Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,993
muanze na zile pesa mlizopewa na yule tajiri sijui Sabodo alizotoa kuboresha maisha ya watz zikayeyushwa.....
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 2020 wapinzani tukishinda serikali tunawaahidi watanzania kuanzisha kodi mbili mahususi
1. Kodi ya Kuboresha Elimu
2. Kodi ya kuboresha Makazi
Kodi ya kuboresha Elimu
Miaka ya 80, 90 ilikuwa kusoma shule za serikali ni ufahali na kusoma shule za private ni fedheha lakini leo hii tunashuhudia kibao kimegeuka kusoma shule za private ndio ufahari huku kusoma za umma ni kama ishara ya kipato kidogo cha familia.
Changamoto sio status za familia bali mazingira ya kujifunzia wanafunzi katika shule hizi.
Nini kinaweka tofauti tangu enzi hizo mpaka leo ni "Uwekezaji unaofanywa na wamiliki wa shule hizo" zamani watu binafsi hawakuwa na mitaji ya kuwekeza kutengeneza mazingira bora ya elimu na hivyo kile kidogo ambacho serikali ilifanya kilitosha kutoa mazingira bora kulinganisha na private. Lakini leo hii uchumi umebadilika, elimu imekuwa biashara na watu binafsi wamewekeza na kutengeneza mazingira bora ya elimu na kugeuza kibao kusomeka kusomea shule za umma ni kama kuonyesha umasikini wa familia.
Swali ni je, hivi huu umma unaomiliki shule hizi za umma umeshindwa kweli kuboresha mazingira ya elimu katika shule za umma au kinachokosekana ni watu wenye vision na kuhamasisha watu kufanya wenyewe?
Wapinzani tunaamini kinachokosekana ni watu wenye vision na sisi wapinzani vision hiyo tunayo.
Kwanza tutaweka plani ya miaka 50 ijayo tunataka mwanafunzi wa shule ya umma asomee katika mazingira gani? Kama ni ubora wa madarasa, vifaa gani anahitaji vya elimu, vifaa gani anahitaji vya michezo, vifaa gani anahitaji vya kumjenga kijamii na kimaisha. tuta ainisha mtoto anatakiwa kutembea umbali gani kufuata shule na je ili mtoto asome vizuri anahitaji kukaa mazingira gani kama ni hosteli, au nyumbani au kuchanganya vvyote.
Baada ya kuwa na vision ya tunakotaka kwenda tutaanzisha kodi kwa ajili ya kuboresha elimu ambayo kila mtanzania atachangia na tunaamini tutaleta mabadiliko makubwa sana katika sekita ya elimu kwa watoto wetu na kubadili future ya watu wetu
2. Tunawaahidi kuanzisha kodi ya kuboresha makazi.
Inasikitisha sana leo hii kuona miji yetu inasambaa kwa kasi sana bila mpangilio wowote. kuna watanzania wako kwenye miji mikubwa hawana umeme, hawana maji, nyumba nyingi hazifikiwi na barabara.
Sisi wapinzani tunaamini maisha bora sio kukaa kwenye magorofa bali ni kila mwananchi kuishi "decent life" kulingana na kipato chake. Unaweza kuwa na nyumba ya vyumba viwili na sebule ikiwa imeezekwa kwa paa moja ukawa na maisha mazuri.
Sisi tunaamini tunaweza kusimamia ukuaji wa miji yetu na kuweka arrangement, usafi wa mazingira, tutaweka kanuni za makazi ambazo zitasimamiwa, tutaondoa utunzaji wa viwanja katikati ya miji.
Sisi tunaamini biashara ya ardhi inawapa watanzania maisha magumu, kuna watu wameshikilia viwanja maeneo ya karibu na hawajengi wakisubiri miaka isonge vipande bei na matokeo yake ni majirani kuzungukwa na mapori huku wanaotaka kujenga wakikimbilia mbali kutafuta unafuu wa bei. Huwezi kuacha mfumo wa makazi ukaendeshwa kiholela ukategemea watu wako waishi maisha bora.
Sent using Jamii Forums mobile app