Wapinzani Tukipewa serikali tutaanzisha kodi mahususi kwa mambo mawili

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,408
Mwaka 2020 wapinzani tukishinda serikali tunawaahidi watanzania kuanzisha kodi mbili mahususi

1. Kodi ya Kuboresha Elimu

2. Kodi ya kuboresha Makazi

Kodi ya kuboresha Elimu

Miaka ya 80, 90 ilikuwa kusoma shule za serikali ni ufahali na kusoma shule za private ni fedheha lakini leo hii tunashuhudia kibao kimegeuka kusoma shule za private ndio ufahari huku kusoma za umma ni kama ishara ya kipato kidogo cha familia.

Changamoto sio status za familia bali mazingira ya kujifunzia wanafunzi katika shule hizi.

Nini kinaweka tofauti tangu enzi hizo mpaka leo ni "Uwekezaji unaofanywa na wamiliki wa shule hizo" zamani watu binafsi hawakuwa na mitaji ya kuwekeza kutengeneza mazingira bora ya elimu na hivyo kile kidogo ambacho serikali ilifanya kilitosha kutoa mazingira bora kulinganisha na private. Lakini leo hii uchumi umebadilika, elimu imekuwa biashara na watu binafsi wamewekeza na kutengeneza mazingira bora ya elimu na kugeuza kibao kusomeka kusomea shule za umma ni kama kuonyesha umasikini wa familia.

Swali ni je, hivi huu umma unaomiliki shule hizi za umma umeshindwa kweli kuboresha mazingira ya elimu katika shule za umma au kinachokosekana ni watu wenye vision na kuhamasisha watu kufanya wenyewe?

Wapinzani tunaamini kinachokosekana ni watu wenye vision na sisi wapinzani vision hiyo tunayo.

Kwanza tutaweka plani ya miaka 50 ijayo tunataka mwanafunzi wa shule ya umma asomee katika mazingira gani? Kama ni ubora wa madarasa, vifaa gani anahitaji vya elimu, vifaa gani anahitaji vya michezo, vifaa gani anahitaji vya kumjenga kijamii na kimaisha. tuta ainisha mtoto anatakiwa kutembea umbali gani kufuata shule na je ili mtoto asome vizuri anahitaji kukaa mazingira gani kama ni hosteli, au nyumbani au kuchanganya vvyote.

Baada ya kuwa na vision ya tunakotaka kwenda tutaanzisha kodi kwa ajili ya kuboresha elimu ambayo kila mtanzania atachangia na tunaamini tutaleta mabadiliko makubwa sana katika sekita ya elimu kwa watoto wetu na kubadili future ya watu wetu

2. Tunawaahidi kuanzisha kodi ya kuboresha makazi.

Inasikitisha sana leo hii kuona miji yetu inasambaa kwa kasi sana bila mpangilio wowote. kuna watanzania wako kwenye miji mikubwa hawana umeme, hawana maji, nyumba nyingi hazifikiwi na barabara.

Sisi wapinzani tunaamini maisha bora sio kukaa kwenye magorofa bali ni kila mwananchi kuishi "decent life" kulingana na kipato chake. Unaweza kuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule ikiwa imeezekwa kwa paa moja ukawa na maisha mazuri.

Sisi tunaamini tunaweza kusimamia ukuaji wa miji yetu na kuweka arrangement, usafi wa mazingira, tutaweka kanuni za makazi ambazo zitasimamiwa, tutaondoa utunzaji wa viwanja katikati ya miji.

Sisi tunaamini biashara ya ardhi inawapa watanzania maisha magumu, kuna watu wameshikilia viwanja maeneo ya karibu na hawajengi wakisubiri miaka isonge vipande bei na matokeo yake ni majirani kuzungukwa na mapori huku wanaotaka kujenga wakikimbilia mbali kutafuta unafuu wa bei. Huwezi kuacha mfumo wa makazi ukaendeshwa kiholela ukategemea watu wako waishi maisha bora.
 
Inshu ni optimum utilization of scarce resources kuna maeneo mengi ya kucover.

Kulenga huko tu kutasababisha haya malalamiko ya kuangalia sector moja au mbili na kuacha zingine.

Mimi naona tunahitaji sera zenye nguvu katika sekta zote na kuthamini backward and forward linkages.

Nitaeleza siku moja why hata viwanda vimefeli.
 
