Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la Leo.
Kiukweli kabisa, upinzani Tanzania una hali mbaya sana, uko dholfu bin taaban kwa kukosa watu wa mikakati, hivyo kuendelea kufanya siasa za kiharakati kwa kutumia utopian politics!, badala ya kufanya siasa za kimikakati, matokeo yake ni kushindwa vibaya, na ni kwa zaidi ya miaka 30, upinzani umeshindwa kushika dola, upinzani huu unatakiwa kusaidiwa, bila kusaidiwa, uchaguzi wa 2025, unakwenda kuwa kama uchaguzi wa 2020, Bunge la 2025 litakosa tena kambi rasmi ya upinzani Bungeni, matokeo yake ni hasara wote, CCM, Nchi na Watanzania kwa ujumla.
Kukosekana kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kumepelekea kuwa na Bunge legelege, lisilo na uwezo wa kuisimamia serikali kikamilifu!. Bunge hili limekuwa linapitisha kitutusa, kila linacholetewa na serikali!.
Tungekuwa na wapinzani makini mule Bungeni, yale baadhi ya madudu ya ajabu.ajabu yaliyopitishwa na Bunge letu, kama kama ule Mkataba batili, kisha kuletewa muswada batili wa sheria mpya ya uchaguzi na kutunga kuwa sheria huku inakwenda kinyume na katiba yetu, yasingepita kabisa kirahisi ki vile!.
Leo nazungumzia umuhimu wa Tanzania kuwa na upinzani makini, upinzani imara na upinzani wa kweli kwa maendeleo ya taifa, bila kuwepo kwa upinzani imara, upinzani makini, hakutakuwa na CCM imara!, kwasababu imethibitishwa pasipo shaka, nchi zenye upinzani legelege, hupelekea vyama tawala kubweteka kwa kukosa changamoto, hivyo upinzani makini, imara na wa ukweli ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Hili limethibishwa na hili Bunge ambalo ni kama Bunge Rubber Stempu, linapitisha kila kitu hata madudu ya ajabu ajabu, hivyo kukosa msisimko, ili Bunge lichangamke, lazima baadhi ya wapinzani makini waingie Bungeni, Bunge lijalo liwe na kambi rasmi ya upinzani. Wapinzani wasiposaidiwa, uchaguzi wa 2025, utakuwa kama uchaguzi wa 2020!.
Kazi ya upinzani makini na upinzani wa kweli ni kupinga kwa kutumia hoja mbadala, na sio kupinga tuu ili mradi unapinga, upinzani makini unapinga kwa kutumia nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu, unapinga kwa hoja kwa kupangua hoja kwa hoja na wakati huo huo unaweka hoja mbadala ili kutoa changamoto kwa chama tawala kuwa tunakuangalia, ukishindwa unaondolewa!.
Upinzani wetu hapa Tanzania, una tatizo kwa wapinzani karibu wote, hawana hoja mbadala za kushindanisha na hoja za serikali, hivyo kuonekana kama upinzani wa kupiga tu kelele nawapinzani wengine karibu wote ni wapinzani wa kupinga tuu kila kitu bila kuwa na hoja mbadala, matokeo yake ni tuna upinzani uchwara usiotimiza majukumu ya upinzani makini, matokeo yake CCM kuutumia udhaifu wa upinzani wa aina hii kujiimarisha, uchaguzi mkuu wa 2025 upinzani usiposaidiwa, uchaguzi huu ni CCM tena!.
Kwa kuanzia kwanza tujifunze upinzani makini na wa kweli ni nini, unatakiwa kufanya nini, na upinzani legelege na uchwara ni nini, unafanya nini, kwanini Tanzania hatuna upinzani makini?
Tanzania tuna vyama 21 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.
Lengo kuu la vyama vyote vya siasa, ni kushika dola na kuongoza serikali yaani kutawala. Kila chama kinaandaa ilani yake ya uchaguzi kwa kueleza iwapo kitapewa ridhaa ya kutawala na wananchi, kupitia uchaguzi huru, na wa haki, kitafanya hivi na vile katika maeneo haya na yale.
Kazi ya chama tawala ni kuongoza serikali kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi, kazi ya upinzani makini duniani kote ni kupinga sera za chama tawala kwa hoja mbadala na sio kupinga tuu alimradi kupinga.
Hii imeifanya Tanzania kuwa na chama kimoja kikuu chenye nguvu, CCM ambacho ni kama dola, na vyama utitiri vya upinzani vinavyofanya siasa za uchwala, hali inayopelekea hakuna serious people wenye kutaka mabadiliko ya kweli, wanaweza kuviaminia kuvikabidhi nchi kutokana na kujikita kwenye siasa uchwara za matukio na kupinga tuu kila kitu badala ya kujikita kwenye siasa za kujenga hoja.
Upinzani makini unatakiwa kupinga hoja za serikali kwa hoja mbadala zenye mashiko, kwa upinzani huu wa kupinga tuu bila mbadala, nani atawaaminia wapinzani na kuwapa ridhaa?.
Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.
Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, ana strengths zake, (umahiri), ila pia ana madhaifu yake ambayo anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo wa kusaidia, ili Tundu Lissu, Chadema na wapinzani wengine, waweze kubadilika na kuachana na siasa za kiunaharakati na badala yake kufanya siasa za kimikakati ya kujiandaa kutawala.
Hivyo vibwagizo vya kiuanaharakati, kama “no reforms no election” vibwagiza hadaa (utopian politics) visivyotekelezeka!. Chadema na wapinzani wote, lazima wajikite kwenye kufanya siasa za ukweli, (real politics) ambazo ni siasa za mikakati, (politics of engagement), vinginevyo uchaguzi wa 2025, mambo ya 2020 yanakwenda kujirudia, na itakuwa ni CCM tena!.
Hivyo natoa wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kuwasaidia wapinzani, na kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze na pia kuwasaidia wapinzani wengine wote kufanya siasa za ukweli za kutaka kushika dola.
Kwenye kipindi hicho, TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!. Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.
Natoa wito, kwa watu wowote, wenye uwezo, kutoka popote hata wana CCM, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, kwa kuishauri kuwa uchaguzi mkuu wa 2025, Chadema ina fursa!, hii ni fursa adhimu na fursa adimu kwa Chadema kuichangamkia, muda uliobaki kabla ya uchaguzi, sio rafiki kufanya siasa za kiharakati, huu ni muda wa kufanya siasa za kimikakati ya ushindi, tena namshauri TAL na Chadama wakumbatie falsafa ya pragmatism politics, wawe pragmatic and do what is possible!.
TAL na Chadema na wapinzani wengine wote, wasaidiwe waachane na utopian politics, wafanye real politics, the time is almost too little too short!, hakuna muda wa kupoteza!.
Paskali.