Uncle Araali
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 950
- 1,262
Nianze kwa kunukuu usemi wa wahenga usemao "Mjusi ukimkimbiza sana hugeuka na kuwa nyoka". Maana huru ya usemi huu ni kuwa mtu hata akiwa mwema au mpole kiasi gani,ukimchokoza sana anaweza kubadilika na kuwa mbaya sana.
Niseme wazi kuwa kwa sasa Tanzania inahitaji katiba mpya kuliko katika wakati wowote, hasa ikizingatiwa kuwa tumeonja chungu ya katiba iliyopo ambayo inatengeneza watawala badala ya viongozi. Majeraha ya utawala uliopita yanaonekana kila mahali na tiba yake ya kudumu ni katiba mpya, hasa iliyopendekezwa na Tume ya Warioba.
Dai la vyama vya upinzani, hususani Chadema la kutaka katiba mpya ni la msingi sana.Changamoto niionayo mimi ni namna hiyo katiba mpya inavyoombwa kutoka kwa watawala. Nafahamu kuwa katiba mpya haitakiwi kuwa hisani ya watawala, lakini kwa kuwa katiba iliyopo inatulazimisha tuwaombe walioshikilia madaraka, nawaomba wapinzani na Watanzania wote wanaohitaji katiba mpya tutumie njia nzuri, tusiwe na haraka sana. Rais Samia ameonesha tangu awali kuwa ana nia njema na taifa letu na kwa muda mfupi ameleta ahueni katika taifa letu, hususani katika suala la haki na uhuru.
Niombe vyama vya upinzani viwe na subira na njia sahihi ya kuwakumbusha watawala kuhusiana na uhitaji wa katiba mpya. Maadam Rais amesema anaona umuhimu wa katiba mpya, vyama hivi viende naye taratibu, hasa ikizingatiwa amepokea nchi hii katika njia isiyo ya kawaida, hivyo kuna mambo mengi ya kushughulikia kabla ya kuipata katiba mpya. Naamini kabisa Rais wetu wa sasa ni msikivu sana,hivyo atatupatia katiba mpya.
Naomba kuwasilisha. Hoja haipigwi kwa nyundo.