Wapinzani simameni na Rais sakata la Bomba la mafuta; Mabadiliko ya tabia nchi hayasababishwi na Bomba la mafuta pekee, wanaharakati wanatumika

Wapinzani simameni na Rais sakata la Bomba la mafuta; Mabadiliko ya tabia nchi hayasababishwi na Bomba la mafuta pekee, wanaharakati wanatumika

Kuna kale kabinti na wanamazingira wenzie kutoka Kenya, Poland, France na Germany wanajifanya kupinga huu mradi juzi nilikatumia meseji ya kukablust kutumiwa na wakenya akakujibu kitu, Kimsingi wakenya wanahusika sana na hii propaganda.
Hili bomba tutakuwa tunakula Transit fees zetu kwa miongo mingi hao Wanaharakati wa Mazingira wakawazuie INDIA biggest polluters.
 
Kuna kale kabinti na wanamazingira wenzie kutoka Kenya, Poland, France na Germany wanajifanya kupinga huu mradi juzi nilikatumia meseji ya kukablust kutumiwa na wakenya akakujibu kitu, Kimsingi wakenya wanahusika sana na hii propaganda.
Kuna kipindi rais wao alienda france kujifanya ziara tu ya kawaida lakini issue ilikua ni hilo bomba,hatari ukiwa na jirani mwenye roho mbaya ako kadada kanaitwa nani?
 
Majasusi wa Kenya wapo kazini.
Majasusi wa Tanzania wanalinda maslahi ya ccm.
Bomba la mafuta ni fursa yenye faida nyingi kwa sasa.
 
Kuna clip inatrend baada tu Mhe. RAIS kutoka nchini Uganda ikionyesha kikundi kidogo Cha watu wakipinga uwekezaji kwenye Bomba la mafuta eti Ufaransa Kuna joto Kali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hawa wazungu Sasa wamekosa hoja, kwamba tuache kufanya maendeleo kisa kwao Kuna joto. Mbona viwanda vyao vinatoa Moshi hakuna anayeandamana vifungwe? Ni nchi Gani Ulaya imewekeza kupunguza utoaji wa hewa chafu? Wao wawekeze sisi eti Bomba kulazwa chini linaharibu mazingira. Kwamba wanawaonea huruma watanzania wanaoishi Katibu na Bomba la mafuta, kwamba wanaonea huruma misitu karibu na Bomba; ulimbukeni.

Kwenye hoja kama hizi lazima tuungane kusema Tanzania niyetu siyo Yao. Hatuwezi Kuishi maskini kuwalinda wazungu no, hizi propaganda hapana.

Nchi nyingi zinamabomba kwanini Vita iwe TANZANIA? Nani yupo nyuma ya wanaharakati Hawa? Ni yapi malengo Yao? Tusonge Mbele na mama.

Economic intelligence unit hapa inahitajika kuundwa na kuingia Duniani, Tunahitaji intervention ya Dola kwenye hii hoja, Tunahitaji kuonyesha sovereignty yetu kama nchi, Tunahitaji kutoka ndani na kupeleka watu nje kufanya kazi nakushauri strategies, Tunahitaji kuwA Mbele ya Total kimkakati wasitusaliti, tupambane suala hili lifanikiwe; kufeli ni fedhea.

Mama usiondoke kwenda kwao wataandamana na kukuza popularity, tumia wanadiplomasia Ili wakifeli usionekane umefeli Moja Kwa Moja. Kuwa wa Mwisho kutokea kwenye camera, waachie akina January na Mulamula Maana ule upepo unavuma Kwa Kasi ya ajabu. Usiufuate tuma mgambo, polisi na majeshi ya akiba wachokonoe wakushauri tupite wapi tufanikiwe.

Mwisho, usiruhusu watu wakushawishi kuweka rehani rasilimali zetu au vitega uchumi Kwa Bomba hili, Bora tukose kuuza uzaliwa wa kwanza Kwa kikundi Cha watu wanaotumia wanaharakati. Bomba tunalitaka ila mikataba ya mashinikizo tupate uungwaji mkono hapana.
Mkipanga mipango yenu miovu huwa mnawatenga na kuwazodoa wapinzani, ila mambo yakianza kuwaendea kombo mnaanza kuwalaumu kuwa hawawaungi mkono. Kwanini mambo yanapokuwa mazuri mnawatenga
 
Shida mkuu sio kujitoa kwa total,hali iliyopo wanaharakati wanadai hilo bomba likipitia TZ litaharibu mazingira wanachotaka wao baada ya kufanikiwa lisipitie TZ liende kenya,sasa hapo uoni kama kuna sabotage ya kuukwamisha huu mradi kuja TZ?
4B80E97A-1612-43C3-A31C-A29B909BAFD3.jpeg


Mradi umeshafikia construction stage hadi costs ya route inajulikana na serikali ya Tanzania imelipa fidia maeneo ya njia ya bomba; kuvunja huo mkataba bila kigezo cha ‘contract frustration’ au any other reason beyond control ni swala la kushitikiana.

Either way ata kama ni frustration you would still need to compensate serikali ya Tanzania ukiachana na mradi kabisa.

Hilo bomba aliwezi badili njia kwa hatua project ilipofikia kwa sasa kama kuna mkenya anadhani hayo maamuzi yanaweza badilika at this stage of the project ni highly stupid it’s more than desperation na roho mbaya; but that decision won’t change or else it will be financially costly kwa mwekezaji for many reasons.

Kama ni mazingira kila siku makampuni ya mafuta wanamwaga mafuta kwa bahati mbaya na kuna huge environmental costs and damage to eco-systems. Huko Delta region Nigeria kila siku shida local wanatoboa bomba kuiba mafuta na gharama za spillage on environment anadaiwa BP.

Makampuni ya mafuta yanatumia zaidi $2 billion on clean bill za spillage duniani wanapambana na international environmental groups with global political influence na hawajaacha kuchimba mafuta wala kutafuta visima waje kumsikiliza mwanamke wazimu wa kikenya.
 
Kwa anayeelewa mradi wa bomba la mafuta ulishaonesha kufeli tangu kitambo kabisa kiasi cha miaka minne iliyopita na nimekuwa nawaambia watu mradi huo hautafanikiwa lakini hawaelewi. Kwa kifupi mno:

-Kuna trend nyingine inayoendelea ambayo watanzania wengi mno hawaielewi wakifikiri na mambo ya kufikirika au ya siku nyingi sana zijazo; haya ni masuala renewable energy. Suala hili limeshika kasi kubwa takribani miaka 5 sasa na nchi zote matajiri zilishajiwekea malengo ya kuachana na matumizi ya fossil fuels nchi ngingine kuanzia 2030, nyingine 2040, hadi 2050.

Sisi huku hatujui kuwa nchi zilizoendelea sasa zina discourage uwekezaji kwenye fossil fuels, tunaendelea kumshauri mama awekeze huko tunapotea sana.

-Tayari makampuni makubwa kama BP yalishajitoa kwenye uwekezaji wa bomba la Uganda-Tz. Pia mabenki makubwa ya kimataifa yalishajitoa hivi majuzi tu.

Haya yote ni wachache wanaelewa na wengine serikalini hawataki kuwa wazi kumshauri rais au kuwaambia wananchi.

Ukweli ni kwamba bomba hilo halitajengwa tena sasa zimebaki siasa za danganya toto zitakazoisha with time pekee.
ushasainiwa mara 6
 
Back
Top Bottom