Wapigaji na wezi wa mashirika ya Umma wanaposubiri kupandishiwa mishahara yao Mei Mosi

Wanyonge washamba sana. Wewe philipo na wenzako mnasumbuliwa na ujinga.
1. Juni 2021 mama alipandisha vyeo watumish karibia 80 elfu

2. Mei 2022 watumish laki 1 kasoro watapanda vyeo.

Mama ana roho nzuri sana.

Ngoja niende nmb kuchukua m7 nimalizie hekalu langu.

Wachawi ***** zenu
Mwalimu unajenga hekalu? Labda hekalu la tope
Alafu tulishasema humu walimu sio watumishi wa umma, Bali walimu ni watawa.

Watumishi wa umma wapo Ega, TRA, BOT, EWURA, TCRA, TMDA, WCF, NSSF, TPA, N.K na kamwe walio humo hawawezi kuandika comment kama yako.
 
Uache kufuatilia yasiyokuhusu. Cag, pccb na usalama wa taifa wanajua majukum yako.

Wewe mwenyewe unalelewa na huyo nesi.

Acha roho mbaya ya kishwetani. Hata hivyo wanaoumia ni sekta binafsi. Huku kwa mama samia mikataba ni permanet anda pensionable.

Ongeza juhudi za kulipa kodi uwatunze watumish hadi watakapokufa.
Ww jamaa kazi ya ualimu sio ya kuja kujitutumua mbele za watu. Unatia aibu kabisa

Alafu tulishasema humu kuwa walimu sio watumishi wa umma
 
Binadamu alivyoimbwa ni tofauti na wanyama wengi anaowatawala maishani mwake kila siku. Anao uwezo wa kuificha ile hulka yake ya ndani kabisa akacheka kwa bashasha na uchangamfu na usiweze hata kidogo kuitambia nia yake ya ndani. Huwa natizama vile vipindi vya matukio ya maisha ya wamarekani wanaitwa ID (Investigation Discovery) na sura zote za wale wauwaji makatili mara nyingi ni zile zilizozoeleka kuonekana makanisani tena zikiwa zimekaa viti vya mbele kabisa.

Zimeimbwa nyimbo nyingi ni wanamuziki mbalimbali kuelezea hizi sura mbili za mwanadamu na namna anavyoweza kuuma na kupuliza akiwa ni sehemu muhimu ya jamii inayomzunguka. Binadamu ni kiumbe mwenye uwezo wa kuificha nia yake na anayemzunguka wala asiweze kufahamu anawaza nini na kwa muda gani. Simba, Fisi, Kima, Chui na hata hawa paka na panya walio karibu zaidi na binadamu huwa hawana uwezo wa kuficha kusudio lao wanapokuwa mbele ya macho yetu. Wapo wazi na ukiwaona tu unajua wanachotaka kukifanya ni kipi.

Nimejikuta nikiwa katika tafakari hii baada ya kukumbuka ahadi aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana siku ya Mei Mosi pale Kirumba Stadium Mwanza. Aliahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi akitumia maneno ya kingereza 'package'. Wafanyakazi wa serikali kwa sasa wanaisubiri kwa hamu hiyo package yao mpya ambayo kwa kawaida huambatana na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa za kila siku.

Ni hawa hawa wanaoisubiri hiyo package mpya waliojawa na ufundi wa kuchora michoro ya wizi wa mapesa. Kibaya zaidi huwa wanaiba mabilioni ya shilingi za waajiri wao. Ni hawa hawa wanaotengeneza stika feki pale Uhamiaji ndio wanaopita na mabango ya kudai nyongeza za mishahara wakati wa yale maandamano maarufu ya Mei Mosi ya viwanjani. Ni hawa hawa ambao CAG anawapa hati ya chafu baada ya kugundua wizi uliokubuhu ndio wenye ushujaa wa kubeba mabango ya kudai malipo mazuri zaidi.

Ni hawa hawa wafanyakazi wenye uaminifu karibu na zero, ndio wanaoanzisha nyuzi za kuponda awamu za serikali iwapo wanaoona mishahara yao haipandishwi. Wanataka wapewe kikubwa na mwajiri wakati huo hawana sifa ya maana sana ya kuwa nayo, ile ya uaminifu kwa mali ya umma. Ni hawa hawa wabeba mabango wanaonuna wanaposikia mwaka huu kutakuwa hakuna nyongeza ya mshahara wenye maarifa ya kutengeneza michoro ya mishahara hewa inayokwenda mpaka kufikia pensheni hewa wakati huyo mwajiriwa hewa anapokuwa amestaafu.

