LGE2024 Wapiga Kura Dodoma ni kama wamegoma kujiandikisha, Waandikishaji wameamua kuwafuata nyumbani na kazini ili wajiandikishe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Your browser is not able to display this video.
Hali ya uandikishaji wenye Daftari la Kupiga Kura kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mtaa siyo rafiki, imefikia hatua baadhi ya Waandikishaji wameamua kuingia mtaani kuwatafuta Wananchi ili wajiandikishe.

Hapa Dodoma nimeshuhudia hali hiyo ikijitokeza kwenye Mitaa ya Chinangali West na Nkuhungu, sijajua kwa nini lakini kwa ufupi raia hawajitokezi na kinachotokea wanaamua kuwafuata Wapiga Kura kwenye maduka, bodaboda, nyumbani na sehemu nyingine nyingi.
 
Mbona tunalimishana kujiandikisha. Kama mmeshindwa kuwashawishi wananchi kwa uchaguzi wa haki, uhuru, amani na huduma bora. Usitegemee ukimfuatq nyumbani au kazini ndiyo atajiandikisha. Serikali ijitafakari.
 
Siku yabkupiga kura watawafuata nyumbani wakapigie kura vyumbani kwao?
 
Nilkuwa naomba kuuliza!
Hivi kwa sheria za Uchaguzi inaruhusiwa Mwandikishaji kuacha kituo na kwenda kusaka watu wajiandikishe?
Kwa vile CCM haina aibu kule mitaani wataandikisha hata majina ya marehemu!
 
Mkuu walikulazimisha kutoa taarifa zako au..?
Nilikua natoka kazini sasa nikapita njia ya karibu ya serikali ya mtaa weee nikaitwaa kwa sauti njoooo. Kuangalia kwambalia namuona mwenyekiti wacha wanichangamkie kuandika jina.😠😠
 
2019 wakitumia FFU, wakurugenzi na watendaji Jafo aliutangazia ulimwengu kuwa CCM imeputa bila kupingwa.

Watu hawajiandikishi na waliojiandikisha hawapigi kura ili kuwarahisishia CCM michakato ya ushindi.
 
Sio poa! Juzi jamaa walitufwata adi kwenye tungi tujiandikishe.
 
Kauli ya Nape nadhani inachangia na kutia uvivu sana "matokeo ya uchaguz yanategemea nani anasimamia"
 
Kwa ka clip haka hakasibitishi unachokisema.

Weka clip mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…