Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,561
- 24,428
WATU WA ARUSHA TANGA UPARENI NAO WAJENGEWE STAND YA KWAO WANAPATA SHIDA SANA
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...Ndipo na Mimi ninaposhangaaHao so ndio wanyonge alioongea bwana mkubwa.
Machinga mna balaa sanaumepanick [emoji2]
Wapiga debe 30 wamekamatwa katika Kituo cha Mabasi cha Magufuli kilichozinduliwa siku mbili zilizopita na Rais John Magufuli.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Februari 26,2021 Meneja wa kituo hicho, Maira Mkama amesema wapiga debe waliokuwa Ubungo, Riverside na Mbezi wamevamia na kusababisha usumbufu kwa abiria.
"Leo tumeanza operesheni ya kuwakamata, hadi kufikia saa nne tumewakamata wapiga debe zaidi ya 30 na hapa Mbezi palikuwa na wapiga debe zaidi ya 100 bado waliokuwa Ubungo na wengine Riveside wote waliposikia kinafunguliwa wamevamia huku ndani,"amesema
Mkama amesema wameliomba Jeshi la polisi Kanda Maalum kuongeza askari na gari kwaajili ya doria ili kuwakamata wapiga debe watakaoendelea na shughuli hiyo.
Amesema wapiga debe hao wanasababisha usumbufu kwa abiria pamoja na kuhatarisha usalama wao hivyo viongozi wa kituo hicho watashirikiana na wamiliki wa mabasi kuangalia hatua za kuzichukua ili kuwaondoa wapiga debe.
Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua) Maulid Masalu amesema wanaweza kutoa ushauri lakini Serikali ndiyo yenye mkakati wa kuwaondoa wapigadebe.
"Hawa wapigadebe hawapo ndani ya stendi hii tu, wapo kuanzia stendi ya daladala wakati abiria anaposhushwa wanamvamia na kusababaisha usalama wake kuwa ndogo,"amesema Masalu.
Chanzo: Mwananchi
Kabisa mkuu manake hao wapiga debe wa Riverside walikuwa wanadalalia abiria waliokuwa wanaenda kupanda mabasi hapo ibungo Sasa kituo kimeamishiwa mbezi so lazima na wao wahame...Ndipo na Mimi ninaposhangaa
Si ndio alisema hawa boda bofa na mama na baba ntilie ni wanyonge wake wasifukuzwe stendi hapo.
Sasa hawa wapiga debe si nao wanatafuta tu kipato chao halali hapo kwa kuwabughudhi Abiria! Si nao wapi kundi LA wanyonge na waachwe ili kupata riziki zao??
Aah unazingua mkuu nao ndio fursa yao hiyo...Ninashauri hao wapigadebe wote 30 waishie jela, na huko jela wakafundishwe kulima na wakirudi waelekee vijijini wakalime.
Ongea ila shukuru Mungu hayajakukuta
Au unadhani mpiga debe anapenda lile lyf
Waende
wap
Huyo meneja wa stendi ajiandae.akisikia mkulu.Mtetezi wa wanyonge hajasikia?
Wewe una moyo wa kusaidia pia ni mwerevu pia unaishi maisha mazuri na yenye amaniOn contrary hao jamaa ni wa muhimu pia endapo wakiwekewa utaratibu mzuri.
Mimi pale ubungo kila nikienda kukata tiketi naongozana na mmoja mpaka ofisi ya basi naloenda kukakata tiketi.sio kwamba ofisi siijui no! Ila waliniambia wakipeleka mtu mmoja basi anapewa buku naye anasogesha maisha. Hivyo huwa siwakatai japokuwa sijui kama kuna wezi na matapeli kati yao