Wapinzani waandaa hoja: Wamtaka Pinda kujiuzulu

Wapinzani waandaa hoja: Wamtaka Pinda kujiuzulu

Gembe: Kwa mwaka mzima sijaandika kitu chochote kuhusu Pinda. Niliapa wakati ule anateuliwa kumpa nafasi ya kufanya kazi yake bila kuanza kukosolewa (nilisema miezi sita, lakini nikaamua kukaa mwaka mzima). NI hadi alipotoa kauli hii ndipo nimeandika. Wakati mwingine nafikiri umeanza kujua kinachonisukuma, mara zote ukireact you prove me wrong.

Hili la kutaka kuvunja sheria wazi, ndiyo limenishtua kuwa a popular leader is the most dangerous.

Hoja imeshakuwa Nzito. We need a tape here ambayo inaeleza nini Waziri Mkuu alisema. Wote hapa tunashabikia jambo kwa kulisikia bila ya kuwa na usahihi wa habari yenyewe.

Pinda alizungmza Nini? We need a tape na hata Wewe ndugu yangu Kabwe Zitto Zuberi you can't judge a Person without kuwa na Ushahidi of what he said.

Mpaka sasa nasimamia kwenye upande wa Waziri Mkuu. Waziri Mkuu hana kosa hapa mpaka tutakapopata Tape!

Nimetafakari sana nafasi ya Pinda na Mkono wa wezi wa nchi hii na sasa naungana na wazo la Mzee Mwanakajiji. Mie nitatoa TSH 50,000 kwa yeyote atakeyeniletea tape!

Mwisho kwako zitto, Nchi inaelekea kukumbwa na janga la Njaa, Muulize PM ana Mpango gani na hilo!

I NEED A TAPE VERY SOON

Kama unayo niandike mkomboziufisadi-at-yahoo-dot-co-dot-uk
 
Wapinzani wa Tanzania kiboko, inaonekana wanakaa wanasubiria nani achemshe wamlime(IMHO).

Mkuu Icadon vipi kuhusu Bush kurushiwa kiatu, si kwasababu alichemsha? Tukitaka kujenga Taifa imara lenye heshma ni lazima viongozi wa kitaifa wawe clean na wenye uwezo wa kuongoza. Nchi kama China (licha ya kutokuwa na demokrasia), viongozi wao ni wawajibikaji sana, akikosea anajiuzuru mara moja au anaondolewa madaraka na kunyongwa. Ndo maana displine yao ipo juu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi yapo juu sana. Tena wanaomshughulikia ni hao hao chama tawala. Siyo kama sisi CCM kulindana tu, ndo maana wapinzani wamejaza hiyo nafasi. CCM wangekuwa wanawajibishana, wapinzani wangefanya mengine.
 
Hakusema nini alisema. Ninawaletea maneno yake verbatim (hansard) muone hasa kasema nini. Ninadhani kuna haja ya kumtaka aseme nini alisema (to restate what he said in Tabora). Unajua Bunge haliwezi kutumia kauli reported katika vyombo vya habari. Hivyo kuna haja ya kumtaka arudie alichosema Tabora ili hoja kutokuwa na imani ianze

Kwanini msubirie kuletewa nini alisema? Si kuna vyombo vya habari vilikuwepo lakini pia watu wa usalama wa taifa si huwa wanarekodi matukio katika ziara za waziri mkuu? Ofisi ya Spika ama ofisi ya kiongozi wa upinzani bungeni si muombe muletewe? Mkisubiri yeye aseme akiamua asiseme je?

Ndio mambo haya haya mpaka leo hamjaijadili hotuba ya Rais, mnasubiri awaletee aliyoikarabati toka Ikulu. Kikwete si alitoa ile hotuba yake bungeni na ilirushwa live? Kwanini msiende tu kwenye media kama TBC au Star TV mkachukue? Au wakiwanyima si muende tu kwenye makampuni yanayofanya off air recording?

