Wapinzani Tanzania kumzodoa Raila ni kupoteza Dira na Mwelekeo

Wapinzani Tanzania kumzodoa Raila ni kupoteza Dira na Mwelekeo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Raila Odinga ni mpigania haki nguli wa wakati wetu. Amaarufu GOAT, kama alivyotambuliwa Messi Qatar, 2023.

Maneno ya Odinga kwa wafuasi wake ni sheria.

FvGkpo4WAAANb7T.jpeg

Leo wako mapumziko, kujipanga na kuja na nguvu mpya na kasi mpya. Tukutane kesho Tahrir.

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir

Screenshot_20230502-193822.jpg

Kwa mtu huyu tunayo ya kujifunza. Huyu siyo wa kubeza.

Screenshot_20230503-042635.jpg

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Ukurasa wake unajiongelea zaidi.

Screenshot_20230503-040703.jpg

Raila Odinga hawezi kubezwa na wapinzani uchwara walioingiwa na tamaa ya ubunge kwa maslahi binafsi. Wenye kuuwaza ubunge tu, tena kwa gharama yoyote? Kwamba hata kama ni kwa kuiuwa agenda yetu kipaumbele ya kupata katiba mpya sasa?!

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Wapinzani wa namna hii wana tofauti gani na wale 19 wasiokuwa na chama bungeni?

Kwamba kundi la wapinzani wasaka ubunge ndilo hilo lenye kumzodoa Odinga leo? What a coincidence?!

Ukombozi hupiganiwa. Kuna kupigania au kutopigania ukombozi. Ni hayo mawili tu.

Huwezi kuwa katikati.
 
Mtaji mkubwa alionao ni hao wafuasi wapumbavu wasioweza kutumia bongo zao. Huku tunawaita nyumbu.

Ukurasa wake wa Twitter una wafuasi 4.2M plus. Kina Karua, Uhuru, Musyoka nk yuko nao bega kwa bega na wanamwelewa vilivyo. Kenyatta (Mzee) alimfunga miaka mingi tu.

Moi hakuwahi kumgusa Kwa kumwelewa. Kibaki na Uhuru walifanya kushikana mikono naye.

Akiita maandamano nyomi si za mchezo.

Maajabu ni pale nyumbu wa ukweli anapomwita binadamu kuwa ni nyumbu.

Haipo shaka nyumbu ni wewe ndugu.
 
Nimeshindwa kuona connection ya uzi wako vs lawama kwa Wapinzani wa Tanzania! Kuna kitu nimemiss maybe!

Ukweli hauwezi kuwa mtamu:

Connection Iko hapa. Ni ajabu kuwa hata waliosadikiwa kuwa wapinzani kIndaki ndaki, leo wanamzodoa Raila na harakati zake huko kwao. Wengine wakimwitisha kupumzika, kumwita majina, nk.

(Waterloo nasema uongo ndugu yangu?).

Waangalie vizuri wapinzani hao wanaomzodoa Odinga. Mambuzi hao tunajua kwa nini wanafanya hivyo. Wapinzani wanaofanya hivyo wana kitu kimoja in common. Ni wasaka ubunge kwa gharama yoyote.

Wanaotaja ubunge, hawaipendi njia ya Odinga ya kupata haki au katiba mpya kwa kesi yetu. Kauli za kuwa bIla katiba mpya hakuna uchaguzi hawazitaki tena hata kuzisikia tu.

Wapinzani wanaomzodoa Odinga ni ndumila kuwili.

Wana tofauti gani hao na kina Mdee?
 
Okay ila at least ungemtaja MTU au ungekua more specific ingesaidia au ungetumia neno BAADHI maana siamini kuwa ni Wapinzani wote Tanzania.

Lakini pia sidhani pia kuwa na mtazamo tofauti ni udhaifu! Binafsi sina tatizo na Approach ya Mzee Laila au ya "Wapinzani wa Tanzania" maadam kama itawafikisha pale wanapotaka. Mfano, Approach ya Mzee Mbowe imesaidia Leo hii mikutano ya hadhara haileti maumivu yasiyo ya lazima Tena au uanzishwaji wa mchakato wa katiba mpya au kuachiliwa kwa baadhi ya Wanachama hayo kwangu ni mafanikio, siwezi kuyabeza! Same kama Mzee Raila Approach yake itamsaidia that's well and good. Hatuwezi kusafiria njia Moja wote.

