Wapinzani ndio walio shauri tununue ndege tena wakaanza kuzipinga

Wapinzani ndio walio shauri tununue ndege tena wakaanza kuzipinga

Zikapigwa chapa HAPA KAZI TU kumtukuza mnunuzi! Wamefeli wanakuja kulalamikia wapinzani! Kama mazuzu vile!
Msukuma mmoja mkulima kule Chato angependa kufuga ng'ombe wa maziwa baada ya kushahriana na mke wake wakakubaliana waanze na 10 na maziwa watauza kwenye ile Hoteli mpya na Uwanja wa Ndege ya ziada yatatumika nyumbani. Ng'ombe watahitaji zizi imara ili wasiibiwe kwa hiyo wanatafutwa vijana wa Kijijini mafundi wa kazi hiyo kwa malipo nafuu na baada ya kazi kukamilika atahitajika mtu wa kuchunga maana watoto wote wanaenda bure elimu lakini atapata Mrundi mmoja atalipwa na fedha za mauzo ya maziwa. Baada ya kumpatia mchungaji mzuri mwenye uzoefu, wanaenda pamoja mpaka kwenye eneo la kuchungia wakionyeshana njia za kupitia na kutopita ili wanyama wasiharibu mali za watu wengine. Sasa wanaanza kuleta ng'ombe mmojammoja, wawiliwawili jinsi matayarisho mengine yanavyokamilika. Yule Msukuma mwingine mwenye PhD angefuata utaratibu wa Mkulima, hakuna mtu angehoji kila kitu kingeenda sawa.
 
Tz haina wapinzani makini ina wapumbavu fulani ambao leo wakisema hili kesho wanabadilika tena, wapinzani wenyewe akina mbowe aka faru John aka sultan unategemea nini?
 
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania

Wao ndio walio ishauri serikali inunue ndege na kufufu ATCL leo tena hao hao ndio wapingaji wa ndege na ATCL.

Naomba niweke hii video kama ilivyo, niwaombeni dada zangu na kaka zangu wa upinzani hebu tizameni hii video. Hiki ndicho mlicho kizungumza katika bunge letu la awamu ya nne mkaja tena mkakizungumza katika bunge la awamu ya tano.

View attachment 1741271
Wao walishauri ila naona bwana yule alipopewa hii idea akaona ndio sehemu ya kupigia hela. Unajua hata tunaposema mtoto akizingua usimnyime makofi au fimbo hatujamaanisha sasa upige kama unaua chatu. Huyu mwenzetu akaamua kwenda extreme. Ndege nne zingetosha au tano kwa kuanzia halafu shirika lijiendeshe sasa yeye akaona ndio afanye yake.
 
acha kunidanganya mimi sio mtoto mdogo
 
Kwanza tupe sababu kuu za mfalme kuzuia bunge kuwa live

Pia tupe sababu ya kutosemwa shirika linatia hasara badala yake tunaimbiwa mapambio ya faida ya billioni 28..

Tupe sababu ya mfalme kufanya siasa mwenyewe kwa miaka 5 huku akizuia wenzie wasishindane kwa hoja jukwaani
 
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania

Wao ndio walio ishauri serikali inunue ndege na kufufu ATCL leo tena hao hao ndio wapingaji wa ndege na ATCL.

Naomba niweke hii video kama ilivyo, niwaombeni dada zangu na kaka zangu wa upinzani hebu tizameni hii video. Hiki ndicho mlicho kizungumza katika bunge letu la awamu ya nne mkaja tena mkakizungumza katika bunge la awamu ya tano.

View attachment 1741271
Hii mbona ilishajibiwa kitambo tu au ulikuwa bado kwenu unawinda ndezi? Kinachopingwa ni jinsi zilivyonunuliwa bila kufuata utaratibu uliowekwa na pia jinsi shiririka linavyoendeshwa kwa hasara, mwenyewe unajiona umetoa kitu cha maana.
 
Upinzani wa Tanzania ni zero ndio maana wananchi waliwapiga chini uchaguzi mkuu hawajui hata wanasimamia nini

Hii clip ni ushahidi vicjwani weupe kabisa
 
Sasa kama unashauliwa ununue Mabasi ya daladala ya kufanya ruti ya Kawe ubungo mawasiliano,inabidi utumie akili,sasa baada ya kununua coaster au hiace,wewe ukaenda kununua Bus la abiria 65,kama shabiby harafu lipige ruti Kawe ubungo,ukipata hasara unamlaumu nani?
 
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania

Wao ndio walio ishauri serikali inunue ndege na kufufu ATCL leo tena hao hao ndio wapingaji wa ndege na ATCL.

Naomba niweke hii video kama ilivyo, niwaombeni dada zangu na kaka zangu wa upinzani hebu tizameni hii video. Hiki ndicho mlicho kizungumza katika bunge letu la awamu ya nne mkaja tena mkakizungumza katika bunge la awamu ya tano.

