Wapiganaji wa Kiuyghur waliopo Syria waapa kuja kuishambulia China katika hatua inayo fuata

Kilichotokea kwa urusi pale syria kinaenda kutokea kwa mchina
Haya mambo hupangwa na yako calculated fuatilia kauli ya trump kuhusu brics na vita ya ukraine
Kinaenda kumtokea China wapi ?

Nakukumbusha Syria halikuwa eneo la Urusi wala Assad hakuwa Rais wa Urusi.
 
“Now here in Syria, in all the cities here, we fight for Allah, and we will continue to do this in our Urumchi, Aqsu and Kashgar in the future,”

How!!!hawa watu wanafeli sana wakati mwengine.
 
They can fight but they cannot win.
 
Marekani na vikundi vyake vya kigaidi wanatapatapa sana.

Marekani ilishajaribu sana kufanya color revolution kupitia NED mjini Xinjiang walifeli

Wakaja na propaganda kuwa kuna uvunjifu wa haki za binadamu wakafeli tena

Wakapiga ban importation ya cotton kutoka Xinjiang nchini Marekani na Ulaya wakidai walimaji wa hiyo cotton ni slave labor wamefeli

Marekani ni sawa na mfa maji haachi kutapatapa.

Kwa uchumi, life standard na prosperity waliyo nayo watu wa Xinjiang utaanzia wapi kuwaambia wawaunge mkono magaidi ya Kimarekani

Naona sasa wanataka kutumia hao mgambo waonekane kama freedom fighters hivyo ndivyo Western media na NGOs zitakuwa zinawaita.

Hakuna watafanya hapo Xinjiang
 
Mü Israel yupo mbele ya muda. Baada ya kuzembea Oct 7 sasa hivi sera mpya ni kushambulia kabla ya kushambuliwa
 
Hiko kikundi ni cha magaidi lakini angalia jinsi media za Magharibi zilivyo za kinafiki, The Telegraph jarida la Uingereza wameandika

Uyghur fighters in Syria vow to come for China next.
The Turkistan Islamic Party says its main mission to ‘liberate the Muslims of East Turkistan from the Chinese occupation
–The Telegraph

Badala ya kuwaita terrorist wanawaita fighters

Badala ya kusema wanataka kufanya invasion wanasema wanaenda kufanya liberation

Marekani na Turkey zinatumia billions of dollars kuwatrain hao magaidi. Wanawatrain ili wawatumie kwa maslahi yao.

Jiulize kweli Marekani na nchi za Magharibi wana uchungu sana na Waislam wa China wanaoishi kwa amani, good life kuliko mamilioni ya Waislam waliowaua na kuwafanya walemavu na mafukara Palestina, Iraq, Afghastan, Syria, Libya na maeneo mengine ya M.E?

Kuna vitu vinatafutwa dhidi ya China to destabalize China, kuichokoza China ianze vita na magaidi yanayopambwa kwa jina la freedom fighters ili kuichafulia jina kwenye medani za kimataifa, kuzuia ushawishi wa China na kuzuia kupanuka kwa BRI

By the way hayo magaidi hayana ubavu kwenda kufanya wendawazimu wao Xinjiang

 
hahah wanataka kuutekenya mbuyu. Shauri yao wakifa mimi simo.
 
Inategemea uko upande gani, PKK, na PYD au Syrian na Turkish KURDISH groups, Uturuki wanawaita Magaidi, lakini wao wanajiita ni Freedom fighters.

Umeona hata mgogoro wa Uturuki na Finland, ni kwamba Uturuki inasema Sweden, na Finaland inawatunza Magaidi, lakini Finland na Sweden wanasema wale siyo magaidi, Lakini Uturuki ilikataa hata Finland kujiunga NATO kwa sababu ilitaka, Finland iwalete magaidi uturuki waadhibiwe kijeshi, Finlanda ilikataa na inakataa mpaka kesho.

Lakini hao PKK na YPD waliunda coalition na USA kuwapiga DAESH/ISIS na wamefanikiwa na mpaka sasa wanapata msaada kutoka USA. lakini ukichunguza PKK/YPD na ISIS ni wale wale tu.

YPJ au women's Protection Unit, wamo ISIS na wamo YPD na wamo PKK, yani wanakula kote kote hawaitwi magaidi. Kwasababu licha ya kupigana civilian wars in syria hawavuki mipaka kwenda nje. ila ISIS walitoka nje wakakiona cha moto.
Nilichojifunza mimi pigana ndani usitoke nje wewe ni freedom fighter, hawa Uyughur walienda Syria kupata uzoefu, labda wakirudi China wataleta impact. Maana wao wanapigana kukomboa Uyughur hawampigi mwingine yeyote, hivyo wao siyo terrorist group/organisation.

Hii migogoro inategemea Umesimama wapi na unaangalia wapi na unaangalia nini? Unaye muona Gaidi mwenzio anamuona ni mpigania haki.

HAMAS hawana tofauti na PLO, lakini walijichanganya kuanza kuvuka mipaka na kuendesha vita vya kihuni dhidi ya Israel.

Angalia PLO ya Mahamud Abbas ndiyo hiyo hiyo ilikuwa chini ya Arafat aliyekuwa anaitwa Gaidi wakati huo, alipofariki UN walimpokea Mahamud Abbas kwa mikono miwili na kumuhaidi kumsaidia kupata taifa la Palestina, sijui HAMAS walitoka wapi wakavuruga kila kitu, Nia yao moja lakini mtindo tofauti.

Abbas anataka democratic ways, HAMAS wanataka nguvu.
 
hawa Uyughur walienda Syria kupata uzoefu, labda wakirudi China wataleta impact. Maana wao wanapigana kukomboa Uyughur hawampigi mwingine yeyote, hivyo wao siyo terrorist group/organisation.
Kuikomboa Xinjiang kutoka kwa nani? Unaelewa maana ya neno kukomboa? Huoni wanaipinga serikali ya China?
 
Hii migogoro inategemea Umesimama wapi na unaangalia wapi na unaangalia nini? Unaye muona Gaidi mwenzio anamuona ni mpigania haki.
Xinjiang ni eneo la taifa gani?

Hivi haujui kuwa hiko kikundi kinafadhiliwa na shirika la NED la Marekani.

Tangu lini Marekani akawa na uchungu na Waislam wa Xinjiang, China? Kashawaua na anaendelea kuwaua Waislam wangapi hapo M.E?

Hao ni magaidi this is the game of geopolitics. Kwa kuwa uelewa wako ni mdogo kwenye masula ya geopolitics ndio maana umekuwa brainwashed na Western propaganda
 
Hawa wapiganaji wamevaa sana mabomu ya kujitoa muhanga China na kuua watu.

Wamechoma visu na kushambulia watu kwa gari la mwendo kasi huko Xinjiang.

"Kwa miaka kadhaa nchi ya China ilikumbana na matukio ya kigaidi hasa katika maeneo ya Xinjiang na Beijing hali iliyo pelekea serikali ya Beijing kuchukua hatua kali za kiusalama katika eneo lote la Xinjiang".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…