Ukumbuke pia na ambalo wengi hawajui ni kwamba CCM walikua upande wa Raila kwa Kila kitu, I mean Kwa Kila kitu (wachache tunajua ukweli) japo nje wanahubiri tofauti, kwahio sioni tatizo hapo.
 
Odinga sio mpigania maslahi ya Taifa...kila kiongozi Africa anaonyeshaga ana wapigania watu akiwa hanaingia uongozini tulia aingie ndio mtakua manjiuliza huyu kawa vipi.
So Odinga asiwahadae na hilo wimbi kubwa alilonalo ni kwa sababu ya ukabila walionao wakenya.
 
Ukizungumzia wapinzani unawazungumzia hawa walio nyuma ya keyboard huku JF?

Basi kama ni hivyo naona unakosea, mimi nadhani wapinzani ni viongozi wao wa vyama vya siasa, ambao wao sijui wanasemaje..
 
Raila has become a notorious manipulator. Yes, a destabilizer.

Hafai wala hawakilishi tena "wapinzani" wa ukweli. He's long past his "best use before" time.

Kenya wamepotea njia kwa sasa.
 
Tatizo la Kenya ni ukabila uliokita mizizi

Hoja yako ingekuwa na maana kama Uhuru, Karua, Musyoka na wengi wengine wengekuwa kabila moja na Odinga.

Ni muhimu pia kutambua si Ruto, Gachagua au genge lao lenye kukubaliana nawe kwenye kauli hiyo.

Ni aibu Kwa watanzania kujidhania wako vizuri kisiasa kuliko Kenya au hata kuliko Odinga.

Ni bahati mbaya sana kuwa ulipo ungependa katiba mpya wakati unamdhania mpambanaji kama Odinga ni fala. Ya kwamba huna Cha kujifunza kutoka kwake.
 
Odinga sio mpigania maslahi ya Taifa...kila kiongozi Africa anaonyeshaga ana wapigania watu akiwa hanaingia uongozini tulia aingie ndio mtakua manjiuliza huyu kawa vipi.
So Odinga asiwahadae na hilo wimbi kubwa alilonalo ni kwa sababu ya ukabila walionao wakenya.
Odinga,again gia madarakani kwa njia ipi?. Au atatumia mapinduzi baridi?
 
Raila Odinga ni mpigania haki nguli wa wakati wetu. Amaarufu GOAT, kama alivyotambuliwa Messi Qatar, 2023.

Maneno ya Odinga kwa wafuasi wake ni sheria.

View attachment 2607965

Leo wako mapumziko, kujipanga na kuja na nguvu mpya na kasi mpya. Tukutane kesho Tahrir.

Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir

View attachment 2607968

Kwa mtu huyu tunayo ya kujifunza. Huyu siyo wa kubeza.

View attachment 2607969

Makamanda tunayo ya kujifunza kwa Raila Odinga

Ukurasa wake unajiongelea zaidi.

View attachment 2607970

Raila Odinga hawezi kubezwa na wapinzani uchwara walioingiwa na tamaa ya ubunge kwa maslahi binafsi. Wenye kuuwaza ubunge tu, tena kwa gharama yoyote? Kwamba hata kama ni kwa kuiuwa agenda yetu kipaumbele ya kupata katiba mpya sasa?!

Uchaguzi 2024/25 wa nini kama hakuna Katiba Mpya?

Wapinzani wa namna hii wana tofauti gani na wale 19 wasiokuwa na chama bungeni?

Kwamba kundi la wapinzani wasaka ubunge ndilo hilo lenye kumzodoa Odinga leo? What a coincidence?!

Ukombozi hupiganiwa. Kuna kupigania au kutopigania ukombozi. Ni hayo mawili tu.

Huwezi kuwa katikati.
sheria kwa wafuasi wake wapumbavu wa kabila lake ambao hawajashtuka kuwa huyo kikongwe anataka siku akifa awaache wakiwa mafukara wa kutupwa. Mwanasiasa gani nguli asiyeheshimu hata mamlaka? kumsifia raila kwa anayoyafanya sasa ni kielelezo cha mtu kuwa mjinga.
 
Back
Top Bottom