Upinzani.mungejua mulivyotuumiza na zile Kodi zenu za majengo mlipokamata halmashauri za dar,Arusha,moshi na mbeya na Iringa Sina hamu na nyie.Kodi zenu zilikuwa juu Hadi serikali ikaingilia Kati kuchukua Kodi zote za majengo ndio tukapata unafuu
 
Nusu ya watanzania wakiwa na uwezo wa kutoa tsh 100 kwa kwa miezi 3 na siku 10, yaani siku 100, matatizo yote ujinga, umasikini, maradhi, na akili yatakuwa historia.

Hivyo ni jukumu LA wana siasa kuunganisha watz kwanza, mbadala ya kutenishwa. Na naamini kwa njia ya kuhamasisha kila kitu chawezekana.

Huku diamond, huku Mbowe, huku Tulia

Pesa ya yaweza kukusanywa kwa njia ya siku na watumiaji ambao ni zaidi ya watu 45 mil

Natoa hoja
 
Inshu ni optimum utilization of scarce resources kuna maeneo mengi ya kucover.

Kulenga huko tu kutasababisha haya malalamiko ya kuangalia sector moja au mbili na kuacha zingine.

Mimi naona tunahitaji sera zenye nguvu katika sekta zote na kuthamini backward and forward linkages.

Nitaeleza siku moja why hata viwanda vimefeli.

Tunakubaliana kuwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo tunaweza kutofautiana "approach" na hilo ndilo linalozalisha vyama tofauti hizo ndizo itikadi na sote tutaunganishwa na jambo moja la kutaka kuwaletea wananchi maendeleo.

kwa mtizamo wetu kuna mambo ambayo tunatakiwa kuyapatia mtizamo wa kipekee ili sekita hizo ziweze kuleta tija. Hebu fikiria mfano mtanzania mmoja anaanza sekondari ambayo ni ya umma, shule hii haina maabara, au kama maabara ipo ni jengo tu hajawahi kufanya practical yoyote mpaka anamaliza kidato cha nne, shule hii ya umma unakuta haina walimu katika baadhi ya masomo, watu waliomaliza form 4 na wakafeli ndio wanachukuliwa kuwafundisha.

baada ya miaka minne mtoto mtanzania huyu tunamtungia mtihani kumpima ili tumwambie kama kafaulu au kafeli, hivi kweli mwanafunzi huyu kamaliza kidato cha nne kweli? Ndio maana sisi tunaona tunahitaji kuweka fungu maalumu la kutizama elimu yetu, tuhakikishe tunaitoa hapa tulipo na kuisogeza mahali palipo juu zaidi. tukiweka kodi maalumu kwa ajili ya hili tunajua hata watendaji wa serikali wakibadirika bado fungu hili litakuwa liko palepale. lakini tukitegemea maamuzi ya nani aliyeko madarakani kaweka kipaumbele wapi hatutafika popote. Hivyo wazo la kuanzisha kodi au tozo ya kuboresha elimu haliepukiki kama tunataka kuipeleka elimu yetu mbele.
 
Mawazo yako ni hatari sana, napenda nikuhakikishie mawazo yako juu ya elimu hayana tofauti na namna Magufuri anafikiria ki ujumla.

Magufuri ni ant-private sector, hili linaeleweka.
sasa wewe japo unajificha ficha, lakini una hurka za namna yake, ukipewa madaraka wewe unaweza kudisplay character hatarishi kuliko hata za magufuri.

Kuhusu elimu, kama umeona Secta Binafsi inafanya vizuri, kwa nini usiachilie mfumo mzima wa elimu usimamiwe na sekta hiyo, nyie mjikite kwenye strategic education issues.

waacheni sekta binafsi wapambane kwenye madarasa,madawani,n.k nyie mjikite kwenye mitaala, Tafiti, elimu za vyuo, na uwezeshaji?
 
Binafsi nimekuogopa sana na kamwe mtu kama wewe huwezi kupata nafasi katika serikali yetu iwapo wananchi wakitupa nafasi lakini nakushauri ubaki na msimamo wako huo ili wananchi wabaki kutazama ni sera ipi wanaikubali.

katika serikali yetu sisi mtu yeyote anayedhani shule za serikali zisiboreshwe, ziendelee kubaki na mazingira duni swala la kuboresha miundo mbinu ya elimu lifanywe na sekita binafsi tu sisi tunasema mtu mwenye mawazo hayo anastahili kufungwa jiwe la kusagia shingoni na kutoswa baharini.

