Nina shida binafsi nahitaji mtu mwenye kujua mganga mzuri ambaye anasaidia watu au ata yeye amemsaidia please siihitaji ushauri wala matusi kama uzi haukuusu kaa kimya hapa nahitaji mwenye kujua hili jambo tu narudia usije hapa kama hauna huyo mtu
jambo unalolifanya ni kufuru kubwa sana, Mungu anakuona kila unachofanya na anahuzunika sana juu yako. Imagine, Mungu ndiye aliyekuumba (naamini wewe pia unaamini haujaumbwa na shetani wala wachawi, Mungu alikuumba), badala ya kumtegemea yeye, umegeukia kutegemea waganga wa kienyeji ukiamini ni wazuri. shetani hajawahi kuwa mzuri, hata akikupatia kitu jua mgongoni ameficha rungu, anakusogeza unone halafu akupige rungu moja tu ukafie huko hata kabla haujampa Yesu maisha yako, na ukifa utaenda moja kwa moja motoni. Shetani ni mwizi, anaiba vilivyo vya Mungu, anaiba watoto wa Mungu, na kila kitu, hawapendi wanadamu, anatamani wote wakaingie motoni, na anakutamani wewe ukaingie motoni. Yesu alisema shetani ni baba wa uongo, akija anakudanganya kukupenda na kukusaidia kwenye biashara, cheo au chochote, alivyo mwongo kumbe anakuvuzia akuteketeza ghafla kabla haujatubu na kumrudia Mungu.
Yohana 10:10 inasema,
Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele.
binafsi hayo mambo ya waganga nayajua sana, hata mali za kishetani hizo. hakuna mtua liyewahi kutajirika kwa utajiri wa kishetani mwisho wake ukawa mzuri, never. shetani hawezi kukupenda namna hiyo, mwisho wa siku huwa ni majuto tu, na ulishaukimbia uso wa Mungu unabaki na majuto na motoni utaenda. usimdharau Mungu kiasi hicho, anakuangalia akitegemea wewe ungemtumaini na kumwomba yeye, na wewe unaenda kutegemea waganga? unaenda kuomba kwa waganga? Mungu ameshindwa nini cha kukupatia hadi uende huko? dharau hii kweli Mungu anastahili kwa yote aliyokutendea? Unamdharau Mungu kwa wazi kabisa kwamba unaenda kutaka msaada kwa waganga wa kienyeji wakati Mungu yupo pale alitegemea wewe umwombe na kusaidie wewe unatukuza mashetani? kweli?
SASA UNA OPTION MBILI TU:
1. unatakiwa kuokoka, mpe Yesu Maisha yako, maadamu u haki, ni opportunity Mungu amekupatia, okoka leo, Mungu atakusaidia kwenye hayo unayopitia.
2. ukichagua kwa shetani, tegemea mambo mabaya sana mbele yako ambayo utakuja hapahapa kutoa ushuhuda, kama utapata neema ya kurudi tena, otherwise, shetani huwa anaua kwa ghafla, nimeshuhudia watu wanakufa ghafla hata wasipate nafasi kama hii uliyonayo leo, uchaguzi ni wako kwasababu utakula matunda ya kila unachoamua kuchagua. Mungu akuneemie.