Wapinzani nendeni taratibu na Rais Samia

Uncle Araali

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
950
Reaction score
1,262
Nianze kwa kunukuu usemi wa wahenga usemao "Mjusi ukimkimbiza sana hugeuka na kuwa nyoka". Maana huru ya usemi huu ni kuwa mtu hata akiwa mwema au mpole kiasi gani,ukimchokoza sana anaweza kubadilika na kuwa mbaya sana.

Niseme wazi kuwa kwa sasa Tanzania inahitaji katiba mpya kuliko katika wakati wowote, hasa ikizingatiwa kuwa tumeonja chungu ya katiba iliyopo ambayo inatengeneza watawala badala ya viongozi. Majeraha ya utawala uliopita yanaonekana kila mahali na tiba yake ya kudumu ni katiba mpya, hasa iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.

Dai la vyama vya upinzani, hususani Chadema la kutaka katiba mpya ni la msingi sana.Changamoto niionayo mimi ni namna hiyo katiba mpya inavyoombwa kutoka kwa watawala. Nafahamu kuwa katiba mpya haitakiwi kuwa hisani ya watawala, lakini kwa kuwa katiba iliyopo inatulazimisha tuwaombe walioshikilia madaraka, nawaomba wapinzani na Watanzania wote wanaohitaji katiba mpya tutumie njia nzuri, tusiwe na haraka sana. Rais Samia ameonesha tangu awali kuwa ana nia njema na taifa letu na kwa muda mfupi ameleta ahueni katika taifa letu, hususani katika suala la haki na uhuru.

Niombe vyama vya upinzani viwe na subira na njia sahihi ya kuwakumbusha watawala kuhusiana na uhitaji wa katiba mpya. Maadam Rais amesema anaona umuhimu wa katiba mpya, vyama hivi viende naye taratibu, hasa ikizingatiwa amepokea nchi hii katika njia isiyo ya kawaida, hivyo kuna mambo mengi ya kushughulikia kabla ya kuipata katiba mpya. Naamini kabisa Rais wetu wa sasa ni msikivu sana,hivyo atatupatia katiba mpya.

Naomba kuwasilisha. Hoja haipigwi kwa nyundo.
 
Lengo la kundi la Mbowe ni kutaka kubabaisha utawala wa awamu ya 6 ili usifikie malengo waliyo jiwekea kwa wananchi na mwisho wa siku ionekane hakuna kilicho fanyika.

Katiba mpya hadi mwaka 2040 itakuwa wakati muafaka

Katiba mpya kwa sasa sio hitaji la watanzania bali ni hitaji la wanasiasa na haswa viongozi wa chadema kwa lengo la uchu wa madaraka.
Viongozi wa chadema wanacho waza wao ni jinsi gani watapata vyeo hawana habari na maendeleo ya wananchi.
 
Hakuna haja ya kubembeleza mtu. Chanmuhimu aheshimu katiba. Aruhusu vyama vya siasa vifanye kazi yake kwa mujibu wa katiba. Siyo kwa mujibu wa Samia na mawazo yakem

Otherwise kama mbwayi na iwe mbwayi. Potelea pweteee!
 
Kiukweli wanapaswa kuwa wastahimilivu, Rais anajua maumivu waliyopitia na hata ukiangalia Nia yake ni kuondokana na makovu makubwa yaliyoachwa mwilini na mioyoni mwa watu walioumizwa na utawala uliopita.

Ni vema sasa kufanya siasa za kustahimiliana na kuchukuliana kiutu sio kuanza vurugu na kejeli ambazo zitaondoa dhana nzima ya majadiliano ya kisiasa ya kistaarabu kwa mustakabali wa taifa letu.

Mwenye kisu kikali ndio huwa anakula nyama, ni vema wakasoma upepo kwanza. Rais anaweza kuwa na nia ya kufanya mambo ambayo wanataka, labda hata yeye anataka hivyo, Ila nae anabanwa na chama anachokiongoza, wapinzani ni vema waende kwa step za makini sana otherwise wanampush aamue kukataa kusikiliza mtu yeyote.

Sitamani turudi enzi za bwana yule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…