Wapinzani wa kweli wa nchi hii ni Mbowe na Lissu

Wapinzani wa kweli wa nchi hii ni Mbowe na Lissu

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Habari ndo hiyo, hiyo miamba hapo juu ndo tafsiri haswa ya mpinzani wa nchi hii ni nani.

Ambaye hataki na anabisha kwa nnachokisema, aende akameze boga, akifanikiwa kulimeza basi mimi ni muongo na nipigwe mawe.

Upinzani wa kweli ni kutokuyumbishwa msimamo wako juu ya unachokiamini. Mbowe na Lissu wamepitia mengi sana ambayo yangetosha kuukana upinzani wao, lakini wameendelea kutoyumbishwa kiitikadi.

Angalia kituko cha leo cha ACT Wazalendo, sijawahi kuona jambo la hovyo kama walichokifanya leo. Yaani vile vitimbi vyote mpaka wasamaria wema wazanzibar wameuawa kikatili, halafu leo hii eti wanakubali kushirikiana tena na hao hao watesi wao? Hivi hii ni akili ya namna gani? Bado sijaona hekima iliyotumika hapa. Ni sawa tu nakusema na wao wamewatumia wazanzibari kama chambo ya wao kupiga 'Michongo'.

Bado naendelea kuwa na wasiwasi na upinzani wa Zitto Kabwe kwenye siasa, namkubali kama mtu anayejielewa kwenye issue nyingine za ki intellectual na kujenga hoja, ila kwenye upande wa itikadi halisi ya upinzani, napata shida sana kwamba akae kundi gani.
 
Mpinzani wa kweli na asiyeyumbishwa na chochote ni mmoja tu naye ni Hali ngumu ya kimaisha/uchumi.

Huyu mpinzani wa hali ngumu ya kimaisha yaani hanunuliki, hakamatiki, hatekwi, hapotezwi, hazimiwi internet, hana ubaguzi na wala hakuna wa kumyumbisha. Na bado anaendelea na harakati zake. Kwa sasa ni mitano tena.
 
Lisu huyuhuyu aliekimbilia kwa Amsterdam?

Mbowe kashindwa kuwaongoza watu wasiozidi 50 tena wanawake kina Mdee ndio mpinzani wa kweli?

Mwaka 2015 Mbowe na Lisu wadhalibadiri gia angani na kumkodishia Lowasa chama, hawa ndio wapinzani?

Hakuna kama Slaa! Yule mzee ni mtu na nusu. Siyo hawa wazee wa faraga.
 
Mpinzani kama mpinzani!
1765190.jpg
 
Wapinzani wa kweli hawajazaliwa nchini!

Hujui kama Mbowe alikuwa anahongwa pesa na Mzee Mkono ili asiweke mgombea ubunge wa chadema katika jimbo alilokuwa anagombea Mzee Mkono.

Unajipa matumaini ambayo hayapo!
 
Lissu ana chuki binafsi na Magufuli ndio maana baada ya Lowassa kutotambua matokeo Lissu alikwenda bungeni Mbowe hakuna mpinzani ruzuku ndio mpango!
 
Pole kwa kulitambua hilo leo. Mzee sawasawa tangu akiwa CUF hadi kesho jua ni mtu wa sirikali. Zitto umuone tu nakumuacha jinsi alivyo, Kama unabisha kamuulize Anna M. mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Kitala, Mwigambo na Shoza
 
Mbona CHADEMA madiwani walioshinda wameapishwa Tena bila masharti! Au mlitaka kuwaingiza mkenge ACT Wazalendo
 
Wapinzani wa kweli hawajazaliwa nchini!

Hujui kama Mbowe alikuwa anahongwa pesa na Mzee Mkono ili asiweke mgombea ubunge wa chadema katika jimbo alilokuwa anagombea Mzee Mkono.

Unajipa matumaini ambayo hayapo!

Duuu, bado una mifano ya kizamani ile mbaya, amka mzee baba hii ni karne ya 21, ww bado una mifano ya karne ya 20!
 
Mbaya zaidi, Mbowe alipewa na Rostam hela kukisaidia chama yeye akadai amekikopesha chama. Tuhuma hii ilitolewa na naibu katibu mkuu wa chadema wakati huo, na mtuhumiwa hakuwahi kuikanusha.
Nadhani hawa vijana wamezijua siasa za nchi hii kuanzia mwaka 2015!
 
Duuu, bado una mifano ya kizamani ile mbaya, amka mzee baba hii ni karne ya 21, ww bado una mifano ya karne ya 20!
Kwani hiyo mifano ilitokea kwenye karne ya 20?

Halafu karne haiondoki ukweli wa misimamo ya mtu! Kwa hiyo Mbowe kwenye karne ya 20 hakuwa mpinzani wa kweli na ilipofika karne ya 21 ndio akawa mpinzani wa kweli!

Tanzania tuna vituko!
 
Back
Top Bottom