Wapinzani wa kweli wa nchi hii ni Mbowe na Lissu

Mimi simshangai maalim seif kuikubal serekali hii, kwa sababu hali zote mbili keshaziishi. Na sisi wananchi ndio tunaoumia kwa hili maalim kalipatia kiukweli.

Kwenye kipindi SUK watu walikuwa wakipata ajira bila ya kujali wewe ni ccm au cuf lkn kufikia kipindi maalim kususia serekali, vijana wengi wamebaguliwa wazi wazi kwa sababu ya itikadi za wazee wao kuwa upizani.

Kwenye familia yangu wapo wahanga wa hayo wamefanyiwa hadi vetting lkn kwa sababu tu Baba yetu ni mpinzan ajira wamekosa.
 
Kwani hiyo mifano ilitokea kwenye karne ya 20?

Halafu karne haiondoki ukweli wa misimamo ya mtu! Kwa hiyo Mbowe kwenye karne ya 20 hakuwa mpinzani wa kweli na ilipofika karne ya 21 ndio akawa mpinzani wa kweli!

Tanzania tuna vituko!

Misimamo ya nchi yetu ilikuwaje dhidi ya Morocco kwenye suala la sahara Magharibi na sasa? Misimamo yetu dhidi ya Israel kuhusu Palestina na sasa ikoje? Labda tuanzie hapo.
 
Reactions: BAK
Muacheni mzee nae ale mema ya NCHI.

Kila uchaguzi wanamuibia acha ajibanze hapo hapo mpaka time Huru itakapopatikana.

VINGINEVYO atapoteza muda tu na umri unakwenda.ccm ni MASHETANI.
 
Lissu hawezi kuwa mfano wa kiongozi bora wa upinzani, Lissu ni kiongozi muoga haijapata kutokea katka siasa za Tanzania, amefika Belgium baada kutoka mafichoni mwa balozi wa Ujerumani na alipofika tu interview yake ya kwanza amemtambua Magufuli kama rais wa Tanzania na kumtaka Magu aunde serikali yenye ushirikiano ambayo haitawagawa wapinzani.,

Aliwatelekeza watanzania kwa mamilion waliomuunga mkono wakat wa kampeni mara baada ya uchaguzi hakuonekana tena

Mbowe kawatelekeza kina halima mdee viti maalum, sasa Chadema imeparaganyika kwa uongozi wake legelege, kwa hali ilivyo sasa Chadema sio siri imeanguka chini inabidi waanze mwanzo.,
 
Mbowe na Lissu ni inawezekana ni Wapinzani wa kweli dhidi ya Magufuli sio dhidi ya Mfumo

Kama vile Seif Sharif Hamad alivyokuwa mpinzani wa kweli dhidi ya Hayati Aboud Jumbe, Idrisa Abdulwakeel na Salmin Amour baada ya hapo kawa muigizaji tu
 
Yule Prof wa Kinyamwezi ndiyo mpinzani halisi aliebaki. Watu hawawezi kuukubali huu ukweli lakini ndio ukweli
 
Wapinzani wa kweli hawajazaliwa nchini!

Hujui kama Mbowe alikuwa anahongwa pesa na Mzee Mkono ili asiweke mgombea ubunge wa chadema katika jimbo alilokuwa anagombea Mzee Mkono.

Unajipa matumaini ambayo hayapo!
Leya ushahidi acha maneno matupu
 
Mpinzani wa kweli yuko mmoja tu. Ni Lissu tu.
 
Naunga mkono hoja Lissu au Mbowe sidhani kama watakuja kufika bei ila wengine siwapi dhamana aisee maana njaa mbaya!! Utakuja kusikia Heche,Sugu,Lema,Msigwa,Boniface jacob,John pambalu wameunga mkono JUHUDI.
 
Reactions: BAK
Hapo umenena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…