CAG anawaumbua sana wafanyakazi wa sekta mbalimbali kila mwaka na hawachoki kudai nyongeza ambalo kwa kweli ni jasho lao. Pesa zinazoingia mifukoni mwa watu kwa maana ya wizi ni nyingi kulinganisha na zile zinazotumika katika kuongeza mishahara ya wafanyakazi nchi nzima.

Uaminifu ni mtihani mkubwa kwa watanzania. Mahubiri yale maarufu ya wachungaji, mashekhe na mapadre yanajikita katika kuupiga vita ubinafsi mimi naamini kingine cha kupigwa vita ni ukosefu wa uaminifu kwani unayo hatari ya kuleta mgawanyiko wa kijamii.

Siku zote huwa chanzo kikubwa sana cha malalamiko haswa kutoka watu wa tabaka la chini.

Mei Mosi Samia atakuwa Canada​

  • GDP inasemaje kwa mwaka?
  • Figure halisi za makusanyo + hongo tunazochukua zikoje?
  • Sekta ya umma inaongezaje tija kwa taifa?

Mathalani, Wizara ya Nishati, Ewura, Rea, Tanesco. Hawa wote wanashughulikia umeme nchini, uwepo wao una tija yoyote kwa mwananchi wa kawaida?

Private sectors wanaangalia turnover ya mwaka, wanaangalia input ya wafanyakazi, wanawapa increment kwa kuangalia infation iliyotangazwa na hao wanaotaka kupandishwa mishahara based on 3yrs term AU kwa promotion ambayo nayo haitikani na mseleleko ila uhitaji halisi au perfomance based.

Nchi maskini, watumishi wa serikali matajiri, mishahara midogo; vere machi konfyuzing
Mwalimu huyo, hayo unayomueleza anayajulia wapi?
 
Kuna watu stress zitawauwa. Pambaneni kulipa kodi ili walimu ambao ni ni vibarua wa nchi tupate kula.
 
Wivu wa kike huo
Mngekuwa mnafanya kazi hata kwa asilimia 25% ya kazi mnayotakiwa kufanya tanzania ingekuwa tajiri ila ukweli ni kwamba mnafanya kazi kwa asilimia 4% na asilimia 60% mnafanya kazi za ubadhilifu na uhalifu mwingine sehemu za kazi, asilimia 36% iliyobaki mnafanya kazi ya kutongozana basi[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Wanyonge washamba sana. Wewe philipo na wenzako mnasumbuliwa na ujinga.
1. Juni 2021 mama alipandisha vyeo watumish karibia 80 elfu

2. Mei 2022 watumish laki 1 kasoro watapanda vyeo.

Mama ana roho nzuri sana.

Ngoja niende nmb kuchukua m7 nimalizie hekalu langu.

Wachawi ***** zenu
Vyeo mmepandisha ila panya road wamerudi vyeo mmepandishwa ila rushwa imerudi vyeo mmepandishwa ila ufisadi umerudi vyeo mmepandishwa ila uzembe na dharau vimerudi vyeo mmepandishwa ila kutokuwajibika kazini kumerudi na kuongezeka , wafanyakazi wa serikali kazi pekee mnayo weza ni kujaza vyoo na ufisadi tu
 
Binadamu alivyoimbwa ni tofauti na wanyama wengi anaowatawala maishani mwake kila siku. Anao uwezo wa kuificha ile hulka yake ya ndani kabisa akacheka kwa bashasha na uchangamfu na usiweze hata kidogo kuitambia nia yake ya ndani. Huwa natizama vile vipindi vya matukio ya maisha ya wamarekani wanaitwa ID (Investigation Discovery) na sura zote za wale wauwaji makatili mara nyingi ni zile zilizozoeleka kuonekana makanisani tena zikiwa zimekaa viti vya mbele kabisa.

Zimeimbwa nyimbo nyingi ni wanamuziki mbalimbali kuelezea hizi sura mbili za mwanadamu na namna anavyoweza kuuma na kupuliza akiwa ni sehemu muhimu ya jamii inayomzunguka. Binadamu ni kiumbe mwenye uwezo wa kuificha nia yake na anayemzunguka wala asiweze kufahamu anawaza nini na kwa muda gani. Simba, Fisi, Kima, Chui na hata hawa paka na panya walio karibu zaidi na binadamu huwa hawana uwezo wa kuficha kusudio lao wanapokuwa mbele ya macho yetu. Wapo wazi na ukiwaona tu unajua wanachotaka kukifanya ni kipi.