Sisi tunaamini watanzania wote wanatakiwa kupata fursa sawa za kupata elimu bora. Mtu kupata elimu bora isiwe ni kipimo cha utajiri au kipato cha familia anakotoka kama ambavyo tunaona leo hii mtoto wa masikini, mkulima wa kijijini anasoma katika shule haina hata madawati ya kukalia, zipo shule zimeezekwa kwa nyasi, kuna wengine wanakaa kwenye miti huku wengine wakikaa katika mazingira ya kusomea kama vile wako ulaya.

Sera zetu hatuna haja ya kuwazuia sekita binafsi kuwekeza katika elimu kwa ukomo wanaouona wao lakini tunasema hilo isiwe kigezo cha watoto wetu kupata elimu ya ovyo eti wakitaka elimu bora waende shule binafsi. Mtu yeyote anayedhani public services zisiboreshwe ili private sector wafanye biashara hasa katika sekita muhimu kama Elimu, Afya, Maji, Umeme, Mawasiliano, Usafiri huyo sisi tunamuona ni mtu mwenye mawazo hatari kwa jamii na ndio maana tunadhani anastahili kufungwa jiwe la kusagia na kutoswa baharini

Watu kama hawa ndio wale waliokuwa wakiua tanesco ili private sector wafanye biashara ya majenereta, watu kama hao ndio waliokuwa wakiua reli ili malori yaendelee kusafirisha mizigo.

Hatuna nia ya kuua private sekita katika elimu bali tunasema watanzania wote kama mtoto wa primary anahitaji kufundishwa kompyuta basi kila anayemaliza darasa la saba awe anafahamu kutumia kompyuta, kama tunasema mtoto anayemaliza darasa la saba awe na uelewa fulani katika mambo haya basi wote wawe na uelewa huo.

malengo yetu si nani afanye nini, serikali tutafanya kinahitajika kufanyika hasa katika sekita muhimu kama elimu na afya.

kuna mambo mengine ni madogo lakini kwa "ignorance yetu hatufanyi"

nimepita mtaani mjini na kukuta watoto wa umri wa miaka 14 mpaka 19 wanacheza mpira wa kusukwa kwa nyuzina makratasi.?

nimejiuliza hivi mtoto mwenye umri kama huu kweli bado anacheza mpira wa makaratasi kweli? huo ni umri ambao ulaya mtoto kama huo anasajiliwa na timu kubwa kama simba na yanga sisi kwetu bado wanacheza mpira wa makaratsi????

Nimejiuliza hivi wazazi wa watoto hawa kweli wanashindwa kuchanga shilingi 2,000 (elfu mbili kwa kila mzazi au mlezi au kwa yeyote) watoto hawa wakacheza mpira sahihi ambao unaweza kuwaibua mastaa na pengine kuendesha maisha.

bado fikra zetu ni kujenga academy kubwa, kupata wafadhili lakini sisi wenyewe kufanya hata vitu basic ambavyo viko ndani ya uwezo wetu hatufanyi.

watoto wengi wenye akili wanapotea kwa mazingira ambayo tunawajengea, mtu umemwambia kafaulu unampeleka shule hakuna walimu, hakuna vifaa, hakuna vitabu ikiisha miaka minne unampa mtihani na kumwambia umefeli.
 
Mwaka 2020 wapinzani tukishinda serikali tunawaahidi watanzania kuanzisha kodi mbili mahususi

1. Kodi ya Kuboresha Elimu

2. Kodi ya kuboresha Makazi

Kodi ya kuboresha Elimu

Miaka ya 80, 90 ilikuwa kusoma shule za serikali ni ufahali na kusoma shule za private ni fedheha lakini leo hii tunashuhudia kibao kimegeuka kusoma shule za private ndio ufahari huku kusoma za umma ni kama ishara ya kipato kidogo cha familia.

Changamoto sio status za familia bali mazingira ya kujifunzia wanafunzi katika shule hizi.

Nini kinaweka tofauti tangu enzi hizo mpaka leo ni "Uwekezaji unaofanywa na wamiliki wa shule hizo" zamani watu binafsi hawakuwa na mitaji ya kuwekeza kutengeneza mazingira bora ya elimu na hivyo kile kidogo ambacho serikali ilifanya kilitosha kutoa mazingira bora kulinganisha na private. Lakini leo hii uchumi umebadilika, elimu imekuwa biashara na watu binafsi wamewekeza na kutengeneza mazingira bora ya elimu na kugeuza kibao kusomeka kusomea shule za umma ni kama kuonyesha umasikini wa familia.