Lakini yote kwa yote kwa kodi zetu wananchi si tunagharamia watu wa hansard pale Dodoma? Kazi gani wanafanya kama hawana hata kumbukumbu ya hotuba ya Rais iliyotolewa kwenye bunge?

Inawezekana Spika na wabunge wake mnashirikiana hapo kumlinda Rais Kikwete, hivi hotuba yake itajadiliwa tena? Au mtazugwa kuwa mkiijadili mnaingilia mambo ya mahakama kuhusu EPA?

ICADON: Haya ni makubwa kuliko kusubiri matukio, yanahusu KATIBA ya nchi na UTAWALA wa sheria. Hakutakuwa na sera wala maendeleo bila haya kuheshimiwa

Asha
 
BTW: Nimetaka la Pinda liende sambamba na la Kikwete kuvunja katiba na kudharau utawala wa sheria kwa kuwasamehe wezi walioghushi nyaraka kuiba fedha benki kuu na kurejesha. Zitto, ombeni na hotuba ya Rais iletwe bungeni ijadiliwe hata kama imepitwa na wakati kwa kuwa kuna kauli mbovu mbovu mule kuliko hata za Pinda.


Asha

Asha dada yangu, sio rahisi kumuingiza Rais kwenye uvunjaji wa sheria kama unavyosema. Kumbuka tu kwamba hakuna sheria iliyovunjwa kwa mtuhumiwa kutokufikishwa mahakamani. Sheria inavunjwa kwa kutenda kosa na sio kutokuchukua hatua.

Hata hivyo, sheria inamruhusu Rais kumfutia mtu yeyote makosa yoyote yanayomkabili. Sasa hata akihukumiwa, Rais akitaka anaweza kumsamehe makosa yote, bila kuwa amevunja sheria. Kazi kweli kweli.
 
Wapinzani wa Tanzania kiboko, inaonekana wanakaa wanasubiria nani achemshe wamlime(IMHO).

Hivi unataka sema kuwa kila mtu anayezungumzia kauli za Pinda kuwa alikosea ni mpinzani. Kama ndio una hayo mawazo ina maana likifanyika jambo baya kwa taifa, basi CCM wakae kimya, hapo hatuwezi kupiga hatua. Kuna mamo ya kitaifa hutakiwi angalia uko chama gani, manake yanatuathiri wote.
 
Unataka yeye ndio akwambie alichosema, unaanda hoja dhidi ya ulichosikia sikia Waziri Mkuu amesema halafu huna rekodi, huna hakika, hujui, alichosema!
Wakati mwingine huwa najiuliza kazi ya wapinzani ni kukosoa tu na kudandia mambo?
 
Hivi unataka sema kuwa kila mtu anayezungumzia kauli za Pinda kuwa alikosea ni mpinzani. Kama ndio una hayo mawazo ina maana likifanyika jambo baya kwa taifa, basi CCM wakae kimya, hapo hatuwezi kupiga hatua. Kuna mamo ya kitaifa hutakiwi angalia uko chama gani, manake yanatuathiri wote.

Rudi kasome alichoandika Asha Abdalla na Zitto.
FYI si kusema CCM vs Chadema nimesema Wapinzani waangalia nani amechemsha wamlime, so inaweza kuwa kati ya wapinzani kwa wapinzani etc etc...geez people are driven by emotions or what?
 
Taifa lisilokuwa na priorities... wote tunafahamu tuna matatizo ya uchumi tunaanza kupoteza muda na vitu visivyokuwa na vichwa wala miguu....

Hili jambo tena litawachukulia muda wapinzani...maskini ukikosa strategy kila linalotokea unalichukua.

Ningekuwa Mh.Pinda... najiandaa kujibu hilo swali la upinzani kwa natafuta hadithi nzuri na kuwachekesha wabunge tu... maana wakicheka watasahau kila kitu.....
 
Asha dada yangu, sio rahisi kumuingiza Rais kwenye uvunjaji wa sheria kama unavyosema. Kumbuka tu kwamba hakuna sheria iliyovunjwa kwa mtuhumiwa kutokufikishwa mahakamani. Sheria inavunjwa kwa kutenda kosa na sio kutokuchukua hatua.

