Wapi wanatoa mkopo kwa dhamana ya vyeti?

Uchunjuba Punjubi

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
799
Reaction score
622
Wakuu,

Nataka kujua wapi wanaweza kumpa mtu mkopo kwa dhamana ya kuweka vyeti vyake iwe cha O-level, Advance, Chuo au vyote kwa pamoja.

Kutokana na hili janga la ajira kutopatikana wasomi wengi tunajikuta tunatunza vyeti kwenye mabegi bila kuwa na faida yeyote na muda unaenda. Ikipatikana sehemu kama hiyo nahisi itanisaidia mimi na wengine pia.
 
Nasikitika kusema kwamba hakuna taasisi inayofanya hivyo
 
hahah jaman me nimewah kuwaza had nikafika mwisho , nahc pia nimeshapita kiwango chako cha kufikiria ila na shukuru Mungu hapa nilipo fikia , cjui kama kuna hii kitu ngoja wadau waje,
 
Hakika inasadifu hivyo vyeti vyako bila kujali ulivipataje havina maana yoyote. Hivi mathalani ndo unaongoza taasisi ya mikopo sijui itajiendeshaje, yaani mtu aki default kulipa unauza vyeti ili kurejesha pesa ama?
Mtaji wa kwanza ni mawazo kama umeshindwa kufikiri basi mtaji mwingine tumia nguvu za mwili.
 
Kwa vyeti unakopeshwa mwisho Tsh200,000 kama upo Dar nicheki.
Mimi nipo mbeya nina cheti cha chuo kikuu. Vipi haijalishi masomo niliyosoma?
Naweza kuja Dar! Hali ni ngumu.




Yaani ingewezekana serikali nayo ingesaidia kuunda taasisi ya mikopo kwa dhamana ya vyeti.
 
Ukipapata uniambie na mm nkatoe chet Chang cha form 4 dvn 4 ya 33.nawaachia chote kabsa mm skitaki kama ni kuuza wauze tuu
 
 
Hakuna mtaji wa mawazo bali mtaji ni pesa. Watu wana mawazo mazuri sana lkn hakuna pesa ya kufanikisha mawazo yao.
N:B
Mawazo na mtaji ni vitu viwili tofauti.
1. Mawazo ni mtaji?
2. Mtaji ni mawazo?
Hayo maswali mawili huwezi kujibu utaishia kudanganya watu.
 
Mtoa mada sijui kama umeandika hii thread kwa uhalisia au kwa utani.. lakini nikusaidie zipo banks na some financial institutions ambazo hutoa mtaji kwa graduates ambao wanakuwa na mawazo mazuri ya biashara.. ukiwa na wazo zuri wao hukufinance ili ufanikiwe ili nao baadae waweze faidika.. i'll go deep baada ya game ya taifa kwisha..
 
Kwenye suala la pesa/mkopo vyeti vya taaluma au shule kama dhamana ni useless...

Vyeti vyenye tija ni kama- hati ya nyumba, kadi ya gari, hati ya kiwanja au shamba ambavyo hata asiyeenda shule akiwa navyo anajipatia mkopo...


Cc: mahondaw
Useless kabisa mkuu, kuna graduate amewah kuniachia vyeti kwa mwaka. Tena nikagaeuka kuwa mlinzi wa vyeti vyake maana vikipotea ni tatzo kubwa.
 
mkuu haupo sawa kabisa mtaji unaweza kuwa fedha au wazo Kwa hali ya kawaida utaona sio sawa ila kiujasiriamali hilo lipo sawa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…