Wapinzani wangeliungana na Hayati Magufuli hakika tungelikuwa tushapata Tanzania Mpya, tatizo ni maslahi binafsi

Magufuli hakuwahi kutaka katiba tuache kudanganya watu.
Katiba kwa nchi za kiafrika sio tiba, level zetu zinahitaji viongozi wehu ila Wenye nia njema na uchungu na nchi zao, jirani mmoja ana Katiba inayodaiwa mpya kila siku majanga kisiasa. Jirani mwingine nchi ndogo inaendeshwa kidikteta, Maendeleo super karibu kila sekta, wamefikia mahali ukijaribu kumpa rushwa askari anakukamata, kila sehemu ni clean, shule zote watoto Wanatumia kompyuta, ujambazi zero
 

Mbona Kenya katiba inafuatwa, mbona south africa na Botswana katiba zinafuatwa. Kwanini sisi Africa tuna tofauti gani na binadamu wengine eti sisi tu ndiyo tusipende demokrasia? Sio kweli Mbona Waafrica waliopo diaspora wanafurahia hizo system na wengine wanakuwa hadi viongozi?
 

..kuna wapinzania waliomfuata Magufuli, au waliomuunga mkono, je, sasa hivi wana hali nzuri kisiasa kuliko kabla Magufuli hajaingia madarakani?

..Wapinzani kama Shibuda, Cheyo, na Mrema, walipata faida gani kwa kumuunga mkono Magufuli? Je, vyama vyao vina hali nzuri kuliko Chadema, Act, au Cuf?
 
Magufuli alikuwa na chuki ya wazi na wapinzani toka akiwa waziri. Hakuwahi kutaka kuungwa mkono kwa mantiki ya kuheshimiana na upinzani, bali alitaka aungwe mkono kwa kuua upinzani ili abaki akinyenyekewa.

Ugomvi wa Mafufuli ulianza rasmi siku anahutubia bunge kwa mara kwanza, kwani wapinzani walitoka nje kuonyesha kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar. Kitendo kile kilimuudhi sana, husda na chuki yake ya muda mrefu dhidi ya wapinzani ikawa dhahiri. Toka siku ile hakutaka uhusiano wowote na wapinzani bali alifanya too personal dhidi yao, na kuanza kuwa brand kama wasaliti. Hakutaka kuungwa mkono kwa maslahi ya taifa, bali alitaka kunyenyekewa. Msitake kupotosha kama hatukuwa na uelewa wowote.
 
Jiwe aliwahitaji sana wapinzani kuna kipindi walidai anatekeleza Ilani yao sema ni pinga pinga
Huu ujinga wa kuwa wapinzani wanapinga kila kitu uliienea sana kipindi cha Magufuli. Cha ajabu hata wasomi walihadaika na hii dhana ya upotoshaji! Hakuna mpinzani alipinga ujenzi wa barabara, shule nk. Hii dhana ya kupinga kila kitu ilitumika ili kufunika uovu wa Magufuli dhidi ya wapinzani waliokuwa wanasema udictator wake uchwara.
 
waliopinga mrad wa umeme ni watu gani waliokejeli fly over ni watu gani waliopinga ununuzi wa ndege ni kina nani waliopinga mradi wa sgr hadharan na mengine mengi wakidai anajenga kwao ni watu gani? Sio wapinzani? Haya magufuli aliua demokrasia samia amerejesha demokrasia.
 
Magufuli na huyo Samiah wote mashetani tu. Hakuna wa maana.
 
Acheni unafiki. Leo mnasema jiwe aliwahitaji wapinzani. Si ni huyo jiwe wenu alisema wapinzani wamechelewesha maendeleo Tanzania?. Acha unafiki wewe chawa wa magu
 
Unategemea wangemuunga mkono kina Mbowe wafaidika wa mfumo wa kifisadi nchini .. sasa hivi kahongwa mabilioni katulia anafanya siasa za drama tu..
Acheni unafiki. Leo mnasema jiwe aliwahitaji wapinzani. Si ni huyo jiwe wenu alisema wapinzani wamechelewesha maendeleo Tanzania?. Acha unafiki wewe chawa wa magu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…