Nimejikuta nikiwa katika tafakari hii baada ya kukumbuka ahadi aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana siku ya Mei Mosi pale Kirumba Stadium Mwanza. Aliahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi akitumia maneno ya kingereza 'package'. Wafanyakazi wa serikali kwa sasa wanaisubiri kwa hamu hiyo package yao mpya ambayo kwa kawaida huambatana na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa za kila siku.

Ni hawa hawa wanaoisubiri hiyo package mpya waliojawa na ufundi wa kuchora michoro ya wizi wa mapesa. Kibaya zaidi huwa wanaiba mabilioni ya shilingi za waajiri wao. Ni hawa hawa wanaotengeneza stika feki pale Uhamiaji ndio wanaopita na mabango ya kudai nyongeza za mishahara wakati wa yale maandamano maarufu ya Mei Mosi ya viwanjani. Ni hawa hawa ambao CAG anawapa hati ya chafu baada ya kugundua wizi uliokubuhu ndio wenye ushujaa wa kubeba mabango ya kudai malipo mazuri zaidi.

Ni hawa hawa wafanyakazi wenye uaminifu karibu na zero, ndio wanaoanzisha nyuzi za kuponda awamu za serikali iwapo wanaoona mishahara yao haipandishwi. Wanataka wapewe kikubwa na mwajiri wakati huo hawana sifa ya maana sana ya kuwa nayo, ile ya uaminifu kwa mali ya umma. Ni hawa hawa wabeba mabango wanaonuna wanaposikia mwaka huu kutakuwa hakuna nyongeza ya mshahara wenye maarifa ya kutengeneza michoro ya mishahara hewa inayokwenda mpaka kufikia pensheni hewa wakati huyo mwajiriwa hewa anapokuwa amestaafu.

CAG anawaumbua sana wafanyakazi wa sekta mbalimbali kila mwaka na hawachoki kudai nyongeza ambalo kwa kweli ni jasho lao. Pesa zinazoingia mifukoni mwa watu kwa maana ya wizi ni nyingi kulinganisha na zile zinazotumika katika kuongeza mishahara ya wafanyakazi nchi nzima.

Uaminifu ni mtihani mkubwa kwa watanzania. Mahubiri yale maarufu ya wachungaji, mashekhe na mapadre yanajikita katika kuupiga vita ubinafsi mimi naamini kingine cha kupigwa vita ni ukosefu wa uaminifu kwani unayo hatari ya kuleta mgawanyiko wa kijamii.

Siku zote huwa chanzo kikubwa sana cha malalamiko haswa kutoka watu wa tabaka la chini.
Watanzania tuna wivu wa kijinga Sana. Hakuna mtu atapata nafasi yajuu awatengenezee maslahi wengine ajinyime yeye. Hata ubane vipi serikalini watu bado watatoboa. Ila nchi yetu naipongeza Sana tuna watu smart Sana hata wakijineemesha wanahakikisha mipango ya maendeleo yanatekelezwa. Ndugu Mwandishi Nina uhakika hata wewe ungekuwa waziri lazima ungepiga. Unampaje mchina Mradi wa bilioni 40 na wewe usiambulie hata 10,000 kweli ?
 
Kuna watu stress zitawauwa. Pambaneni kulipa kodi ili walimu ambao ni ni vibarua wa nchi tupate kula.
Mwalimu? Mwalimu ?

Uwe unaona aibu, wenzio wengi hata kuzungumza tu wanaona aibu.

Hapa ilipaswa waliopo kwenye utumishi wa umma kweli ndio wazungumze.