Hata hivyo, sheria inamruhusu Rais kumfutia mtu yeyote makosa yoyote yanayomkabili. Sasa hata akihukumiwa, Rais akitaka anaweza kumsamehe makosa yote, bila kuwa amevunja sheria. Kazi kweli kweli.

Recta

Ukisoma vizuri sheria ya kudhibiti rushwa na ile ya maadili ya viongozi wa umma utaona makosa ya kuvunja sheria yanahusisha yale ya kutenda yasiyopaswa kutendwa na kutokutenda yanayopaswa kutenda. Ndio msingi wa hoja ya ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Kama Rais amekiri mwenyewe kuwa palikuwa na ufisadi na akamtuma katibu mkuu kiongozi kutoa maelezo marefu kwa umma kueleza hasira yake. Halafu Rais akaunda timu ya Mwanasheria Mkuu na Mkuu wa Polisi na wenzao, wakafanya uchunguzi wakabaini kuna wizi kweli. Halafu wakawaambia wezi walioghushi nyaraka warejeshe fedha halafu wezi hao wakarejesha. Halafu Rais akatangaza amewasamehe bila hata ya kuwapeleka mahakamani kwa kuwa wameonyesha ushirikiano. Unadhani Rais hapo hajavunja Katiba ya nchi na Sheria za jamhuri?

Kama angewasamehe kwa mamlaka yake ya kikatiba na kisheria ya amnesty/clemance hakuna ambaye angehoji.

Hotuba ya Kikwete ijadiliwe bungeni, kama si hotuba nzima basi wapinzani wachambue yale maeneo ambayo Rais ametoa kauli zenye kuvunja katiba na zenye kudharau utawala wa sheria wahoji kama walivyomhoji Waziri Mkuu Pinda.

Asha
 
WM amekwisha omba radhi. Labda kama kuna agenda nyingine. Wataalamu na wachambuzi wa KATIBA yetu ambao zamani mliiona haifai iandikwe upya kumbe imo mistari mle inakubalika hasa inapokuwa ni kumshughulikia WM, Rais,...
 
naona maneno yangu yana timia... oneni thread yaku ya siku nyingi kuhusu kauli za pinda... inapatika hapa https://www.jamiiforums.com/habari-...auli-zake-zilizopinda-hatma-ya-nchi-yetu.html
HTML:
[B][COLOR="Blue"][SIZE="5"]kauli za waziri mkuu pinda zinatia njia panda hatama ya nchi yetu.
kauli ya kuwa meremeta ni suala la usalama wa taifa haliwezi kujadiliwa bungeni wakati kampuni imesajiliwa visiwa vya uingereza na wakurugenzi ni wazungu inatisha. je usalama wa taifa umebinafsishwa? inatisha!!
kauli kuwa waliochota hela za EPA hawawezi kushtakiwa kwa sababu ya uwezo wao kifedha inatisha zaidi. je sheria za jinai ni kwa ajili ya maskini tu?
na hili la zanzibar si nchi sio geni watu walikuwa wanajua lakini kulizungumza kama kiongozi wa ngazi ya juu ya nchi inahitaji umakini kidogo si kuropoka tu. huyu jamaa kweli ni mwanasheria au tunadanganywa?
je tatizo ni hana washauri au ni mkurupukaji?
je kama huyu ndie anaemshauri rais wetu tutegemee nini?
kazi ipo[/SIZE][/COLOR][/B]
 
Taifa lisilokuwa na priorities... wote tunafahamu tuna matatizo ya uchumi tunaanza kuanza kupoteza muda na vitu visivyokuwa na vichwa wala miguu....

Priorities manake nini wewe? Viongozi wasiokuwa makini kwenye kauli zao unadhani watakuwa makini kwenye kutoa kauli za kutatua matatizo ya uchumi wetu?