View attachment 1741271
Miaka 15 iliyopita kumetokea mabadiliko makubwa ya biashara ya anga. Hali iliyopelekea mashirika mengi ya ndege ya kitaifa kufilisika yakiwa na madeni makubwa. Nchi za Zambia, Malawi, Zimbabwe, Uganda nk zote zilifunga mashirika yake kutokana na ushindani wa Mashirika ya nchi za ghuba. Ni Ethiopia, Kenya na South Africa ndiyo wamekuwa wakitamba kwenye bara zima la Africa ingawa nao Kenya na South Africa wamekuwa wakiendesha kwa hasara.

Kama Jiwe angekuwa anashaurika angepaswa kufuata ushauri wa wataaalamu katika ufufuaji wa ATCL ambao ungekuwa guided na Businness plan. Mwandishi Peter Drucker alisema "If you don't know where you are going, any road will get you there". Kufufua ATCL bila business plan ni sawa na kuanza safari bila kujuwa unakwenda wapi. Hivyo njia yeyote itakufaa. Na hapo pa kudaiwa mara na mkulima Hermanus Steyn, Kampuni ya Ujenzi wa Barbara na sasa Kampuni ya Willis ya Lebanon ni kiashiria kuwa hatukuwa na Business plan. Yaani tunakwenda kwa ashiki tu ya mtu mmoja.

Katika Business plan lazima kungekuwa na chapter inayoonyesha kitu kinaitwa SWOT (Strengths, Weaknesses, Opportunities and Threats). Vilevile kungekuwa na chapter ya RISK framework ambayo ingeainisha madeni tunayodaiwa na namna yanavyoweza sababisha ndege zetu kukamatwa.

Mwishowe Businnes plan ingeonyesha madeni yaliyopo na namna ya kuyalipa na pengine ingetengeneza utaratibu wa kuyalipa na kukubaliana na wadai.

Tusilaumiane kuhusu tawala zilizopita kwa kuwa ATCL ni business entity na vilevile iko na kitu kinaitwa "on going concern ". Na mwendo huu wa Jiwe kufanya maamuzi makubwa kwa kutegemea akili yake ndogo tujiandae kupata shida kwenye miradi yote mingine aliyo lazimisha bila kufuata ushauri.
 
Nijibu hoja zipi mkuu, tizama hiyo video utaelewa nini nimekilenga sihitaji maswali mengi.
Ndege zimenunuliwa kabla ya kuandika business plan. Zilikuwapo kwenye sera ya CCM ya uchaguzi wa 2015

2. Walioamua kununua ni Jiwe ma mpwa wake wa Hazina Dotto James wala siyo ATCL

3. Upangaji wa ruti ni wa kisiasa. Angalia jwanalazimisha kwenda Chato, Mpanda Airport, je kuna abiria wa kutosha kule?

4. Wanaogopa ushindani, ndiyo wakaifuta na kuifukuzilia mbali FASTJET. Ushindani huwa kuwasaidia kuboresha huduma

5. Waliitoa ATCL kwenye Kasma ya Wizara ya Uchukuzi na kuipeleka Kasma ya Ikulu. Maana yake CAG alikuwa haruhusiwi kukagua. Chochote utakachokikimbiza kwa CAG huwezi kujua kama kinakupa faida. Ila Samia amelibadili hili

6. Zile Bombardier za awali ni second hand. Kwa miaka 5 ya kwanza tusingehitaji ndege ya masafa mrefu (Dreamliner) mpaka tuimarike kibiashara. Matokeo yake tunalazimika kwenda Mumbai then Guangzhou ili ndege iruke isikostahili lakini siyo kwa ukubwa wa soko

7. Kununua taslimu siyo sifa na kihezo cha kutofilisika bali kuendesha kwa ufanisi na kwa faida ndivyo vigezo vya survival

8. Kwenda nje ya East Africa katika miaka 5 ya kwanza siyo mpango mzuri. ATCL ingepambana na soko la nyumbani kwanza ndipo baadaye ianze kufikiria kwenda kimataifa zaidi
 
Nimekuja na uthibitisho hapa unaonyesha jinsi wapinzani walivyo wanafiki.
Wanatuchanganya watanzania

Wao ndio walio ishauri serikali inunue ndege na kufufu ATCL leo tena hao hao ndio wapingaji wa ndege na ATCL.

Naomba niweke hii video kama ilivyo, niwaombeni dada zangu na kaka zangu wa upinzani hebu tizameni hii video. Hiki ndicho mlicho kizungumza katika bunge letu la awamu ya nne mkaja tena mkakizungumza katika bunge la awamu ya tano.

View attachment 1741271
Kiufupi akili yako ni fupi.

Full stop:
 
Wewe ndio hujui lolote, mkuu. Ungekua unajua lolote ungejieleza kwa weledi lakini kwasababu hujui lolote zaidi yangu basi ndio sababu unajieleza kwa jazba.
Umeanzisha mada usiyoweza kuitetea, ni vema ukapotea.
 
Walishauri mnunue ndege kwa cash?

Wapinzani ndio walishauri mnunue ndege kama mnavyonumua nyanya sokoni?

Yaan ulitaka serikali inunue ndege hizo kwa ? Maoni mengine ni ya ajabu sana !!
 
Back
Top Bottom