Habari Wadau.
Nmesoma hoja nyingi sana za wanaopinga serikali tatu na "to be honest they are very weak" kutokana na sababu zifuatazo:
1.Hoja ya gharama
Ukimsikiliza mwenyekiti wa tume amebainisha dhahiri jinsi mgawanyiko wa wizara utakavyokuwa na jinsi gharama zitakavyopungua kutokana na hayo mabadiliko na pia juu ya kupunguza idadi ya wabunge. Mbona serikali ya Zanzibar imeexist miaka yote hii na hatujaongea suala la gharama. Kwa nini leo tunataka kuwanyima fursa ya Watanganyika kujitawala kwa kisingizio cha gharama?? Suala la serikali tatu ni muhimu kwa ustawi wa nchi yetu pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali zetu. Kilio cha wazanzibar kitakua kimesikika kwa kuanzisha huu mfumo sababu itazipa pande zote mbili uwezo wa kujitawala na pia kukuutafakari zaidi muungano kwa pamoja kama pande mbili husika.
2.Kupuuza madai ya zanzibar
Kila siku tunasikia malalamiko kutoka upande wa pili wakitaka kupata mamlaka kamili kwa nchi yao hata leo tukipitisha referendum lazima washinde katika hilo. Kukataa serikali tatu ni kuzidi kuchochea vurugu za kisiasa hapa nchini.
3. Kutokutoa mbadala wa serikali tatu
Hata viongozi wakubwa niliowasikia hawatoi mbadala wa serikali tatu zaidi ya kutaka kuwakaririsha wananchi juu ya gharama gharama gharama. Please toeni alternative sio kubwabwaja tu.
Kwa jinsi ninavyoona suala la serikali moja haliwezekani wala tusipoteze mda na hilo. Pia mfumu huu wa muungano uliopo ushaprove failure. Mambo yanayowezekana ni serikali tatu au kuvunja muungano na kubaki na serikali mbili huku tukiishi kwa ujirani mwema.
I STAND TO BE CORRECTED.