On contrary hao jamaa ni wa muhimu pia endapo wakiwekewa utaratibu mzuri.
Mimi pale ubungo kila nikienda kukata tiketi naongozana na mmoja mpaka ofisi ya basi naloenda kukakata tiketi.sio kwamba ofisi siijui no! Ila waliniambia wakipeleka mtu mmoja basi anapewa buku naye anasogesha maisha. Hivyo huwa siwakatai japokuwa sijui kama kuna wezi na matapeli kati yao
Wewe una moyo wa kusaidia pia ni mwerevu pia unaishi maisha mazuri na yenye amani
Binafsi huwa sipendi usumbufu, maana nilikutana nao wawili kila mmoja kwa wakati na sehemu tofauti
Mmoja nilikutana nae Tanga,
huyu jamaa alikua ni mstaarabu sana maana nilikua na mizigo pia nilikua naongozana na mzee 80yrs, mbaya zaidi nilikua nimevunjika mkono, pia nilikuta watu kibao wanasubiri dala dala ya mwisho kuelekea pangani, jamaa alichokifanya dala dala ilipofika tu akawahi kunikamatia siti mbili nikamlipa buku ilikua 2014 huko, jamaa akaniambia, akaniomba nimuonge nikamwambia hapa nimebaki na nauli tu
Akaniambia, "Poa naamini siku nyingine tukionana utanipa"
Nami nikamjibu, "Poa"
Baadae ikawa kila nikitembelea Tanga nikawa najaribu kupepesa macho pale nimtoe japo 10k sikuwahi kumuona
Kuna mwingine huyu wa Ubungo,
Nadhani huyu ndo kasababisha nimejikuta nawachukia hawa jamaa, yaani basi ninaloenda kupanda nalijua lakini jamaa ananifata tu afu nikakata tiketi nataka kuingia kwenye basi ananidai buku la kunipeleka nikamwangalia hadi akajishtukia akaondoka kimya kimya
Sa hv huwa nawaambia tu, "nimeshafanya Booking tayari" nikiwajibu hivyo hawanifati
Kuna baadhi ni wastaarabu na waelewa ila wengine wanakera sana