Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,584
- 6,136
Ndiyo maana nasema tunahitaji mtu kama PUTIN. Mbabe zaidi ya Mkapa ila anayependa sana nchi yake. Hii demokrasia kwa kweli katika nchi changa kama yetu naona inatumuka kivingine. Unaweza kukuta Pinda ni kiongozi mzuri ila si MWANA SIASA, watu wanakuja na kumuondoa na kumleta nduguye Lowassa.
Tujuwe kuheshimu watu hasa katika kipindi hiki cha mapigano. Hata USA wenyewe pamoja na kwamba CLINTON alidanganya, hawakukubali kumuondoa madarakani. Kosa kama lile lilifaa mtu kuadhibiwa au kupigwa warning. Sasa ona yanayoendelea.
Sijui kama Pinda kama kiongozi ni mtu wa aina gani zaidi ya yale tunayosoma. Ila kama ni kiongozi mzuri, basi tusifanye kosa la kumuondoa. Ila kama ni kumpa WARNING au adhabu ya aina yoyote, hilo nalikubali.
Wana siasa wa kweli huwa hawasemi. Putin mwenyewe wala maneno mengi hana. Anakuweka ndani, anakutumia majambazi yanakulima risasi, anakutumia makachezo na wanakunywesha Radio-active chemicals nk. Huyu ni MBAYA zaidi ya PINDA. Ila kuserma ukweli, heri ya PINDA anayesema UWA, kuliko hao waliofisadi nchi yetu na hadi leo wameshauwa watu wengi sana kwa watu kukosa maji safi, madawa, usafiri wa ovyo nk. Na kwa kukosa elimu, watanzania wanazidi kwenda chini.
Kama kuna agenda ya siri na mlikuwa mnasubiri pakutokea, na tusikie hayo MABAYA. Mwisho, nashindwa kuelewa kwa nini mnasema alikuwa ANALILIA U-PM? Hivi, mkipiga kura kumuondoa, Wapinzani mko zaidi ya nusu? Au ni kusema tu kuwa analilia madaraka? Kama CCM wakiamua kumtosa PM, basi nafikiri mkono wa Mafisadi utakuwepo, maana kwa CCM ya sasa, sijui kama watakubali PM wao wa pili aondoke na mwakani ni uchaguzi.