Wapinzani msimwamini Dkt. Slaa

Wapinzani msimwamini Dkt. Slaa

Slaa ni Mzalendo, vijana waache kumnanga sana. Kwanza kakipigania chama sana kuliko watu wengi ambao walikuja wakaondoka.
Mzee kasaidia sana Watanzania kujua nini kinaendelea kwenye maridhiano,

Walikaa muda mrefu vikao Kwa vikao bila mrejesho Kwa umma Hadi Mzee huyo alipohoji akisaidiana na Lissu na Lema.
 
Hi!

Mara nyingi tunasema kuwa Watanzania ni wasahaulifu sana na ni watu wanaopenda kwenda sambamba na upepo. Kwa lugha nyepesi tunasema mtengenezee skendo au tukio Mtanzania ili umtoe kwenye reli.

Huyu Dkt. Slaa alichotufanyia Watanganyika 2015 mmekisahau?

Mmesahau nasaha zake za miaka miwili iliyopita?

Dkt. Slaa either propagandist mkuu hapa nchini aliyeajiriwa na serikali miaka mingi iliyopita au ni mtu wa fursa tu asiye na uchungu na taifa hili. Hupanua kinywa chake pale tu anapohitaji fursa.

Nasema hivi hiyo kesi ya Uhaini ndiyo stahiki yake, avune alichopanda.

Jioni njema.
Waambie! Deep under cover na kiapo chake hatakisaliti. Baada ya gia nyingine kubuma .... upenyo unatafutwa kwa njia hii sasa?
 
Mzee kasaidia sana Watanzania kujua nini kinaendelea kwenye maridhiano,

Walikaa muda mrefu vikao Kwa vikao bila mrejesho Kwa umma Hadi Mzee huyo alipohoji akisaidiana na Lissu na Lema.
Mzee ni asset sana kwa upinzani. Inawezekana akawa na makando yake lakini nadhani mazuri yake na uwezo wake unafunika hayo mengine.
 
Mpaka sasa hawajaona shida. Mfano, kama mliweza kusema lowassa fisadi miaka 10, halafu mkageuka, kwanini leo hii muaminike mkisema mkataba wa DP world ni wa kuuza nchi? Mind you mimi siungi mkataba mkono ila najaribu kumake sense ya hawa vijana wanaomsema Slaa kuwa haaminiki na wengine wanaaminika wanasimamia msingi gani?
Mimi personally, naona Slaa aliendelea kusimamia alichohubiri.
Ccm yenyewe waliomkata kwenye ugombea u Rais kwa sababu hizo hizo. Walimpokea kwa sherehe zilizoongozwa na mwenyekiti/Rais wa nchi, lumumba baada kumshawishi aihame Cdm. Hapo utasema Je ?!

Kwanini uione kosa la Cdm na si ya ccm inayoongoza nchi. Why double standard ?!
 
Mimi naongelea chadema kama chamba mbadala ya ccm. Hivyo kinapaswa kuwa kimenyooka sio kufanya yale ya ccm na ukigeugeu.
 
Back
Top Bottom