Wapi wanatoa mkopo kwa dhamana ya vyeti?

Wapi wanatoa mkopo kwa dhamana ya vyeti?

mkuu haupo sawa kabisa mtaji unaweza kuwa fedha au wazo Kwa hali ya kawaida utaona sio sawa ila kiujasiriamali hilo lipo sawa kabisa
Sawa fanya ufanyavyo lkn pesa ndiyo kila kitu.
Ni biashara gani utaifanya bila kuwa na pesa na ukafanikiwa?
 
Kwenye suala la pesa/mkopo vyeti vya taaluma au shule kama dhamana ni useless...

Vyeti vyenye tija ni kama- hati ya nyumba, kadi ya gari, hati ya kiwanja au shamba ambavyo hata asiyeenda shule akiwa navyo anajipatia mkopo...

Cc: mahondaw
Hapo ndio tunapoona kuwa mfumo wetu wa elimu uliojikita kwenye utoaji wa vyeti badala ya maarifa usivyo na faida kwa taifa letu!
 
Mkuu benki au taasis gani hizo?

Wewe ulishawahi kwenda kujaribu au umesikia kutoka wa watu au wanasiasa?
Mtoa mada sijui kama umeandika hii thread kwa uhalisia au kwa utani.. lakini nikusaidie zipo banks na some financial institutions ambazo hutoa mtaji kwa graduates ambao wanakuwa na mawazo mazuri ya biashara.. ukiwa na wazo zuri wao hukufinance ili ufanikiwe ili nao baadae waweze faidika.. i'll go deep baada ya game ya taifa kwisha..
 
Hakuna mtaji wa mawazo bali mtaji ni pesa. Watu wana mawazo mazuri sana lkn hakuna pesa ya kufanikisha mawazo yao.
N:B
Mawazo na mtaji ni vitu viwili tofauti.
1. Mawazo ni mtaji?
2. Mtaji ni mawazo?
Hayo maswali mawili huwezi kujibu utaishia kudanganya watu.
Hivi unajua thamani ya wazo bora la biashara, unafikiri kwanini kuna taasisi zenyewe zinahitaji business proposal ili zitoe funds kwaajili ya mradi husika? Mtu aliypata pesa kwa namna hiyo akaendesha mradi wake kwa mafanikio, je unadhani mtaji wake ulikuwa pesa ama mawazo bora?
 
Tunza vyeti vyako sehemu salama. Niliwahi kupitiliza kuwaza kwenye level yako juu ya vyeti, yaani nilifikia hatua ya kutaka kuvichana na kuvichoma vyeti baada ya kila aina ya mbinu niliyokuwa najaribu kuitumia nijikwamue kushindikna. Niliona kabisa elimu niliyokuwa nimepata ya chuo cha kati haikuwa na msaada kwangu, hivyo vyeti ni mzingo. Ilibaki kidogo tu nivichome...ghafla, alifika mtoto wa mzee wa mtaa aliyekuwa anamiliki sanduku la barua...alinikabidhi bahasha ya kaki iliyokuwa inanihitaji kwenda kwenye usaili wa kazi...!Na ilisisitiza niende na vyeti orijino....mwili wote wa kwangu ulitetemeka...nilivyowaza nilichokuwa naelekea kufanya dhidi ya vyeti vyangu....

Kazi nilipata..na ilinifungulia milango mingine ya kazi bora zaidi na ya maslahi ya kuridhisha.

Narudia tunza vyeti vyako sehemu salama.
 
Hivi unajua thamani ya wazo bora la biashara, unafikiri kwanini kuna taasisi zenyewe zinahitaji business proposal ili zitoe funds kwaajili ya mradi husika? Mtu aliypata pesa kwa namna hiyo akaendesha mradi wake kwa mafanikio, je unadhani mtaji wake ulikuwa pesa ama mawazo bora?
Mtaji wake ni pesa sbb bila pesa huwezi kutekeleza mawazo yako mazuri.
1.Km mtaji wako siyo pesa kwann uandike proposal halafu upeleke kwenye taasisi fulan ukapewe pesa?
2.Kwann hayo mawazo mazuri usiyatumie kufanyia biashara bila ya pesa?
N:B
Fanya ufanyavyo pesa ndiyo mtaji na pia Fedha ina control hata mawazo yako mazuri ya biashara
 
Mimi nipo mbeya nina cheti cha chuo kikuu. Vipi haijalishi masomo niliyosoma?
Naweza kuja Dar! Hali ni ngumu.

Yaani ingewezekana serikali nayo ingesaidia kuunda taasisi ya mikopo kwa dhamana ya vyeti.
mbeya-dsm ukafate laki 2?!!

ukienda ukirudi imebaki laki[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Hakuna mtaji wa mawazo bali mtaji ni pesa. Watu wana mawazo mazuri sana lkn hakuna pesa ya kufanikisha mawazo yao.
N:B
Mawazo na mtaji ni vitu viwili tofauti.
1. Mawazo ni mtaji?
2. Mtaji ni mawazo?
Hayo maswali mawili huwezi kujibu utaishia kudanganya watu.
wanafunzi bumu lao wanaendea disco,hawafikiri chochote kuhusu biashara akimaliza chuo akikosa kazi ndio anaanza kufikiria kujiajiri lazima ukose mtaji ila ukianza na mawazo ya biashara muda mrefu unaweza anza na mtaji wowote ulio na uwezo nao!
 
1.Ww umesoma chuo?
2.Km ulisoma, bumu lako ulikuwa unafanyia nini?
 
USIPOLIPAHUO MKOPO MKOPESHAJI ATAPATA HELA YAKE KWA KUTUMIA VYETI VYAKO,MAANA LENGO LA COLATERAL NI ILI MKOPESHAJI AUZE ILI APATE CHAKE PALE UNAPOZINGUA KUREJESHA, AU ATAKUUZA WEWE MKUU
 
USIPOLIPAHUO MKOPO MKOPESHAJI ATAPATA HELA YAKE KWA KUTUMIA VYETI VYAKO,MAANA LENGO LA COLATERAL NI ILI MKOPESHAJI AUZE ILI APATE CHAKE PALE UNAPOZINGUA KUREJESHA, AU ATAKUUZA WEWE MKUU
 
Mtoa mada sijui kama umeandika hii thread kwa uhalisia au kwa utani.. lakini nikusaidie zipo banks na some financial institutions ambazo hutoa mtaji kwa graduates ambao wanakuwa na mawazo mazuri ya biashara.. ukiwa na wazo zuri wao hukufinance ili ufanikiwe ili nao baadae waweze faidika.. i'll go deep baada ya game ya taifa kwisha..
Bank gani au financial institution ipi? Hizo ni nadharia. Kupata mkopo kwenye mabenki yetu ni kazi. Kama huna dhamana basi uwe mtumishi. Mwenye wazo la biashara utasubiri sana.
 
Back
Top Bottom