Wapinzani Tanzania kumzodoa Raila ni kupoteza Dira na Mwelekeo

Uhuru na Karua hawakuwa na ushawishi wa kumpatia kura Odinga kutoka kwa Wakikuyu kama vile Gachagua alivyoweza kumletea kura nyingi Ruto. Raila alipiga hesabu zake vibaya za makabila ndio maana alishindwa.
Ukabila ndio huwa unamfanya Raila anashindwa siku zote na Wakikuyu na Wakalenjini kukalia kiti cha urais na makamu wa rais tangu uhuru. Yan Kenya tangu uhuru marais na makamu wake ni kutoka makabila mawili ya Wakikuyu na Wakalenjini tu!

Sasa huvi Ruto anajaza Wakalenjini katika serikali yake kila mahali, wizara ya nishati ya Kenya na mashirika yake nafasi zote muhimu za juu wamewekwa Wakalenjini. Hiyo haiwezi kuwa siasa nzuri, wana bahati wana kaunti kwa sasa angalau makabila mengine wanaambulia huko.
 

Mkuu siasa siyo kuhusu majina yaani mtu au watu. Kusema CCM walikuwa nani hakuwezi kuwa sahihi milele.

CCM wakibadilika leo wakaikumbatia haki tunaungana nao tu. Suala ni kuwa nani anasema nini leo.

Mswahili anasema mla mla leo mla jana kala nini?

Kwamba hatuwezi kuwa na approach moja? Sijasema kutumia approach yake. Ninasema kumbeza, kumkebehi, kumdogosha, kumzodoa, nk.

Huko si sahihi na zaidi sana tulipaswa kumpongeza na hata kujifunza.

Nani atatupa katiba mpya tunayoitaka kwa wakati tunaotaka? Vipi zile kauli za hakuna katiba mpya hakuna uchaguzi zingalipo?

Tutenganishe watu na siasa. Agenda na malengo ni ya kudumu si watu.
 

Huoni aibu kudhani mtu mwenye wafuasi Twitter 4.2M + ni mjinga ila wewe?

Watanzania aliyeturoga alitupata kweri kweri!
 

Ulichoandika hapo hakuna mkenya anayekisema. Si Ruto, Gachagua au genge lao. Mnaliokoteza wapi ndugu?

Karua, Uhuru, Musyoka si wajaluo.



Unapasoma vizuri hapo?

Kwenye Twitter huyu mwamba ana followers 4.2M plus. Kigogo2014 anao wangapi? Wewe unao wangapi hata humu JF tu?

Raila ana ajenda zake zilizowavutia watu mbali mbali ambao sisi wengine tunawaita kuwa na kazi za laana.



Tembelea hapa kuziona agenda za Raila. Kufungua vyungu ni agenda moja tu.

Kenya kama kwetu, Maandamano halali na haramu sambamba leo

Zingatia Raila alifungwa miaka mingi hatimaye Kenyatta akamwachia. Moi hakumgusa zaidi ya kumvuta kushirikiana naye. Kibaki na Uhuru walishikana mikono.

Kwamba huyo mjinga ila wewe Yoda? Hata aibu kidogo hakuna wajomba?
 
Huoni aibu kudhani mtu mwenye wafuasi Twitter 4.2M + ni mjinga ila wewe?

Watanzania aliyeturoga alitupata kweri kweri!
aisee kumbe wewe ni mpu.mbavu na fala wa kiwango hiki? kwamba hao followers wa twitter wana impact kwa siasa za kenya? Wangekuwa na impact kwa nini Kura za raila hazikuwa nyingi sana kiasi cha kumzidi ruto au hujui hawa followers wa twiiter hata wajinga wajinga kama wewe ambao si wapiga kura wa kenya mumo?

Ujinga huo wa kuangalia wafuasi wa mitandaoni wasiyopiga kura ndiyo ulimponza Raila akabweteka akidhani serikali itamtangaza tu kuwa mshindi wa urais na sasa anaweweseka pamoja nanyi malofa wake.
 