Chukua hii, Kuna taasisi ya serikali mtu anayeanza kazi leo analipwa mil 2.8 basic salary. Hapo allowances zingine bado
 
Vyeo mmepandisha ila panya road wamerudi vyeo mmepandishwa ila rushwa imerudi vyeo mmepandishwa ila ufisadi umerudi vyeo mmepandishwa ila uzembe na dharau vimerudi vyeo mmepandishwa ila kutokuwajibika kazini kumerudi na kuongezeka , wafanyakazi wa serikali kazi pekee mnayo weza ni kujaza vyoo na ufisadi tu
Mwalimu huyo, achana nae
 
Watanzania tuna wivu wa kijinga Sana. Hakuna mtu atapata nafasi yajuu awatengenezee maslahi wengine ajinyime yeye. Hata ubane vipi serikalini watu bado watatoboa. Ila nchi yetu naipongeza Sana tuna watu smart Sana hata wakijineemesha wanahakikisha mipango ya maendeleo yanatekelezwa. Ndugu Mwandishi Nina uhakika hata wewe ungekuwa waziri lazima ungepiga. Unampaje mchina Mradi wa bilioni 40 na wewe usiambulie hata 10,000 kweli ?
Na hayo ndio yamefanya hadi leo hii pesa za kujenga vyoo tunasubiri msaada.

Tunapoona wenzetu wameendelea na umaskini umeisha basi jua waliweza kudhibiti hayo.

Nchi haiwezk kuendelea kwa watu wake kuiibia
 
Wanyonge washamba sana. Wewe philipo na wenzako mnasumbuliwa na ujinga.
1. Juni 2021 mama alipandisha vyeo watumish karibia 80 elfu

2. Mei 2022 watumish laki 1 kasoro watapanda vyeo.

Mama ana roho nzuri sana.

Ngoja niende nmb kuchukua m7 nimalizie hekalu langu.

Wachawi ***** zenu
HEKALU??!! MATAJIRI WA JF,
 
Na hayo ndio yamefanya hadi leo hii pesa za kujenga vyoo tunasubiri msaada.

Tunapoona wenzetu wameendelea na umaskini umeisha basi jua waliweza kudhibiti hayo.

Nchi haiwezk kuendelea kwa watu wake kuiibia
Yaliyofanya wenzetu waendelee ni kuruhusu nchi iongozwe na matajiri. Ukiangalia mataifa Makubwa Kuna makampuni mpaka ya umeme, Maji, mawasiliano yanajitegemea. Serikali inawabeba matajiri Ili wawekeze watengeneze ajira. Mfumo wetu wa serikali ni mbovu unampa mtu nyumba na V8 kwa sababu ya cheo. Inabidi umpendelee mtu kwa sababu ameajiri watu wa kutosha na ana mtandao wa masoko Mkubwa. Mtu kama Rostam ni mtu smart Sana. Ni kumtengenezea mazingira mazuri na madeal atakayofanya yataneemesha nchi yetu kwa Kodi. Wengi wetu tunalipa Kodi tunaponunua bidhaa za matajiri kama Soda, Juice,Bia n.k.
 
Watanzania tuna wivu wa kijinga Sana. Hakuna mtu atapata nafasi yajuu awatengenezee maslahi wengine ajinyime yeye. Hata ubane vipi serikalini watu bado watatoboa. Ila nchi yetu naipongeza Sana tuna watu smart Sana hata wakijineemesha wanahakikisha mipango ya maendeleo yanatekelezwa. Ndugu Mwandishi Nina uhakika hata wewe ungekuwa waziri lazima ungepiga. Unampaje mchina Mradi wa bilioni 40 na wewe usiambulie hata 10,000 kweli ?
Tunaongelea ufisadi na vita ambayo kila unayemuamini kama ni mpambanaji wa kikosi cha mbele kabisa kumbe haaminiki.
 
Yaliyofanya wenzetu waendelee ni kuruhusu nchi iongozwe na matajiri. Ukiangalia mataifa Makubwa Kuna makampuni mpaka ya umeme, Maji, mawasiliano yanajitegemea. Serikali inawabeba matajiri Ili wawekeze watengeneze ajira. Mfumo wetu wa serikali ni mbovu unampa mtu nyumba na V8 kwa sababu ya cheo. Inabidi umpendelee mtu kwa sababu ameajiri watu wa kutosha na ana mtandao wa masoko Mkubwa. Mtu kama Rostam ni mtu smart Sana. Ni kumtengenezea mazingira mazuri na madeal atakayofanya yataneemesha nchi yetu kwa Kodi. Wengi wetu tunalipa Kodi tunaponunua bidhaa za matajiri kama Soda, Juice,Bia n.k.
Lugha gongana
Mm nilikua najibu ulipokuwa unasema wanakula hizo pesa za wizi kwa 10% ni kawaida na waachwe. Ww umekuja na suala la serikali kuwakumbatia matajiri ambalo mm sikulisema Wala kuzungumzia
 
Back
Top Bottom