Wapinzani wangeliungana na Hayati Magufuli hakika tungelikuwa tushapata Tanzania Mpya, tatizo ni maslahi binafsi

Wapinzani wangeliungana na Hayati Magufuli hakika tungelikuwa tushapata Tanzania Mpya, tatizo ni maslahi binafsi

Alisemaga hivyo baada ya kuona hawakuwa wakimuunga mkono kwa yale aliyokuwa akiyafanya japo yalikuwa ndio yale yale waliyokuwa wakiyahubiri wapinzani siku zote kabla ya JPM kushika madaraka !

Wapinzani walivyoona Jiwe anashangiliwa sana na Wananchi wakasema huyo Jiwe anafuata sera zetu !
Lakini wakaendelea kumpinga na kumponda badala ya kumuunga mkono !

Ndipo alipoona kumbe na hawa wapinzani ndio kama hao hao aliokuwa akipambana nao huko Serikalini na Chamani kwake !
Akaamua sasa ajitengenezee sapoti kutoka kwa Wananchi na kutoka kwa baadhi ya wale aliowainua kutoka Chamani kwake na upinzani !

Ukweli ni kwamba JPM alikuwa na nia ya kuibadilisha Nchi kabisa lakini alihitaji sana sapoti ya kutoka Upinzani ili aweze kuyatimiza yale aliyokuwa ameyakusudia !
Bahati mbaya Wapinzani walishindwa kumuelewa hata alipokuwa akiwashughulikia kweri kweri wa Chamani kwake lakini Wapinzani walishindwa kabisa kuusoma mchezo !
Wao wakaendelea na pinga pinga Jazz Band yao ndipo Ngosha akabadili ubao 😳🙄 !
Wapinzani wanafiki sana kwa kifupi
 
Very Interesting.

Yaani Magufuli Alitaka ushirikiano na wapinzani? Na kupatikana kwa katiba mpya?
Mbona mleta mada kaiweka kirahisi sana lakini ajabu imekua ngumu kueleweka.

Amesema “Laiti Kama wangemuunga mkono…”

Means the route that Marehemu was taking ni ile ile upinzani walikua lakini ajabu wakamkataa, but if wangemkubali basi ingekua rahisi zaidi Kwa upinzani kuiteka CCM from within maana nafasi aliwapa na aliendelea kuwapa.
 
Magufuli alikuwa na chuki ya wazi na wapinzani toka akiwa waziri. Hakuwahi kutaka kuungwa mkono kwa mantiki ya kuheshimiana na upinzani, bali alitaka aungwe mkono kwa kuua upinzani ili abaki akinyenyekewa.

Ugomvi wa Mafufuli ulianza rasmi siku anahutubia bunge kwa mara kwanza, kwani wapinzani walitoka nje kuonyesha kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar. Kitendo kile kilimuudhi sana, husda na chuki yake ya muda mrefu dhidi ya wapinzani ikawa dhahiri. Toka siku ile hakutaka uhusiano wowote na wapinzani bali alifanya too personal dhidi yao, na kuanza kuwa brand kama wasaliti. Hakutaka kuungwa mkono kwa maslahi ya taifa, bali alitaka kunyenyekewa. Msitake kupotosha kama hatukuwa na uelewa wowote.
Every action has an equal and opposite reaction, simple fact.

Walking away from the Nation's President in the middle of him addressing the Parliament + Nation, Live on the National Tv, who wouldn’t make it personal?

Considering all the facts he had at his disposal of all that was going on those hot days?!

Still he never let his hate blind his vision, the best were picked for Hapa kazi tu!

I’m sure if tables were turned, your reaction would be worse.

Ubaya ni mmbaya zaidi ukifanyiwa na unaye mjua na yeye anakujua na anajua unajua kwamba anakufanyia ubaya makusudi na cha kufanya huna maana unamjua nae anakujua na makusudi ya ubaya wake anajua unayajua na ujanja huna, njia yako Ndio njia yake, even a rat would panic in such a corner!
 
waliopinga mrad wa umeme ni watu gani waliokejeli fly over ni watu gani waliopinga ununuzi wa ndege ni kina nani waliopinga mradi wa sgr hadharan na mengine mengi wakidai anajenga kwao ni watu gani? Sio wapinzani? Haya magufuli aliua demokrasia samia amerejesha demokrasia.
Mradi wa umeme ulipingwa na wataalamu ww mazingira tena kwa riport rasmi ya kitaalamu, wakati huo January Makamba akiwa waziri. Mimi ni mmojawapo wa aliyepinga mradi wa umeme wa hilo bwawa, tena nikiwa na sababu za msingi. Kabla ya 2015 tuliimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas na bomba limefika hapa Dar, kumbuka tulikopa 2T kwa ajili ya mradi wa umeme wa gas. Na matatizo ya wakati ule kuhusu umeme wa maji ilikuwa ni mabadiliko ya tabia nchi. Wakati tukilishwa haya, Magufuli alikuwa kimya huko kwenye chama chake akilinda cheo.