Uko sahihi lakini pia ni ngumu ku-generalize au kutuhumu upinzani wote kwa ujumla wake si sahihi sana, unajua fika kuwa Kuna vyama vipo kwa maslahi yao binafsi, sasa Hawa watafuata upepo siku zote.

Pili, zile kauli za Vitisho ni nzuri ila pia Zina namna ya kuziweka, hazikufanya kazi mara ya kwanza ila sasa hivi bila hata zile kauli MCHAKATO UNAANZA mwezi July unless iwe ni changa la macho.
 

Mkuu hakuna niliposema wapinzani wote bali nimewalenga wanaomwona Odinga kama mpuuzi fulani.

Odinga ana wafuasi kwa maelfu wenye kumwelewa katika harakati zaje za kudai haki. Kulikoni kujiveka ujuaji kumponda huyo mwamba wa wenyewe?

Waulize wapondaji hao Wana nini au nini wamefanya wapi? Kimsingi CV zero.

Tafadhali unione katika mantiki sahihi.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Kua na wafuasi wengi kwenye mitandao yakijamii sio kipimo cha akili.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Usininukuu nje ya mada. Raila ni mwanasiasa. Raila siyo bongo fleva. Wafuasi wa Raila siyo wafuasi wa bongo fleva. Wafuasi wa Raila wanamfuatilia kisiasa. Ndiyo maana wito wa Raila una majibu ya kisiasa.

Ndiyo maana akiitisha Raila kinanuka hata kama Ruto au Gachagua haya ni maneno yao:

Your browser is not able to display this video.


Wewe una wafuasi wangapi ndugu? Hebu jaribu kuwaitisha kufanya jambo lolote kupima maji?

Msimwonee gele Odinga. Wivu huo Spika Sitta (rip) hakuwa na jina zuri nao.
 
Asante nimekuelewa Mjumbe. Nilihofia pale ulipotumia hii Wapinzani wa Tanzania. Nikutakie wakati mwema
 

Mjinga na mpumbavu ni wewe. Umeona kwenye list za sifa alizonazo Odinga ni followers peke yake? Zingine mbona umeziruka?

Kwamba ulipo huna lolote na hata follower nao ila huna bado unadhani ubora kuliko Odinga.

Kuna haja ya kujadili lolote na mtu kama wewe?

Wewe si ni Utingo lakini? Kwanza dereva wako yuko wapi? Haya yamekuzidi kimo.
 
Asante nimekuelewa Mjumbe. Nilihofia pale ulipotumia hii Wapinzani wa Tanzania. Nikutakie wakati mwema

Si sahihi kumwekea mtu maneno mdomoni ni vyema mtu akasema mwenyewe.

Si sahihi kumzodoa mpambanaji kama Odinga indicators zote zinaonyesha tungekuwa na Odinga mmoja tu, tumgeshakuwa na katiba mpya zamani.

Nina taabu na hizi nguchiro zenye kushupaza shingo na kujiona kuwa hata zina mawazo bora zaidi ya walio tayari kufa wakipigania haki zao makwao.

Mtu upo kwa mfuga mbwa huko, apeche alolo huna mbele wala nyuma mdomo mrefu kama wa tai kutwa zee jinga, Odinga mpuuzi nk.

Kwani werevu wa Mburumundu wa kijani Hawa bila kujali walipo uko wapi?

CV zao ziko wapi tulinganishe? Kwa sababu ya uchu wa u ubunge? Wengine sisi tuliamini kwenye katiba mpya kipaumbele na tungali tunaamini Hivyo.

Odinga si wa kubezwa. Huyo ni wa kupata shule.

Huyo kwenye region yetu leo ni GOAT.

Habari ndiyo hiyo.
 
 

Attachments

  • Kabila mbili Kenya.mp4
    11.2 MB

Unadhani Uhuru, Musyoka, Karua na wengi wengine wamekuja kwenye maandamano hayo kwa sababu uchwara hizo ndugu?

Hebu angalia clips mbili hizi. Hizo mbinu uchwara mbona zimeelezwa mno?

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.


Mbinu kama hizo ni za kudanganyana wenyewe Lumumba huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…