten, kesho saa12 asubuhi jamaa huyu hapa mlangoni ananiomba msamaha anasema ana mil1 inayobaki nimvumilie tarehe 5 February, nikabeba tarehe tano akaleta laki tatu, iliyobaki kaahidi tarehe 25 tena naifuata mwenyewe kwa mhasibu wake, pili Kuna jamaa yangu mmoja nilimpa ramani alikua ananiambia Kuna rafiki yake waliyeanza Maisha ya utafutaji sasa hivi yuko njema sasa kila akimuomba amkopeshe mil 5 jamaa anachomoa nilimpleka akafanyia kazi hadi aliondoka anachechemea, baada ya siku mbili nikaambiwa jamaa amenunua pump na machine Fulani za Mgodini sasa nilipomuuliza kama dili lilifanikiwa ananificha hadi Leo but najua alifanikiwa coz alikua hana hata mia mbovu hata gharama ya kwenda kwa mtaalam nilimchangia 20k but anamsifia sana fundi.
 
Dah! Kama naona vile unavyokutana na Mataperi wa JF...!
 
Nina shida binafsi nahitaji mtu mwenye kujua mganga mzuri ambaye anasaidia watu au ata yeye amemsaidia please siihitaji ushauri wala matusi kama uzi haukuusu kaa kimya hapa nahitaji mwenye kujua hili jambo tu narudia usije hapa kama hauna huyo mtu
jambo unalolifanya ni kufuru kubwa sana, Mungu anakuona kila unachofanya na anahuzunika sana juu yako. Imagine, Mungu ndiye aliyekuumba (naamini wewe pia unaamini haujaumbwa na shetani wala wachawi, Mungu alikuumba), badala ya kumtegemea yeye, umegeukia kutegemea waganga wa kienyeji ukiamini ni wazuri. shetani hajawahi kuwa mzuri, hata akikupatia kitu jua mgongoni ameficha rungu, anakusogeza unone halafu akupige rungu moja tu ukafie huko hata kabla haujampa Yesu maisha yako, na ukifa utaenda moja kwa moja motoni. Shetani ni mwizi, anaiba vilivyo vya Mungu, anaiba watoto wa Mungu, na kila kitu, hawapendi wanadamu, anatamani wote wakaingie motoni, na anakutamani wewe ukaingie motoni. Yesu alisema shetani ni baba wa uongo, akija anakudanganya kukupenda na kukusaidia kwenye biashara, cheo au chochote, alivyo mwongo kumbe anakuvuzia akuteketeza ghafla kabla haujatubu na kumrudia Mungu.

Yohana 10:10 inasema, Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele.

binafsi hayo mambo ya waganga nayajua sana, hata mali za kishetani hizo. hakuna mtua liyewahi kutajirika kwa utajiri wa kishetani mwisho wake ukawa mzuri, never. shetani hawezi kukupenda namna hiyo, mwisho wa siku huwa ni majuto tu, na ulishaukimbia uso wa Mungu unabaki na majuto na motoni utaenda. usimdharau Mungu kiasi hicho, anakuangalia akitegemea wewe ungemtumaini na kumwomba yeye, na wewe unaenda kutegemea waganga? unaenda kuomba kwa waganga? Mungu ameshindwa nini cha kukupatia hadi uende huko? dharau hii kweli Mungu anastahili kwa yote aliyokutendea? Unamdharau Mungu kwa wazi kabisa kwamba unaenda kutaka msaada kwa waganga wa kienyeji wakati Mungu yupo pale alitegemea wewe umwombe na kusaidie wewe unatukuza mashetani? kweli?

SASA UNA OPTION MBILI TU:

1. unatakiwa kuokoka, mpe Yesu Maisha yako, maadamu u haki, ni opportunity Mungu amekupatia, okoka leo, Mungu atakusaidia kwenye hayo unayopitia.

2. ukichagua kwa shetani, tegemea mambo mabaya sana mbele yako ambayo utakuja hapahapa kutoa ushuhuda, kama utapata neema ya kurudi tena, otherwise, shetani huwa anaua kwa ghafla, nimeshuhudia watu wanakufa ghafla hata wasipate nafasi kama hii uliyonayo leo, uchaguzi ni wako kwasababu utakula matunda ya kila unachoamua kuchagua. Mungu akuneemie.
 
Waganga asilimia 80 ni wa uongo ssbabu tukimpata wa kweli tunaogopa kumexpose ikimfikia namba adui yako umekwisha.pia kwa uzoefu mganga huwa mnakuja gombana akitaka toa siri za kambi anajikuta hana uliemtambulisha .

Nakushauri katafute mganga mwenyewe acha kuomba sijui namba za simu .mfano mm natoa ramani ya bure hii.

1.kibondo vijijini .ww ukifika usiulize watu mganga yuko wapi nyoosha kijijini kisha usiseme umefata nini siku 2 ukihoji mabodaboda utawapata
2.nenda hadi kigoma mjini .usiulize mtu nenda panda boti bandar inaitwa kibirizi wambie wakuache kijiji kiko ziwani kinaitwa kalya hapo usikurupuke nenda kwenye vibaa vyao wasome watu mwenyewe tafuta mzee mstaarabu mueleze .
Baaada ya kuwapata hao sasa ndo watakuwa wanakuhudumia kwa simu na kukutumia madawa pia nakushauri usitoe namba kwa watu wa karibu yako kama ambavyo mm hata unihonge kariakoo na posta sitoi wangu.
Nb : usije jisumbua inbox sijibu mimi sio tapeli niulize nkujibu hapa hapa
Good
 
Kuna mmoja yupo tabora ni mzuri sana, yeye anakufanyia kazi majibu unayaona kesho, Kuna mjinga mmoja nilimkopesha mil 1.7 akaanza kunizungusha pamoja na kwamba tuliandikishana kwa mwanasheria but ilipofika tarehe ya kulipa ulikua 20/January this year jamaa anasema hana pesa, kwenda kwa mwanasheria akaniambia nimuandikie barua nikimkumbusha deni pia nimuambie kuwa Nina nia ya kumshtaki baada ya siku saba nikafungue kesi mahakamani ambapo Hutu huyu mwanasheria ndo awe mtetezi na wakili wangu sasa nikapiga hesabu kama kuandikisha mkataba wa kukopeshana wakili alilamba laki je akinisimamia kesi si atanitoboa patefu pia muda utapotea basi nikampigia Huyo Fundi nikamueleza shida anasema nimuandalie chakula( pombe ) niende nazo usiku akapiga kazi akaniambia kesho asubuhi atakuletea pesa, nikamtoa ten, kesho saa12 asubuhi jamaa huyu hapa mlangoni ananiomba msamaha anasema ana mil1 inayobaki nimvumilie tarehe 5 February, nikabeba tarehe tano akaleta laki tatu, iliyobaki kaahidi tarehe 25 tena naifuata mwenyewe kwa mhasibu wake, pili Kuna jamaa yangu mmoja nilimpa ramani alikua ananiambia Kuna rafiki yake waliyeanza Maisha ya utafutaji sasa hivi yuko njema sasa kila akimuomba amkopeshe mil 5 jamaa anachomoa nilimpleka akafanyia kazi hadi aliondoka anachechemea, baada ya siku mbili nikaambiwa jamaa amenunua pump na machine Fulani za Mgodini sasa nilipomuuliza kama dili lilifanikiwa ananificha hadi Leo but najua alifanikiwa coz alikua hana hata mia mbovu hata gharama ya kwenda kwa mtaalam nilimchangia 20k but anamsifia sana fundi.
Toa ramani mkuu
 
Back
Top Bottom