Swali ni je, hivi huu umma unaomiliki shule hizi za umma umeshindwa kweli kuboresha mazingira ya elimu katika shule za umma au kinachokosekana ni watu wenye vision na kuhamasisha watu kufanya wenyewe?

Wapinzani tunaamini kinachokosekana ni watu wenye vision na sisi wapinzani vision hiyo tunayo.

Kwanza tutaweka plani ya miaka 50 ijayo tunataka mwanafunzi wa shule ya umma asomee katika mazingira gani? Kama ni ubora wa madarasa, vifaa gani anahitaji vya elimu, vifaa gani anahitaji vya michezo, vifaa gani anahitaji vya kumjenga kijamii na kimaisha. tuta ainisha mtoto anatakiwa kutembea umbali gani kufuata shule na je ili mtoto asome vizuri anahitaji kukaa mazingira gani kama ni hosteli, au nyumbani au kuchanganya vvyote.

Baada ya kuwa na vision ya tunakotaka kwenda tutaanzisha kodi kwa ajili ya kuboresha elimu ambayo kila mtanzania atachangia na tunaamini tutaleta mabadiliko makubwa sana katika sekita ya elimu kwa watoto wetu na kubadili future ya watu wetu

2. Tunawaahidi kuanzisha kodi ya kuboresha makazi.

Inasikitisha sana leo hii kuona miji yetu inasambaa kwa kasi sana bila mpangilio wowote. kuna watanzania wako kwenye miji mikubwa hawana umeme, hawana maji, nyumba nyingi hazifikiwi na barabara.

Sisi wapinzani tunaamini maisha bora sio kukaa kwenye magorofa bali ni kila mwananchi kuishi "decent life" kulingana na kipato chake. Unaweza kuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule ikiwa imeezekwa kwa paa moja ukawa na maisha mazuri.

Sisi tunaamini tunaweza kusimamia ukuaji wa miji yetu na kuweka arrangement, usafi wa mazingira, tutaweka kanuni za makazi ambazo zitasimamiwa, tutaondoa utunzaji wa viwanja katikati ya miji.

Sisi tunaamini biashara ya ardhi inawapa watanzania maisha magumu, kuna watu wameshikilia viwanja maeneo ya karibu na hawajengi wakisubiri miaka isonge vipande bei na matokeo yake ni majirani kuzungukwa na mapori huku wanaotaka kujenga wakikimbilia mbali kutafuta unafuu wa bei. Huwezi kuacha mfumo wa makazi ukaendeshwa kiholela ukategemea watu wako waishi maisha bora.
Wala shule za serikali hazijafa kwa sababu ya ukosefu wa pesa,bali shule nyingi za private ama zinamilikiwa na viongozi na makada wa ccm au viongozi wa ccm wanahisa kwenye shule hizo.So wameua shule za umma makusudi ili wafanye biashara
 
Upinzani.mungejua mulivyotuumiza na zile Kodi zenu za majengo mlipokamata halmashauri za dar,Arusha,moshi na mbeya na Iringa Sina hamu na nyie.Kodi zenu zilikuwa juu Hadi serikali ikaingilia Kati kuchukua Kodi zote za majengo ndio tukapata unafuu
Sioni kama tatizo ni kodi kuwa juu.Nchi yoyote dunia haijengwi kwa mikopo au misaada,bali inajengwa kwa kodi za wananchi.So swala la kodi kuwa kubwa kwa watu wenye akili si shida,shida ni kodi hiyo inatumikaje.Ukiwa na akili zako hata ukilipa kodi kiwango kidogo namna gani then akatokea mtu anakuwa anazigawa yeye tena pesa taslimu na bila kufata utaratibu lazima ikiboe mno
 
Umeshasema mpizani. Kwaiyo hata uje na story zakuwachukua walimu wote wa private wafundishe government sijui kama watakuelewa

Kuna watu wanavichwa vigumu

Ningesema hizi sera za watawala sasa si wangeniuliza mbona hawafanyi? Lakini tujenge utamaduni wa kujenga hoja na kushawishi wananchi kwa hoja.

ninaamini wapinzani tumekuwa tukikosea kwa kuchukua dhana ya upinzani kama ni kupinga serikali na matokeo yake ni kutokujenga hoja ili wananchi washawishike na pale mda wa kuchagua ukifika watupe nafasi bali sisi tumekuwa tukichukua maana ile ya kupinga kile serikali inachokifanya. Wao wakinunua ndege sisi tunabaki kuwaambia (kuwapinga) kwa nini mnunue ndege, wakijenga strigler sisi tunabaki kusema kwa nini mjenge stigle, wakijenga reli sisi tunahangaika kuwalazimisha wasijenge reli, hapo ndipo tulipo kosea. Kama wananchi waliyakubali haya na wananchi wanaona haya ni bora kwa sasa basi waache wajenge.

