Wapi wanatoa mkopo kwa dhamana ya vyeti?

Wapi wanatoa mkopo kwa dhamana ya vyeti?

wanafunzi bumu lao wanaendea disco,hawafikiri chochote kuhusu biashara akimaliza chuo akikosa kazi ndio anaanza kufikiria kujiajiri lazima ukose mtaji ila ukianza na mawazo ya biashara muda mrefu unaweza anza na mtaji wowote ulio na uwezo nao!
Mtu unapata laki mbili ya hamsini kwa mwezi na bado unataka apate mtaji..kuweni serious bhana..hio ni hela ya kujikimu tu..
 
Hakika inasadifu hivyo vyeti vyako bila kujali ulivipataje havina maana yoyote. Hivi mathalani ndo unaongoza taasisi ya mikopo sijui itajiendeshaje, yaani mtu aki default kulipa unauza vyeti ili kurejesha pesa ama?
Mtaji wa kwanza ni mawazo kama umeshindwa kufikiri basi mtaji mwingine tumia nguvu za mwili.
Mkuu sio kila mtu vyeti vyake hana uchungu navyo, yaani vyeti nivihangaikie kwa miaka kadhaa na pesa nyingi eti leo nije kuvitelekeza kwa 2 au 3 millions? Serious? Mtu anakuwa na uhakika na kile anachotaka kufanya na anajua atarudisha kwa muda muafaka.
 
TALA ndo wapi huko mkuu
hio ni campuni ya kutoa mikopo nahisi ipo kenya ila inatoa mikopo online utaweka kitambulisho na picha alafu maswali yao ukifanikiwa hapo mkwanja unazama Kwa simu yako kiasi ulichoomba ila kumbuka huwezi watoroka maana uliacha picha na kitambulisho chako pamoja na ile barcode
 
Wakuu,

Nataka kujua wapi wanaweza kumpa mtu mkopo kwa dhamana ya kuweka vyeti vyake iwe cha O-level, Advance, Chuo au vyote kwa pamoja.

Kutokana na hili janga la ajira kutopatikana wasomi wengi tunajikuta tunatunza vyeti kwenye mabegi bila kuwa na faida yeyote na muda unaenda. Ikipatikana sehemu kama hiyo nahisi itanisaidia mimi na wengine pia.
Unahitaji mkopo wa kiasi gani?
 
Back
Top Bottom