Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Uhuru na Karua hawakuwa na ushawishi wa kumpatia kura Odinga kutoka kwa Wakikuyu kama vile Gachagua alivyoweza kumletea kura nyingi Ruto. Raila alipiga hesabu zake vibaya za makabila ndio maana alishindwa.Hoja yako ingekuwa na maana kama Uhuru, Karua, Musyoka na wengi wengine wengekuwa kabila moja na Odinga.
Ni muhimu pia kutambua si Ruto, Gachagua au genge lao lenye kukubaliana nawe kwenye kauli hiyo.
Ni aibu Kwa watanzania kujidhania wako vizuri kisiasa kuliko Kenya au hata kuliko Odinga.
Ni bahati mbaya sana kuwa ulipo ungependa katiba mpya wakati unamdhania mpambanaji kama Odinga ni fala. Ya kwamba huna Cha kujifunza kutoka kwake.
Ukabila ndio huwa unamfanya Raila anashindwa siku zote na Wakikuyu na Wakalenjini kukalia kiti cha urais na makamu wa rais tangu uhuru. Yan Kenya tangu uhuru marais na makamu wake ni kutoka makabila mawili ya Wakikuyu na Wakalenjini tu!
Sasa huvi Ruto anajaza Wakalenjini katika serikali yake kila mahali, wizara ya nishati ya Kenya na mashirika yake nafasi zote muhimu za juu wamewekwa Wakalenjini. Hiyo haiwezi kuwa siasa nzuri, wana bahati wana kaunti kwa sasa angalau makabila mengine wanaambulia huko.