2Laws
Member
- Sep 4, 2022
- 37
- 38
Tazama;
- Tunashuhudia matukio ya kikatili yakiendelea hapa nchini,
-
picha toka mtandaoni ya mwanafunzi aliyechomwa mikono.
- Tumeshuhudia idadi kubwa ya vijana kupotea ama kufanyiwa ukatili ama kuondolewa baadhi ya viungo vyao sababu ya pesa,
- Tumeshuhudia kesi za ubakaji na ulawiti wa watoto zikiendelea,
- Tunaona watu wakiendelea kuua bila woga na kuumizana kwa sababu ya vitu vinavyoweza kupuuziwa,
- Tunaona viongozi wakipuuza haki za wananchi wao,
- " Kwa mujibu wa Takwimu za Jeshi la Polisi Tanzania, katika kipindi cha Januari hadi Desemba, 2021 jumla ya matukio 11,499 ya ukatili dhidi ya watoto yalitolewa taarifa katika vituo mbalimbali vya Polisi. Mikoa iliyoongoza ilikuwa ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Mkoa wa Kipolisi Ilala (489). Aidha, Makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114)." Mwaka huu kuna dalili za kuweka rekodi mpya
- swali, kosa liko wapi? ni nani hawajibiki ipasavyo? hata tumekua na wingi wa watu wa namna hii katika jamii?