Hadithi za umeme wa gas ilikuwa ni kupata 5,000m mpaka yeye anaingia madarakani kulikuwa 500m tayari za umeme wa gas, huku umeme wa Magufuli ikiwa 2,115m kwa 7t. Sasa kwa akili ya kawaida kwanini, tungeweka 3T tusingeweza kupata hizo 2,115m za kwenye umeme wa maji, tukaacha mazingira salama, na hizo 4T nyingine tuwekeze kwenye kilimo ama viwanda? Sasa nikuulize ww unayedhani kila mtu aliibeba hoja ile kwa mtazamo wa kipropaganda.
  1. Je kuna mabadiliko ya tabia nchi ama hakuna?
  2. Ni kwanini tuliwekeza 7T kwenye umeme wa maji ambao tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, tukaacha kuwekeza hela chini ya 7T kupata umeme zaidi ya 2,115m?
Ukitoa ufafanuzi wa hayo mawili, nitahamia kwenye hayo mengine uliyorukia kichwakichwa bila kujiuliza.
 
Mbona mleta mada kaiweka kirahisi sana lakini ajabu imekua ngumu kueleweka.

Amesema “Laiti Kama wangemuunga mkono…”

Means the route that Marehemu was taking ni ile ile upinzani walikua lakini ajabu wakamkataa, but if wangemkubali basi ingekua rahisi zaidi Kwa upinzani kuiteka CCM from within maana nafasi aliwapa na aliendelea kuwapa.
Nakumbuka Magufuli si mara moja alidai kuwa wapinzani wamechelewesha sana maendeleo kisha akapiga marufuku shughuli zote za kisiasa za vyama hadi kipindi kingine cha uchaguzi.

Alisema kufikia 2020 atakuwa ameumaliza kabisa upinzani! Kitu ambacho ni fallacy.

Pia alisema kabisa kuwa katiba mpya si kipaumbele chake ni hitaji la watu wanaotaka madaraka. Yeye kazi yake ni kuwaletea Watanzania maendeleo tu.

Hiyo ndiyo ilikuwa “route moja” ya Magufuli na wapinzani?

That was a very hostile and ominous construct for the opposition. Ni mtu anayewadharau sana wapinzani ndiye anayeweza kutegemea wamchangamkie na kushirikiana na mtu mwenye attitude na fikra za aina ile.
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
Hivi utawala uliopora haki za kuchagua Viongozi ni utawala gani?
 
Kwani kelele za wapinzani na wananchi kuhusu maendeleo ilikua nini siku zote kabla ya Magufuli?

Hivi unapoanza kufanyia kazi malalamiko ya watu then watu hao hao wakaanza kelele na kukuwekea mitego ujitele, wewe utawaelewaje hao watu?

Bado utataka waendelee kupiga hizo kelele za lawama ama wajiunge wafanye kazi ya kuyafanyia kazi makelele Yao?!

Any enemy is best conquered from within.
 
Every action has an equal and opposite reaction, simple fact.

Walking away from the Nation's President in the middle of him addressing the Parliament + Nation, Live on the National Tv, who wouldn’t make it personal?

Considering all the facts he had at his disposal of all that was going on those hot days?!

Still he never let his hate blind his vision, the best were picked for Hapa kazi tu!

I’m sure if tables were turned, your reaction would be worse.

Ubaya ni mmbaya zaidi ukifanyiwa na unaye mjua na yeye anakujua na anajua unajua kwamba anakufanyia ubaya makusudi na cha kufanya huna maana unamjua nae anakujua na makusudi ya ubaya wake anajua unayajua na ujanja huna, njia yako Ndio njia yake, even a rat would panic in such a corner!
Hao wapinzani wangekuwa wajinga sana kutokuonyesha hisia zao kwa mwenzao kuporwa ushindi wa halali. Na ile ilikuwa sehemu sahihi ya kuonyesha ukweli ule. Yaani ilikuwa ni approach ya kidemokrasia zaidi. Au unadhani kila mtu alipaswa kuwa kondoo kwa Magufuli?
 
