Wapigaji na wezi wa mashirika ya Umma wanaposubiri kupandishiwa mishahara yao Mei Mosi

Wapigaji na wezi wa mashirika ya Umma wanaposubiri kupandishiwa mishahara yao Mei Mosi

Na hayo ndio yamefanya hadi leo hii pesa za kujenga vyoo tunasubiri msaada.

Tunapoona wenzetu wameendelea na umaskini umeisha basi jua waliweza kudhibiti hayo.

Nchi haiwezk kuendelea kwa watu wake kuiibia
Wewe umenielewa vyema kabisa.
 
Watumishi wanaotakiwa kupandishwa mishahara ndio hao wapo bize wanalalamika hawajapewa sare za sikukuu...
 
Binadamu alivyoimbwa ni tofauti na wanyama wengi anaowatawala maishani mwake kila siku. Anao uwezo wa kuificha ile hulka yake ya ndani kabisa akacheka kwa bashasha na uchangamfu na usiweze hata kidogo kuitambia nia yake ya ndani. Huwa natizama vile vipindi vya matukio ya maisha ya wamarekani wanaitwa ID (Investigation Discovery) na sura zote za wale wauwaji makatili mara nyingi ni zile zilizozoeleka kuonekana makanisani tena zikiwa zimekaa viti vya mbele kabisa.

Zimeimbwa nyimbo nyingi ni wanamuziki mbalimbali kuelezea hizi sura mbili za mwanadamu na namna anavyoweza kuuma na kupuliza akiwa ni sehemu muhimu ya jamii inayomzunguka. Binadamu ni kiumbe mwenye uwezo wa kuificha nia yake na anayemzunguka wala asiweze kufahamu anawaza nini na kwa muda gani. Simba, Fisi, Kima, Chui na hata hawa paka na panya walio karibu zaidi na binadamu huwa hawana uwezo wa kuficha kusudio lao wanapokuwa mbele ya macho yetu. Wapo wazi na ukiwaona tu unajua wanachotaka kukifanya ni kipi.

Nimejikuta nikiwa katika tafakari hii baada ya kukumbuka ahadi aliyoitoa Rais Samia Suluhu Hassan mwaka jana siku ya Mei Mosi pale Kirumba Stadium Mwanza. Aliahidi kupandisha mishahara ya wafanyakazi akitumia maneno ya kingereza 'package'. Wafanyakazi wa serikali kwa sasa wanaisubiri kwa hamu hiyo package yao mpya ambayo kwa kawaida huambatana na kupanda kwa bei ya baadhi ya bidhaa za kila siku.

Ni hawa hawa wanaoisubiri hiyo package mpya waliojawa na ufundi wa kuchora michoro ya wizi wa mapesa. Kibaya zaidi huwa wanaiba mabilioni ya shilingi za waajiri wao. Ni hawa hawa wanaotengeneza stika feki pale Uhamiaji ndio wanaopita na mabango ya kudai nyongeza za mishahara wakati wa yale maandamano maarufu ya Mei Mosi ya viwanjani. Ni hawa hawa ambao CAG anawapa hati ya chafu baada ya kugundua wizi uliokubuhu ndio wenye ushujaa wa kubeba mabango ya kudai malipo mazuri zaidi.

Ni hawa hawa wafanyakazi wenye uaminifu karibu na zero, ndio wanaoanzisha nyuzi za kuponda awamu za serikali iwapo wanaoona mishahara yao haipandishwi. Wanataka wapewe kikubwa na mwajiri wakati huo hawana sifa ya maana sana ya kuwa nayo, ile ya uaminifu kwa mali ya umma. Ni hawa hawa wabeba mabango wanaonuna wanaposikia mwaka huu kutakuwa hakuna nyongeza ya mshahara wenye maarifa ya kutengeneza michoro ya mishahara hewa inayokwenda mpaka kufikia pensheni hewa wakati huyo mwajiriwa hewa anapokuwa amestaafu.

CAG anawaumbua sana wafanyakazi wa sekta mbalimbali kila mwaka na hawachoki kudai nyongeza ambalo kwa kweli ni jasho lao. Pesa zinazoingia mifukoni mwa watu kwa maana ya wizi ni nyingi kulinganisha na zile zinazotumika katika kuongeza mishahara ya wafanyakazi nchi nzima.

Uaminifu ni mtihani mkubwa kwa watanzania. Mahubiri yale maarufu ya wachungaji, mashekhe na mapadre yanajikita katika kuupiga vita ubinafsi mimi naamini kingine cha kupigwa vita ni ukosefu wa uaminifu kwani unayo hatari ya kuleta mgawanyiko wa kijamii.

Siku zote huwa chanzo kikubwa sana cha malalamiko haswa kutoka watu wa tabaka la chini.
Pole ssana.
 
Mwalimu huyo, achana nae
Wewe jamaa naona umeumia sana mimi kuwa mwalimu, kwa mujibu wako sina hadhi hata ya kulisha mifugo wako. Mimi nakuhakikishia kuwa nina furaha na amani sana.
Ninachosubiri ni mama kunena neno na hata akichana mkeka ipo siku atatenda jema.

Wewe kwa mchango wako wa kwenye jamii na uchumi ni upi? Kama ni tajiri nakuombea utajirike zaidi ili kodi yako inipatie chakula na uji wa watoto wangu.
 
Wewe jamaa naona umeumia sana mimi kuwa mwalimu, kwa mujibu wako sina hadhi hata ya kulisha mifugo wako. Mimi nakuhakikishia kuwa nina furaha na amani sana.
Ninachosubiri ni mama kunena neno na hata akichana mkeka ipo siku atatenda jema.

Wewe kwa mchango wako wa kwenye jamii na uchumi ni upi? Kama ni tajiri nakuombea utajirike zaidi ili kodi yako inipatie chakula na uji wa watoto wangu.
Walimu mpandishwe tu kwa kweli mnaishi maisha magumu sn
 
Tunaongelea ufisadi na vita ambayo kila unayemuamini kama ni mpambanaji wa kikosi cha mbele kabisa kumbe haaminiki.
Ufisadi upo na utaendelea kuwepo kama haitobadilika. Nimeshasema Ili tuendelee lazima tuwakumbatie wawekezaji na si vinginevyo. Unamnunulia mkuu wa mkoa V8 ya Nini ? anafanya kitu gani productive ? Ametengeneza ajira ngapi ? Ni sawa na watoto wa matajiri mtoto anapata DIV IV unapeleka China akirudi anakuja kuwa mlevi unalaumu. Kwa Sasa hivi mafisadi waibe tu lakini wafungue ajira mpya iba bilioni lakini fungua kiwanda au hoteli watu wapate ajira. Sio unaiba bilioni unamjengea hawara ghorofa, unanunua benzi tatu au unaongeza mke. Jamani swala la ufisadi halikwepeki, na Tanzania kama nchi hatuna ufisadi wa kutisha kama Kenya, Congo na Nigeria. Nigeria wana mafuta lakini wana uhaba wa mafuta. Mpaka leo Nigeria hawana umeme wa uhakika lakini wana mabilionea. Kwa sababu Mafisadi wao hawawekezi kwenye biashara kubwa. Ukitembelea Instagram utaona waNigeria wanamiliki ma Ferrari au Lamborghini. Wanasiasa kama hao hawafai kabisa. Iba uanzishe business sio uibe halafu unayumbisha uchumi wa nchi.
 
Kama mama hata timiza ahadi yake.. b
Basi kuna haja ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi kuchukua hatua kali.
 
Back
Top Bottom