Sasa wapinzani tunakuja na approach mpya, ya kuwaacha wale walioko madarakani wafanye wanachoona sera zao zinasema na sisi tunawaomba kama wananchi wataamua kutupa nafasi basi watuache tufanye kile tutakachokuwa tumewaahidi wananchi kukifanya.

ikifika 2020 october tunaamini wananchi watahitaji mrejesho kujua yale mliyotuahidi kama kununua ndege, kujenga stigler, kujenga reli je mmefanya?

Lakini hilo sio kigezo cha kupewa nafasi tena bali wananchi watarudi kwenye kuchambua je unatuahidi nini katika miaka 5 inayokuja ya 2020 to 2025.

Sisi wapinzani kwanza tunawaambia yote mazuri ambayo yatakuwa yamefanywa na serikali zilizopita tutayaenzi na yale ambayo yatakuwa hayajakamilika tutayakamilisha. miradi mikubwa yote iliyoanzishwa na inayofanyika katika awamu zilizopita tutahakikisha inakamilika.

Tofauti yetu sisi na wenzetu ni kwamba hawawezi kuboresha zaidi ya hapo, sera zao ni zilezile hawatakuwa na jipya.

sisi tunawaeleza wananchi tunakuja kuboresha maisha ya mtanzania mmoja mmoja pamoja na kuboresha mazingira kwa ujumla ya uchumi wetu.

wakati ukifika tutawaomba waweke benchi wapumue kwanza, kiukweli wamefanya kazi nzuri ambayo watakumbukwa na watanzania siku zote ila wamechoka hawana jipya hivyo kunahitajika "super sub" ndio tufunge magoli ya kiuchumi.

Sisi tunasema huwezi kupeleka nchi kwa kasi kama hauna plan, kwamba ikifika mwezi wa 10 unaanza kusukuma watu wajenge madarasa ili mwezi wa kwanza watoto waingie, miji inajengwa hakuna plani kila mmoja anajenga anavyotaka, mvua zikitaka kunyesha ndio unawaambia wa mabondeni wahame, ukitaka kujenga miundombinu ndio unabomoa makazi ya watu.

sisi tunasema tutatengeneza tanzania ya miaka 50 au 100 ijayo tunataka ifananeje katika kila idara na hizo dira ndizo zitakuwa mwongozo wa kila anayetekeleza jambo la maendeleo lazima alenge kwenye dira yetu.

kila mwananchi tutahitaji ajue tunaelekea wapi na wao wajipange kusukuma maendeleo kwa kutizama dira yetu ya pamoja.

Serikali yetu sisi italenga kuwafanya watanzania kuishi kama malaika ili kufanya hivyo fedha mtazipata tena nyingi ila zitakuwa zikitumika nyingi pia.
 
Upinzani sio kupinga kila kitu

Ningesema hizi sera za watawala sasa si wangeniuliza mbona hawafanyi? Lakini tujenge utamaduni wa kujenga hoja na kushawishi wananchi kwa hoja.

ninaamini wapinzani tumekuwa tukikosea kwa kuchukua dhana ya upinzani kama ni kupinga serikali na matokeo yake ni kutokujenga hoja ili wananchi washawishike na pale mda wa kuchagua ukifika watupe nafasi bali sisi tumekuwa tukichukua maana ile ya kupinga kile serikali inachokifanya. Wao wakinunua ndege sisi tunabaki kuwaambia (kuwapinga) kwa nini mnunue ndege, wakijenga strigler sisi tunabaki kusema kwa nini mjenge stigle, wakijenga reli sisi tunahangaika kuwalazimisha wasijenge reli, hapo ndipo tulipo kosea. Kama wananchi waliyakubali haya na wananchi wanaona haya ni bora kwa sasa basi waache wajenge.

Sasa wapinzani tunakuja na approach mpya, ya kuwaacha wale walioko madarakani wafanye wanachoona sera zao zinasema na sisi tunawaomba kama wananchi wataamua kutupa nafasi basi watuache tufanye kile tutakachokuwa tumewaahidi wananchi kukifanya.

ikifika 2020 october tunaamini wananchi watahitaji mrejesho kujua yale mliyotuahidi kama kununua ndege, kujenga stigler, kujenga reli je mmefanya?

