Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Binadamu alivyoimbwa ni tofauti na wanyama wengi anaowatawala maishani mwake kila siku. Anao uwezo wa kuificha ile hulka yake ya ndani kabisa akacheka kwa bashasha na uchangamfu na usiweze hata kidogo kuitambia nia yake ya ndani. Huwa natizama vile vipindi vya matukio ya maisha ya wamarekani wanaitwa ID (Investigation Discovery) na sura zote za wale wauwaji makatili mara nyingi ni zile zilizozoeleka kuonekana makanisani tena zikiwa zimekaa viti vya mbele kabisa.
Zimeimbwa nyimbo nyingi ni wanamuziki mbalimbali kuelezea hizi sura mbili za mwanadamu na namna anavyoweza kuuma na kupuliza akiwa ni sehemu muhimu ya jamii inayomzunguka. Binadamu ni kiumbe mwenye uwezo wa kuificha nia yake na anayemzunguka wala asiweze kufahamu anawaza nini na kwa muda gani. Simba, Fisi, Kima, Chui na hata hawa paka na panya walio karibu zaidi na binadamu huwa hawana uwezo wa kuficha kusudio lao wanapokuwa mbele ya macho yetu. Wapo wazi na ukiwaona tu unajua wanachotaka kukifanya ni kipi.
Nimejikuta nikiwa katika tafakari hii baada ya kukumbuka ahadi aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana siku ya Mei Mosi pale Kirumba Stadium Mwanza. Aliahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi akitumia maneno ya kingereza 'package'. Wafanyakazi wa serikali kwa sasa wanaisubiri kwa hamu hiyo package yao mpya ambayo kwa kawaida huambatana na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa za kila siku.
Ni hawa hawa wanaoisubiri hiyo package mpya waliojawa na ufundi wa kuchora michoro ya wizi wa mapesa. Kibaya zaidi huwa wanaiba mabilioni ya shilingi za waajiri wao. Ni hawa hawa wanaotengeneza stika feki pale Uhamiaji ndio wanaopita na mabango ya kudai nyongeza za mishahara wakati wa yale maandamano maarufu ya Mei Mosi ya viwanjani. Ni hawa hawa ambao CAG anawapa hati ya chafu baada ya kugundua wizi uliokubuhu ndio wenye ushujaa wa kubeba mabango ya kudai malipo mazuri zaidi.
Ni hawa hawa wafanyakazi wenye uaminifu karibu na zero, ndio wanaoanzisha nyuzi za kuponda awamu za serikali iwapo wanaoona mishahara yao haipandishwi. Wanataka wapewe kikubwa na mwajiri wakati huo hawana sifa ya maana sana ya kuwa nayo, ile ya uaminifu kwa mali ya umma. Ni hawa hawa wabeba mabango wanaonuna wanaposikia mwaka huu kutakuwa hakuna nyongeza ya mshahara wenye maarifa ya kutengeneza michoro ya mishahara hewa inayokwenda mpaka kufikia pensheni hewa wakati huyo mwajiriwa hewa anapokuwa amestaafu.
CAG anawaumbua sana wafanyakazi wa sekta mbalimbali kila mwaka na hawachoki kudai nyongeza ambalo kwa kweli ni jasho lao. Pesa zinazoingia mifukoni mwa watu kwa maana ya wizi ni nyingi kulinganisha na zile zinazotumika katika kuongeza mishahara ya wafanyakazi nchi nzima.
Uaminifu ni mtihani mkubwa kwa watanzania. Mahubiri yale maarufu ya wachungaji, mashekhe na mapadre yanajikita katika kuupiga vita ubinafsi mimi naamini kingine cha kupigwa vita ni ukosefu wa uaminifu kwani unayo hatari ya kuleta mgawanyiko wa kijamii.
Siku zote huwa chanzo kikubwa sana cha malalamiko haswa kutoka watu wa tabaka la chini.