Una ushahidi au umerithishwa tu kelele walizopiga wenzako?Wapinzani wa kweli hawajazaliwa nchini!
Hujui kama Mbowe alikuwa anahongwa pesa na Mzee Mkono ili asiweke mgombea ubunge wa chadema katika jimbo alilokuwa anagombea Mzee Mkono.
Unajipa matumaini ambayo hayapo!
Kama hakuwahi kukanusha sasa si ndio ingekuwa vizuri muende mahakamani, mbona bado mnashangaa tu?!Mbaya zaidi, Mbowe alipewa na Rostam hela kukisaidia chama yeye akadai amekikopesha chama. Tuhuma hii ilitolewa na naibu katibu mkuu wa chadema wakati huo, na mtuhumiwa hakuwahi kuikanusha.
Nikikuajiri utaharibu kazi ili serikali yangu ionekane haifanyi kazi. Piga chini, utaajiriwa na uliemchagua na ndiye unayemwamini. Utaoaje mwanamke usiyekupenda?Mimi simshangai maalim seif kuikubal serekali hii, kwa sababu hali zote mbili keshaziishi.
Na sisi wananchi ndio tunaoumia kwa hili maalim kalipatia kiukweli...
Mbowe sawa lakini hiki kituko kipya kwenye siasa za Tanzania kinachoitwa Mboga ya WabeligijiHabari ndo hiyo, hiyo miamba hapo juu ndo tafsiri haswa ya mpinzani wa nchi hii ni nani...
NakaziaLisu huyuhuyu aliekimbilia kwa Amsterdam?
Mbowe kashindwa kuwaongoza watu wasiozidi 50 tena wanawake kina Mdee ndio mpinzani wa kweli?
Mwaka 2015 Mbowe na Lisu wadhalibadiri gia angani na kumkodishia Lowasa chama, hawa ndio wapinzani?
Hakuna kama Slaa! Yule mzee ni mtu na nusu. Siyo hawa wazee wa faraga.
Upo sahihi mkuuHabari ndo hiyo, hiyo miamba hapo juu ndo tafsiri haswa ya mpinzani wa nchi hii ni nani...
Wote hao ni CCMPole kwa kulitambua hilo leo. Mzee sawasawa tangu akiwa CUF hadi kesho jua ni mtu wa sirikali. Zitto umuone tu nakumuacha jinsi alivyo, Kama unabisha kamuulize Anna M. mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Kitala, Mwigambo na Shoza
Mgoja Mbowe ateuliwe mbunge Rais atoke mbio kuenda kuapishwaHabari ndo hiyo, hiyo miamba hapo juu ndo tafsiri haswa ya mpinzani wa nchi hii ni nani.
Ambaye hataki na anabisha kwa nnachokisema, aende akameze boga, akifanikiwa kulimeza basi mimi ni muongo na nipigwe mawe.
Upinzani wa kweli ni kutokuyumbishwa msimamo wako juu ya unachokiamini. Mbowe na Lissu wamepitia mengi sana ambayo yangetosha kuukana upinzani wao, lakini wameendelea kutoyumbishwa kiitikadi.
Angalia kituko cha leo cha ACT Wazalendo, sijawahi kuona jambo la hovyo kama walichokifanya leo. Yaani vile vitimbi vyote mpaka wasamaria wema wazanzibar wameuawa kikatili, halafu leo hii eti wanakubali kushirikiana tena na hao hao watesi wao? Hivi hii ni akili ya namna gani? Bado sijaona hekima iliyotumika hapa. Ni sawa tu nakusema na wao wamewatumia wazanzibari kama chambo ya wao kupiga 'Michongo'.
Bado naendelea kuwa na wasiwasi na upinzani wa Zitto Kabwe kwenye siasa, namkubali kama mtu anayejielewa kwenye issue nyingine za ki intellectual na kujenga hoja, ila kwenye upande wa itikadi halisi ya upinzani, napata shida sana kwamba akae kundi gani.