Lakini hilo sio kigezo cha kupewa nafasi tena bali wananchi watarudi kwenye kuchambua je unatuahidi nini katika miaka 5 inayokuja ya 2020 to 2025.

Sisi wapinzani kwanza tunawaambia yote mazuri ambayo yatakuwa yamefanywa na serikali zilizopita tutayaenzi na yale ambayo yatakuwa hayajakamilika tutayakamilisha. miradi mikubwa yote iliyoanzishwa na inayofanyika katika awamu zilizopita tutahakikisha inakamilika.

Tofauti yetu sisi na wenzetu ni kwamba hawawezi kuboresha zaidi ya hapo, sera zao ni zilezile hawatakuwa na jipya.

sisi tunawaeleza wananchi tunakuja kuboresha maisha ya mtanzania mmoja mmoja pamoja na kuboresha mazingira kwa ujumla ya uchumi wetu.

wakati ukifika tutawaomba waweke benchi wapumue kwanza, kiukweli wamefanya kazi nzuri ambayo watakumbukwa na watanzania siku zote ila wamechoka hawana jipya hivyo kunahitajika "super sub" ndio tufunge magoli ya kiuchumi.

Sisi tunasema huwezi kupeleka nchi kwa kasi kama hauna plan, kwamba ikifika mwezi wa 10 unaanza kusukuma watu wajenge madarasa ili mwezi wa kwanza watoto waingie, miji inajengwa hakuna plani kila mmoja anajenga anavyotaka, mvua zikitaka kunyesha ndio unawaambia wa mabondeni wahame, ukitaka kujenga miundombinu ndio unabomoa makazi ya watu.

sisi tunasema tutatengeneza tanzania ya miaka 50 au 100 ijayo tunataka ifananeje katika kila idara na hizo dira ndizo zitakuwa mwongozo wa kila anayetekeleza jambo la maendeleo lazima alenge kwenye dira yetu.

kila mwananchi tutahitaji ajue tunaelekea wapi na wao wajipange kusukuma maendeleo kwa kutizama dira yetu ya pamoja.

Serikali yetu sisi italenga kuwafanya watanzania kuishi kama malaika ili kufanya hivyo fedha mtazipata tena nyingi ila zitakuwa zikitumika nyingi pia.
 
Mwaka 2020 wapinzani tukishinda serikali tunawaahidi watanzania kuanzisha kodi mbili mahususi

1. Kodi ya Kuboresha Elimu

2. Kodi ya kuboresha Makazi

Kodi ya kuboresha Elimu

Miaka ya 80, 90 ilikuwa kusoma shule za serikali ni ufahali na kusoma shule za private ni fedheha lakini leo hii tunashuhudia kibao kimegeuka kusoma shule za private ndio ufahari huku kusoma za umma ni kama ishara ya kipato kidogo cha familia.

Changamoto sio status za familia bali mazingira ya kujifunzia wanafunzi katika shule hizi.

Nini kinaweka tofauti tangu enzi hizo mpaka leo ni "Uwekezaji unaofanywa na wamiliki wa shule hizo" zamani watu binafsi hawakuwa na mitaji ya kuwekeza kutengeneza mazingira bora ya elimu na hivyo kile kidogo ambacho serikali ilifanya kilitosha kutoa mazingira bora kulinganisha na private. Lakini leo hii uchumi umebadilika, elimu imekuwa biashara na watu binafsi wamewekeza na kutengeneza mazingira bora ya elimu na kugeuza kibao kusomeka kusomea shule za umma ni kama kuonyesha umasikini wa familia.

Swali ni je, hivi huu umma unaomiliki shule hizi za umma umeshindwa kweli kuboresha mazingira ya elimu katika shule za umma au kinachokosekana ni watu wenye vision na kuhamasisha watu kufanya wenyewe?

Wapinzani tunaamini kinachokosekana ni watu wenye vision na sisi wapinzani vision hiyo tunayo.

Kwanza tutaweka plani ya miaka 50 ijayo tunataka mwanafunzi wa shule ya umma asomee katika mazingira gani? Kama ni ubora wa madarasa, vifaa gani anahitaji vya elimu, vifaa gani anahitaji vya michezo, vifaa gani anahitaji vya kumjenga kijamii na kimaisha. tuta ainisha mtoto anatakiwa kutembea umbali gani kufuata shule na je ili mtoto asome vizuri anahitaji kukaa mazingira gani kama ni hosteli, au nyumbani au kuchanganya vvyote.

