Wapigadebe Stendi ya Msamvu wana ushawishi kuliko wa stendi zote nchini

Haha Morogoro! Sitosahau siku naenda Mbeya nawaambia nahitaji bus fulani naambiwa Dada hilo bus siyo zuri na mtachelewa kufika sana panda hili linaondoka sahivi,aah sijui tu nikajikuta nabadilisha maamuzi aisee kilichotokea Mbeya tulifika usiku mnene bus bayaa speed hamna! Ila ahsanten kwa ukarimu wenu watu wa Moro.๐Ÿ˜€๐Ÿ‘
 
Kuna jamaa alinikomalia bro, twende angalau nipate Buku. Nikasema poa, ila masharti Bus liwe na USB port. Maana default usafiri wangu abood nimepeleleza hazifanyi kazi.

Jamaa kwa ujasiri ananipeleka kwenye Bus la BM ambalo haliendi popote. Mwenzake ananicheka na mimi nacheka kwa sababu nilitaka kuona mwisho wake. Baadae akaona noma, ilikuwa saa moja jioni. Ikabidi niingie abood yule jamaa tukaagana vzr hata haibu hana, ila ni mtu mwema tu
 
Kakupeleka kwenye Bus ambalo haliendi popote๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ aisee alitisha sana, hilo buku alipata sasa๐Ÿ™Œ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