Wapinzani ndio walio shauri tununue ndege tena wakaanza kuzipinga

Wapinzani ndio walio shauri tununue ndege tena wakaanza kuzipinga

EllySkyWilly

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
2,204
Reaction score
2,085
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania

Wao ndio walio ishauri serikali inunue ndege na kufufu ATCL leo tena hao hao ndio wapingaji wa ndege na ATCL.

Naomba niweke hii video kama ilivyo, niwaombeni dada zangu na kaka zangu wa upinzani hebu tizameni hii video. Hiki ndicho mlicho kizungumza katika bunge letu la awamu ya nne mkaja tena mkakizungumza katika bunge la awamu ya tano.

Walishauri mnunue bila kuwa na business plan?

Walishauri mnunue ndege kwa cash?

Walishauri mnunue na kisha muendeshe shirika kwa mtindo huu mnaotumia?

Wapinzani ndio walishauri mnunue ndege bila kupata ushauri wa wabunge(Bunge) na wadau wengine?

Wapinzani ndio walishauri mnunue ndege kama mnavyonumua nyanya sokoni?
 
Wapenzi noma, wametupandishia bei za vifurushi.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Nijibu hoja zipi mkuu, tizama hiyo video utaelewa nini nimekilenga sihitaji maswali mengi.

Hoja zipi?
. Biashara yoyote lazima uwe na
1. Mipango thabiti
2. Mikakati
3. Risk analysis
4. Mitigation
Nk

Tueleze ccm wanafanya nini katika hayo?
 
Kwa hiyo walivyoshauri nanyie mkafuata ushauri?kwa nini msijishauri nyie kwanza?

Maana yake mawazo hamna,sasa bunge hili mpo nyie wenyewe ndio maana bunge limekosa mvuto,vichwa vyenye akili kubwa havimo tena....
 
umeungaunga sana

Hakuna hata mmoja haapo aliyesema mnuunue nyingi bila kuangalia ushindani wa soko wala hakuna aliyeshauri zinunuliwe kwa misifaa, NOTHING!
hahahahaaa, mbona wamesema hapo mkuu, acha kukwepa ukweli. Ninacho jifunza ni kimoja tu tuna wabunge mafundi wakuongea maneno mdomoni tu.
 
Tulikuwa tunasafiri na fast jet Dsm - Mbeya kwenda na kurudi tsh180, 000 ndege zilijaa 120 passengers

Sasa hivi Dsm - mbeya tsh 445,000 hovyo kabisa.... pangaboy

Kuifungia Fast jet nafuu kwa nani?

1. Wasafiri wameacha nakurudi kwenye mabasi 13hrs on the road

2. Serikali imekosa kodi iliyokuwa inapata kutoka fast jet

3. Sasa hivi wanapeleka pangaboy ya 45 seats!!! Very expensive

Ujuwaji wa hasara tupu kwa raia na serikali yenyewe
 
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania...
Ulikuwa ushauri.

Kwani walikushikieni BASTOLA kwamba ni lazima mnunue ndege?

Tena mnunue ndege kwa fedha taslimu 2 trillion shillings?

NB:

..mwingine aliyeshauri ni Rais Kagame wa Rwanda ambaye mwaka jana ameamua kuuza ndege zake kwa Qatar Airways.
 
Tulikuwa tunasafiri na fast jet Dsm - Mbeya kwenda na kurudi tsh180, 000 ndege zilijaa 120 passengers

Sasa hivi Dsm - mbeya tsh 445,000 hovyo kabisa.... pangaboy

Kuifungia Fast jet nafuu kwa nani?

1. Wasafiri wameacha nakurudi kwenye mabasi 13hrs on the road

2. Serikali imekosa kodi iliyokuwa inapata kutoka fast jet

3. Sasa hivi wanapeleka pangaboy ya 45 seats!!! Very expensive

Ujuwaji wa hasara tupu kwa raia na serikali yenyewe
Rudi kwenye muktadha wa mada, acha kuropoka
 
Hujui lolote, sana sana mzushi tu.
Wewe ndio hujui lolote, mkuu. Ungekua unajua lolote ungejieleza kwa weledi lakini kwasababu hujui lolote zaidi yangu basi ndio sababu unajieleza kwa jazba.
 
Back
Top Bottom