Baada ya kuwa na vision ya tunakotaka kwenda tutaanzisha kodi kwa ajili ya kuboresha elimu ambayo kila mtanzania atachangia na tunaamini tutaleta mabadiliko makubwa sana katika sekita ya elimu kwa watoto wetu na kubadili future ya watu wetu

2. Tunawaahidi kuanzisha kodi ya kuboresha makazi.

Inasikitisha sana leo hii kuona miji yetu inasambaa kwa kasi sana bila mpangilio wowote. kuna watanzania wako kwenye miji mikubwa hawana umeme, hawana maji, nyumba nyingi hazifikiwi na barabara.

Sisi wapinzani tunaamini maisha bora sio kukaa kwenye magorofa bali ni kila mwananchi kuishi "decent life" kulingana na kipato chake. Unaweza kuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule ikiwa imeezekwa kwa paa moja ukawa na maisha mazuri.

Sisi tunaamini tunaweza kusimamia ukuaji wa miji yetu na kuweka arrangement, usafi wa mazingira, tutaweka kanuni za makazi ambazo zitasimamiwa, tutaondoa utunzaji wa viwanja katikati ya miji.

Sisi tunaamini biashara ya ardhi inawapa watanzania maisha magumu, kuna watu wameshikilia viwanja maeneo ya karibu na hawajengi wakisubiri miaka isonge vipande bei na matokeo yake ni majirani kuzungukwa na mapori huku wanaotaka kujenga wakikimbilia mbali kutafuta unafuu wa bei. Huwezi kuacha mfumo wa makazi ukaendeshwa kiholela ukategemea watu wako waishi maisha bora.
Aisee kama mpango ni kuninyanganya viwanja vyangu kisa sijajenga wakati navilipia basi aisee kura yangu naiweka kuna MTU atakua na haja nayo
 
Tunakubaliana kuwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo tunaweza kutofautiana "approach" na hilo ndilo linalozalisha vyama tofauti hizo ndizo itikadi na sote tutaunganishwa na jambo moja la kutaka kuwaletea wananchi maendeleo.

kwa mtizamo wetu kuna mambo ambayo tunatakiwa kuyapatia mtizamo wa kipekee ili sekita hizo ziweze kuleta tija. Hebu fikiria mfano mtanzania mmoja anaanza sekondari ambayo ni ya umma, shule hii haina maabara, au kama maabara ipo ni jengo tu hajawahi kufanya practical yoyote mpaka anamaliza kidato cha nne, shule hii ya umma unakuta haina walimu katika baadhi ya masomo, watu waliomaliza form 4 na wakafeli ndio wanachukuliwa kuwafundisha.

baada ya miaka minne mtoto mtanzania huyu tunamtungia mtihani kumpima ili tumwambie kama kafaulu au kafeli, hivi kweli mwanafunzi huyu kamaliza kidato cha nne kweli? Ndio maana sisi tunaona tunahitaji kuweka fungu maalumu la kutizama elimu yetu, tuhakikishe tunaitoa hapa tulipo na kuisogeza mahali palipo juu zaidi. tukiweka kodi maalumu kwa ajili ya hili tunajua hata watendaji wa serikali wakibadirika bado fungu hili litakuwa liko palepale. lakini tukitegemea maamuzi ya nani aliyeko madarakani kaweka kipaumbele wapi hatutafika popote. Hivyo wazo la kuanzisha kodi au tozo ya kuboresha elimu haliepukiki kama tunataka kuipeleka elimu yetu mbele.

Ubora wa elimu sio kuwepo kwa maabara na wingi wa walimu bali ni kiwango cha elimu anachopewa mwanafuzi ambacho kitamsaidia kubuni njia mbalimbali za kutatua matatizo yake na nchi.

Ikiwa kuna maabara na walimu wengi alafu unafundisha fishing in Norway, what is stomata? form six sio suluhisho.
 
