Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo msamvu au pangaledi safari trans. Hizi ni za kwetu za kuingilia vijijini mkuu. Hazipo hapo kwenye msafara wa Abood,BM,Alside ...Kisua wako wapi
Hata Hotel ya Morena mbaya? Au ile ya ABC?Kitu ambacho kimewashinda morogoro ni hotel nzuri na chakula kizuri kwa abiria wanaokula Morogoro.
Lukobe kisima maji unapata na utapata faida ya kuyauza kwa wengine.Lukobe qni
lukobe lukobe mbona kama kukavu sana, ukijichimba kisima unapata maji?
Huu u panic buyer ni kama umenisema mimi!Natanguliza pole kwa wote waliolishwa mbwa hapo nje ya stand Msamvu. Nimefanikiwa kukagua eneo liko swari na kuna kijana anauza mishkaki halali ya nyama inayosadikiwa kuwa ya ng'ombe. Ila nilibaki na swali tu, ikiwa moro wametafuna mbwa hivyo sio zaidi Dar ambako watu wanakula hovyo vimishikaki kwenye chelewa na vindizi vya kuchoma?
Turudi madani
Aisee hii ni zaidi ya mara ya 20 napita hapa 'msamvu' hawa wakaribishaji sijawahi kuwaona stand yoyote nchini. Wanabidii ya ushawishi na hawakati tamaa kirahisi.
1: Hata kama sura wengine ni za kiteja kidogo lakini wanalugha nzuri, yakiungwana.
2: Waongo sana, ila wanavyokushawishi kwa uongo utapenda. " Nimewahi panda BM naambiwa ina "Maliwato ndani". Jamaa nikamkaba twende nihakikishe alikuwa na ujasiri wa kutoka nje hadi mlangoni mwa Bus, kwa ujasiri na ushawishi ule nikamwambia basi sawa kuingia hakuna cha maliwato wala maliwata. Ila Yenye maliwato huwa ipo.
3: Hii tabia ya ucustomer care wameambukizana wahudumu wote. Wale wa msosi, tax, machinga, kila mtu yuko active kupitiliza.
Nimewahi kufika stand nyingi, ila msamvu nawakubali sana kuliko hata mbezi mwisho ambako watu wanakomaa kidogo tu anakata tamaa na kutafuta mtu mwingine. Kwa sababu ya usanii mwingi ambao wamenifanyia kwa kuwaamini japo siwalaumu nimewawekea formula kali sana kiasi kwamba hawanisumbui tena bila idhini yangu.
Leo walipojua nahitaji kuchaji, nimepelekwa siti ya mbele ya kosta ya kwenda wilayanu nikaletewa na usb cable nikaunganishwa kwenye radio ili niendelee kula JF. Kuuliza wenzagu wamo tangu saa nne, mimi naambiwa dakk 15 kwa heshima yangu wataondoka ingawa tumeondoka baada ya saa. Wanasema hali mbaya sana leo.
Hawa jamaa wako vzri aisee, ndio maana wanalisha watu mbwa, watu wanauziwa nazi za kuoza, powerbank zenye 0 charging capacity, battery mpya za simu ambazo hazijai na bado watu wanatoa pesa. Hasa wale panic buyers.
[emoji16][emoji16][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23]!Umenikumbusha hapo Moro sitapasahau,walinipandisha cost kwenda Mbeya.waniliniambia bro kuna basi kubwa linatokea Tanga walienda msibani,sasa kuna siti mbili.hiyo haina kusimama popote so utawahi kufika Mbeya. Baada ya kuelewana nao,si nikaacha mabasi yote yakapita,kuja kutahamaki ni ki costa flan hiv ambacho kinafanya dala dala pale mbeya wao huita mzunguko ndiyo kimefika kweli kutoka Tanga kupeleka msiba.
Sina jinsi,muda umeenda na lazima niende.wakaniingiza humo,na wao wakavuta chao.nilikuja jua nimejichanga baada ya kuondoka hapo stendi na kunote speed yake.safari ya mbeya ilikuwa ndefu saana kiwahi kutokea
Utakapo jua tabia za waluguru utajua huijui MoroWatu wa morogoro ni wakarimu sana, ni moja ya sehemu ambazo natamani kuja kuzeekea.
ya morena si mpya..alafu.hizo ni za wamiliki wa mabasi, shabiby na abcHata Hotel ya Morena mbaya? Au ile ya ABC?
kweli kabisa,Wananchi wa Morogoro ni tegemezi kwa Dsm.
Nadhani hii ndo sababu kubwa ya huu mji kuwa slow kwenye maendeleo.
Mtu akitaka kufanya shopping ya laki mbili husafiri kwenda kufanyia Dar.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
ja!Utakapo jua tabia za waluguru utajua huijui Moro
Tena kipindi cha mvua ni hatariLile dongo jekundu loh, dakika mbili umechafuka
Mkuu 60×60 Mkundi, Kiegea naweza kupata kwa Sh ngapi ?Forest kwa moto sana mkuu maana kule ndio makao ya mkoa sijawahi hata uliza bei za kule. Kwa sasa naweza kukushauri utafute Lukobe, Mkundi, Kiegea na Bigwa.
Kijiji gani mkuu?Morogoro napapenda sana kuna ukarimu wa ajabu.
Niliwahi kukodi mashamba kwa mama mmoja hivi nilikuwa nikienda shambani kwa sababu ilikuwa kijijini sana ukilala pale mama anakuachia chumba chake anaenda kulala na wajukuu.
Na mimi nikawa nabeba mazaga yote ya mjini nampelekea.
Ila ndiyo hivyo nilishapoteza mawasiliano nae.[emoji2297]
Hiyo ilikuwa zamani mkuu wa not now.... Halafu hata mtu akihitaji kitu from Dar au Zanzibar watu wanaagiza tuu kwa mitandao na unapokea ofisi ya ABOOD Bus mbona?Wananchi wa Morogoro ni tegemezi kwa Dsm.
Nadhani hii ndo sababu kubwa ya huu mji kuwa slow kwenye maendeleo.
Mtu akitaka kufanya shopping ya laki mbili husafiri kwenda kufanyia Dar.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
MagubikeKijiji gani mkuu?
Still utegemezi wao kwa Dar unabakia.Hiyo ilikuwa zamani mkuu wa not now.... Halafu hata mtu akihitaji kitu from Dar au Zanzibar watu wanaagiza tuu kwa mitandao na unapokea ofisi ya ABOOD Bus mbona?
Hicho ndio kinaniudhi Morogoro na sipapendi kwa ajili hio japo nimekulia hapoLile dongo jekundu loh, dakika mbili umechafuka
Hahahha eti shamba darasaaHuu u panic buyer ni kama umenisema mimi!
Niliwahi kulizwa hiyo power bank pale Ubungo stand, lakini nikachukulia kitendo hicho kama 'shambadarasa'.