Wapinzani tutulie na harakati zetu - ya nani spika hayatuhusu ndewe wala sikio ni lao hilo

Wapinzani tutulie na harakati zetu - ya nani spika hayatuhusu ndewe wala sikio ni lao hilo

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Naona wapiganaji maarufu huwa wanajikita katika mambo ya CCM, mpaka wafuasi tunapata khofu juu yao,inakuwaje hawa viongozi tunaowategemea wanaingilia mambo ya Chama Cha Mashetani (CCM), mpaka wanafikia kusema huyu anafaa huyu hafai,
hivi inakuwaje?

Huku uraiani tunashindwa kuwaelewa viongozi hawa wawe ACT au Chadema ni yao kwa yayo ,tungetegemea wanaitisha vikao na kutueleza wamefikia wapi katika malengo ya kuhakikisha tunapata Tume huru ya Uchaguzi, tunapata Katiba Mpya.

Sasa imekuwa ngoma inapigwa ndani ya CCM viongozi wa upinzani wanahemkwa na kuyavalia njuga mambo ya CCM, nilitegemea wasingekuwa wanayapa kipau mbele na kuyapuuza kama hawakuyasikia. Lakini sivyo wanawashinda hata CCM wenyewe kwa wanavyoyavamia.
 
Back
Top Bottom