Hapa priority ni kutaka uwajibikaji katika uongozi, tukishakuwa na huo uadilifu tutaweza kuwa na dira stahiki ya kuondokana na hilo zogo la kiuchumi.

Hawa ni viongozi wanaosema hakuna mtoto wa masikini atayeshindwa kusoma kutokana na umasikin wa wazazi wake halafu wanawarudisha watoto wa masikini nyumbani. Ndio viongozi hawa hawa wanaosema sasa hakuna mtanzania atakayekufa njaa, unadhani tunaweza kuwaamini? Tukiwaamini tutakufa njaa.

Kama serikali imenasalimu amri na kusema imeshindwa kuwalinda maalbino hivyo wananchi wachukue wenyewe sheria mkononi unadhani serikali hiyo inaweza kulinda uchumi wa nchi?

Tunataka wawajibike Bwana

Asha
 
Halafu mmenikumbusha, muulize na kauli yake kuwa Meremeta ni suala la ulinzi/usalama wa nchi. Tushughulikie suala la uongozi ili tuweke msingi mzuri wa kushughulikia masuala ya kilimo, elimu nk

Asha
 
Kesho kwenye kipindi cha maswali na majibu wabunge wanasubiri kwa hamu kusikia kama PInda atathubutu kutetea msimamo wake huo Bungeni au atakanusha.

- Mkuu Kuhani, nilikuwa nina-respond kutokana na hiki kipande hapo juu na sio anything else, maana kiko clear kuwa Pinda anahitaji kuthibitisha kwanza kuhusu hiyo kauli, sasa one more time naomba kukuuliza je aliithibitisha bungeni leo au? Kabla sijatoa hukumu?
 
Mkuu Gembe tutafakari pamoja...

ulianza hivi
Gembe 26th January 2009, 01:59 PM
KWa taarifa nilizo nazo ni kuwa Mwananchi na TAnzania Daima walimnukuu vibaya Waziri Mkuu,I mean wameelewa vibaya kauli aliyosema nakwa maana nyingine walikimblia kusema jambo la kufikirika kwanza.

Waziri mkuu alisema kuwa ili kukomesha mauaji ya Malbino unaweza tumia sheria Mkononi bila kusubiri mahakama.Sheria mknoni siyo kuua mtu ila hata kumkamata mtu ni kujichukulia sheria mkononi.

Naungana na maneno ya Mkapa aliyowahi kuyasema siku moja,Tanzania ya sasa imejaa watu wanopenda siasa za chuki,wanaweza eneza jambo fulani ili mtu flani achukiwe na Jamii hata akiwa ni mwema.

Na siku zote nimekuwa nikionya kuhusiana na Hili.Mwanakijiji na wewe unatak kukubali kutumika kwa hili kama mtaji?Na hii ndiyo sababu kubwa ya Watanzania kutochagua wapinzani hata kama CCM imewachosha..

ukaja hapa
Gembe 26th January 2009, 11:19 PM
Umeamua kuendeleza jambo lisilo na ukweli wowote.Nilikuonya asubuhi ila unaendelea tena kwa staili mpya,ulitaka kutumia pesa kupata habari ukashindwa..kwa faida ya nani sasa.?tujadili inshu za maana na siyo hili jambo lisilo na manufaa

tena
Gembe Yesterday, 09:13 PM
Umeona Maelezo ya Waziri Mkuu..Umeyakubali sasa?Mie nashangaa sana kulazimisha jambo wakati wewe mwenyewe hauwapo na unakataa na kulazimsiha jambo ulitakalo..Maswali yako yote ni speculations tu na hakuna hoja ya Msingi uliyouliza!