Kuheshimu mamlaka na kufuata protocol katika kudai chako cha halali ni ukondoo?

Kwamba suluhisho ni kuonyesha utovu wa nidhamu mbele ya Rais mteuliwa siku ya kwanza akihutubia bunge na Taifa? Mbele ya wananchi kupitia Tv ya Taifa?

Hizo si Ndio siasa chafu tunazoongelea ama kuna nyingine?!
 
Kwani kelele za wapinzani na wananchi kuhusu maendeleo ilikua nini siku zote kabla ya Magufuli?

Hivi unapoanza kufanyia kazi malalamiko ya watu then watu hao hao wakaanza kelele na kukuwekea mitego ujitele, wewe utawaelewaje hao watu?

Bado utataka waendelee kupiga hizo kelele za lawama ama wajiunge wafanye kazi ya kuyafanyia kazi makelele Yao?!

Any enemy is best conquered from within.
Mkuu kumpenda Magufuli haina tatizo kabisa - kwa waliompenda, kumuelewa na kuwa wafuasi na mashabiki wake. Ni haki yao.

LAKINI kutarajia kuwa wapinzani nao walitakiwa kumuunga mkono na hivyo KUACHA KABISA KUIKOSOA SERIKALI ni kudharau sana intelligence na integrity ya wapinzani.

Na sio tu wapinzani walioko kwenye vyama vya upinzani (opposition) bali pamoja na wote wasio wanachama wa vyama, wanaharakati, na hata walio ndani ya chama tawala. Natumaini utanielewa.

That is my point.
 
Kabisa!..

Kuiokoa Tanzania inabidi kizazi cha kina Nape, Samia, JK, Makamba, Kinana, Membe, Makala, Nchimbi na makundi mengine yote yanauotafuna nchi yaliyojichimbia ndani ya ccm yapotezwe waje watu laini na wapya kama kina Bashiru ndio tuanze kutafuta katiba.

Kazi hiyo Magufuli alikuwa anaiwezea ila matahira ya chadema yakaungana na watesi kutoka ccm yakaanza kumwandama Magu.
 
Huu ujinga wa kuwa wapinzani wanapinga kila kitu uliienea sana kipindi cha Magufuli. Cha ajabu hata wasomi walihadaika na hii dhana ya upotoshaji! Hakuna mpinzani alipinga ujenzi wa barabara, shule nk. Hii dhana ya kupinga kila kitu ilitumika ili kufunika uovu wa Magufuli dhidi ya wapinzani waliokuwa wanasema udictator wake uchwara.
Mama anaupiga mwingi!

Nasikia mtashinda kwa kishindo uchaguzi selikali za mtaa maana toka aondoke jiwe haki imetawla kila mahali
 
Kuheshimu mamlaka na kufuata protocol katika kudai chako cha halali ni ukondoo?

Kwamba suluhisho ni kuonyesha utovu wa nidhamu mbele ya Rais mteuliwa siku ya kwanza akihutubia bunge na Taifa? Mbele ya wananchi kupitia Tv ya Taifa?

Hizo si Ndio siasa chafu tunazoongelea ama kuna nyingine?!
Rais sio Mungu, kama angekuwa ana heshima, huyo rais alipaswa kuheshimu hisia za walioporwa haki yao. Ww ndio unaona rais ni Mungu. Nyie ndio huwa mnatetemekea viongozi hawa majizi ya kura hadi wanaishia kujiona miungu watu.
 
Wewe unafikiri Magufuli ni wa kuungana na mtu?
Magufuli awezi kuungana na wapumbavu tu ndiyo maana hata wapumbavu walio chama chake walimchukia ...wewe unadhani samia alimchukia Jpm kwa sababu gani ....? Sikuzote viongozi uchaguana wenye akili uwachagua wenye akili kuongoza nao na kushaurian na viongozi wapumbavu uchaguana wapumbavu kuongoza na kushauriana ...mfano mshauri wa rais wako kwa sasa ni Mwigulu chemba ya mafii na bwana lukas msambwanda unategemea nini...
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
hivi hata ungekuwa wewe, unaunganaje na serikali yenye watu wasio na ubongo kama mabashite, masabaya, mamnyeti, maalihapi na mengine? unaunganaje na serikali ya one man show? watu wanapigwa risasi mchana eneo la nyumba za wabunge, watu wanapotea, uonevu wa wazi wazi....ungeunganaje? mimi wala siwalaumu.
 
Back
Top Bottom