SOMA HII UCHEKE*
Jana Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Stop Over wa Chadema bi. Magreth Mugyabhuso alihojiwa na vyombo vya habari alisema haya;
Anamshukuru Mh.Mbowe kwa Maamuzi magumu aliyoyachukua ya wagombea wote wa Chadema kuachana na zoezi hilo la uchaguzi wa serikali za mitaa maana kwa asilimia kubwa limeambatana na mambo ya kihuni.....
Bi Magreth alisema .. "Binafsi nilichukua fomu kwa wakati na kurudisha kwa wakati,bahati nzuri nilitoa copy kabla ya kurudisha ile orginal, kitu nilichokikuta baada ya kupewa majina ya walio enguliwa nikauliza sababu , nikapewa fomu nione sababu za kuenguliwa kwagu ,nilistuka kuona fomu yangu imebadilishwa si ile niliokuwa nayo copy...ya kwao inajieleza mimi nilijaza jinsia yangu ni kiume hali mimi najitambua,upande wa unagombea nafasi gani, ? nimekuta imeandikwa naogombea mwenyekiti serikali ya mtaa na mjumbe pia, kitu ambacho ni Uhuni kabisa,ofisi nyeti kama hii ya serikali haipaswi kucheza na documents za watu kihuni namna hii".
Huyu Bi.Magreth ni Mwenyekiti eneo hilo tangu mwaka 2015 mpaka leo, asijue kujaza fomu wala yy ni jinsia gani? Asijue yy anagombea nafasi gani?
CCM mkiamua kukesha na ngoma za watoto mjisitiri nguo....
Lakini pamoja na figisu hizi za aibu, Bi. Magreth aliandika barua za pingamizi na alipofikisha ofisini hapo zilitupiliwa mbali.....
Juzi baada ya Chadema kujitoa , jina likabandikwa ukutani "eti
#Mpya. Magreth *AMETEULIWA*
Nilicheka sana, nikajisemea CCM Mwl. wao ni amekufa.....!
Nimeona afadhali kuendelee kufanya mambo mengine kuliko haya ya siasa za kihuni"
Kuna usemi unasema, *"ukisikia Mfalme anatembea na kijakazi , siku ya aibu inakaribia."*