Gembe 26th January 2009, 11:25 PM
Hiyo pesa mchangie tu Maxenco kwa ajili ya JF.Au ipeleke Nyumbani.

unataka kusema kuna mpango flani umeandaliwa?

halafu
Gembe Yesterday, 09:13 PM
Umeona Maelezo ya Waziri Mkuu..Umeyakubali sasa?Mie nashangaa sana kulazimisha jambo wakati wewe mwenyewe hauwapo na unakataa na kulazimsiha jambo ulitakalo..Maswali yako yote ni speculations tu na hakuna hoja ya Msingi uliyouliza!

sasa upo hapa
Gembe Today, 04:03 PM
Pinda alizungmza Nini..We need atape na hata Wewe ndugu yangu Kabwe Zitto Zuberi you can't jugde a Person without kuwa na Ushahidi of what he said.

Nimetafakari sana nafasi ya Pinda na Mkono wa wezi wa nchi hii na sasa naungana na wazo la Mzee Mwanakajiji. Mie nitatoa TSH 50,000 kwa yeyote atakeyeniletea tape!

I NEED A TAPE VERY SOON

maendeleo mazuri...
 
1. Ni kweli Waziri Mkuu amelia. Lakini amelilia nini?

2. Anajua madhara ya kuvunja Katiba na hivyo anapaswa ama kujiuzulu au kuvuliwa Uwaziri Mkuu. Alikuwa analilia Uwaziri Mkuu......... Hakuwa analilia Albino.

3. Kama angekuwa analilia Albino, angelia huko ziarani na sio Bungeni alipoulizwa swali.

4. I like Pinda, but i can never ever entertain lawlessness. This is a constitutional Country, Pinda invites anarchy. We can not allow that.

- Mpaka hapa ninajaribu kuelewa.

5. Next is a special motion to ask Pinda to restate what he said. What exactly did he say about those who killed Albinos.

6. Leo kashindwa kakiri kiaina. We want him to say in Parliament, to restate his stand so that a no confidence process initiated.

- No hapa sasa sina uhakika, exactly kilichotokea ni nini hasa, amesema hakusema?

Tusithubutu kuruhusu viongozi kuropoka. We will be doing disservice to the country and invite killings, extra judicial killings. Viongozi wawajibike kwa maneno yao, kwa vitendo vyao na kutotenda kwao (words, actions and inactions)

- Ahhhhrrr! I am lost, amesema hakusema, alimaanisha hakumaanisha pleaseee! Mheshimiwa Zitto, sheria inasema nini kiongozi akiropoka? Hebu tuweke sawa mkuu kwamba na akiomba radhi inakuwaje?

Halafu nakuomba niko chini ya miguu yako, Je Pinda amesema au hakusema please?
 
- Mkuu Kuhani, nilikuwa nina-respond kutokana na hiki kipande hapo juu na sio anything else, maana kiko clear kuwa Pinda anahitaji kuthibitisha kwanza kuhusu hiyo kauli, sasa one more time naomba kukuuliza je aliithibitisha bungeni leo au? Kabla sijatoa hukumu?

Pinda nasikia kalialia tu huko bungeni. Hajarudia alichosema na sitegemei arudie.

Hivi Field Marshall mtu akikuripoti kwa Invisible kwa kutumia lugha chafu ni wewe ndio utaambiwa uthibitishe kwa Invisible maneno yako mwenyewe au huyo mripoti ndio atategemewa alete hizo rekodi zilizopo kwa kile unachodai umesema?

Unataka Pinda aji self-incriminate mwenyewe? Hivi unajua hata sisi tuna fifth amendment-like rights?

Who has the burden of proof here to show what was said, Pinda mwenyewe au hawa kina Zitto?

You tell me that.
 
- Kama amesema, na anajaribu kukwepa wajibu basi sheria ichukue mkondo wake, kwani sheria inasema nini on this ishu ya kiongozi mkuu kusema lugha ya kuhatarisha amani ya taifa?

- Hivi huyu si tumesikia kuwa alikuwa pembeni mwa Mwalimu Ikulu kwa muda mrefu sana as a qualification ya kuwa PM, au? Sasa unaona tunayoyasema kila wakati na hawa watu wa karibu sana na Mwalimu? Yaani mimi nawaita the Kingunge likes!
 
"Mwache Mwalimu apumzike..."

Unajua maneno ya nani hayo?
 
Back
Top Bottom