Hivi Mnao beza matokeo ya ufaulu wa shule binafsi na za serikali mnawaza nini serikari inabeba wanafunzi wote wa uelewa wa mwisho kati n.k shule binafsi wanachuja wanachukua bright tu kuna shule mwanao ili ajiunge lazima afanye mtihani na afaulu 90 and above kama tunataka ushindani fare wizara I pick randomly wanafunzi iwatawanye shule zote za gvt na binafsi alafu walimu wa hizo shule waingie kazini then tuone ufundishaji wa hizo shule we shule inachagua watoto wenye A tu unategemea itazalisha nini kama sio A tu
Aisee kama mpango ni kuninyanganya viwanja vyangu kisa sijajenga wakati navilipia basi aisee kura yangu naiweka kuna MTU atakua na haja nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2020 wapinzani tukishinda serikali tunawaahidi watanzania kuanzisha kodi mbili mahususi

1. Kodi ya Kuboresha Elimu

2. Kodi ya kuboresha Makazi

Kodi ya kuboresha Elimu

Miaka ya 80, 90 ilikuwa kusoma shule za serikali ni ufahali na kusoma shule za private ni fedheha lakini leo hii tunashuhudia kibao kimegeuka kusoma shule za private ndio ufahari huku kusoma za umma ni kama ishara ya kipato kidogo cha familia.

Changamoto sio status za familia bali mazingira ya kujifunzia wanafunzi katika shule hizi.

Nini kinaweka tofauti tangu enzi hizo mpaka leo ni "Uwekezaji unaofanywa na wamiliki wa shule hizo" zamani watu binafsi hawakuwa na mitaji ya kuwekeza kutengeneza mazingira bora ya elimu na hivyo kile kidogo ambacho serikali ilifanya kilitosha kutoa mazingira bora kulinganisha na private. Lakini leo hii uchumi umebadilika, elimu imekuwa biashara na watu binafsi wamewekeza na kutengeneza mazingira bora ya elimu na kugeuza kibao kusomeka kusomea shule za umma ni kama kuonyesha umasikini wa familia.

Swali ni je, hivi huu umma unaomiliki shule hizi za umma umeshindwa kweli kuboresha mazingira ya elimu katika shule za umma au kinachokosekana ni watu wenye vision na kuhamasisha watu kufanya wenyewe?

Wapinzani tunaamini kinachokosekana ni watu wenye vision na sisi wapinzani vision hiyo tunayo.

Kwanza tutaweka plani ya miaka 50 ijayo tunataka mwanafunzi wa shule ya umma asomee katika mazingira gani? Kama ni ubora wa madarasa, vifaa gani anahitaji vya elimu, vifaa gani anahitaji vya michezo, vifaa gani anahitaji vya kumjenga kijamii na kimaisha. tuta ainisha mtoto anatakiwa kutembea umbali gani kufuata shule na je ili mtoto asome vizuri anahitaji kukaa mazingira gani kama ni hosteli, au nyumbani au kuchanganya vvyote.

Baada ya kuwa na vision ya tunakotaka kwenda tutaanzisha kodi kwa ajili ya kuboresha elimu ambayo kila mtanzania atachangia na tunaamini tutaleta mabadiliko makubwa sana katika sekita ya elimu kwa watoto wetu na kubadili future ya watu wetu

2. Tunawaahidi kuanzisha kodi ya kuboresha makazi.

Inasikitisha sana leo hii kuona miji yetu inasambaa kwa kasi sana bila mpangilio wowote. kuna watanzania wako kwenye miji mikubwa hawana umeme, hawana maji, nyumba nyingi hazifikiwi na barabara.

Sisi wapinzani tunaamini maisha bora sio kukaa kwenye magorofa bali ni kila mwananchi kuishi "decent life" kulingana na kipato chake. Unaweza kuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule ikiwa imeezekwa kwa paa moja ukawa na maisha mazuri.

Sisi tunaamini tunaweza kusimamia ukuaji wa miji yetu na kuweka arrangement, usafi wa mazingira, tutaweka kanuni za makazi ambazo zitasimamiwa, tutaondoa utunzaji wa viwanja katikati ya miji.

Sisi tunaamini biashara ya ardhi inawapa watanzania maisha magumu, kuna watu wameshikilia viwanja maeneo ya karibu na hawajengi wakisubiri miaka isonge vipande bei na matokeo yake ni majirani kuzungukwa na mapori huku wanaotaka kujenga wakikimbilia mbali kutafuta unafuu wa bei. Huwezi kuacha mfumo wa makazi ukaendeshwa kiholela ukategemea watu wako waishi maisha bora.
Huyo Mwenyekiti wenu ni mkwepa kodi mkubwa,hiyo kodi si itaishia huko Machame kwenye mashamba ya maua
 
Back
Top Bottom