Wapishi wa Kenya wavutiwa na mapishi ya Kichina wakati uhusiano wa kitamaduni ukishamiri

Wapishi wa Kenya wavutiwa na mapishi ya Kichina wakati uhusiano wa kitamaduni ukishamiri

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
20251031586e1429dc83476498e520d134af9d2b_20251031399babdfe9794c998c54e023fe6c92f8.png


Kama ambavyo tunafahamu, China nan chi za Afrika zimekuwa na ushirikiano na uhusiano unaogusa pande nyingi, ikiwemo elimu, kilimo, sayansi na teknolojia, biashara na uchumi, pamoja na masuala ya kitamaduni. Kupitia Taasisi za Confucius zilizoko nchi mbalimbali za Afrika, elimu ya lugha na utamaduni wa China imeweza kutoa mwanga wa utamaduni wa China katika nchi hizo.

Katika suala hili la utamaduni, tumeona jinsi utamaduni wa China unavyogusa nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika, na kubwa zaidi, ni kwamba Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina nayo imeongezwa kwenye kalenda ya matukio ya Umoja wa Mataifa, na katika baadhi ya nchi za Afrika, siku hiyo imekuwa ni siku ya mapumziko.

Kwa upande mwingine, chakula cha Kichina nacho kimekuwa na mvuto wa pekee kwa watu wengi, hususan wageni wanaotembelea China, ambao wanapendelea sana kuonja ladha ya kipekee ya chakula hicho. Hivi karibuni kule nchini Kenya, lilifanyika Shindano la Mapishi ya Vyakula vya Kichina, ambapo washiriki, wengi wao wakiwa ni wapishi, walionyesha ujuzi wao wa kupika vyakula vya Kichina.

Miongoni mwa wapishi hao ni James Wambua, ambaye akivalia mavazi rasmi ya wapishi, anatabasamu wakati akiweka nyama ya ng’ombe, samaki, mbogamboga na vitunguu kwenye sufuria kwa ajili ya kuvikaanga, ambavyo vinatoa harufu nzuri ya kupendeza. Wambua anasema, kwa karibu mwaka mmoja amekuwa akijifunza mapishi ya vyakula vya Kichina, na kuongeza kuwa, mashindano hayo yanavutia sana kwa kuwa wanaweza kujikita zaidi katika uelewa wa sanaa ya kuandaa, kupika, na kupakua vyakula vya aina tofauti vya Kichina.

Katika hoteli ya nyota tano ambako Wambua anafanya kazi, vyakula vya Kichina ni kawaida kuonekana katika meza za wateja, na ushiriki wake katika mashindano hayo ulitokana na shauku yake ya kufahamu vizuri vyakula ambavyo vinaweza kuwavutia zaidi wateja wake.

Mpishi mwingine aliyeshiriki mashindano hayo ni Pala Pala, ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia hiyo, anafurahia harufu nzuri kutokana na aina mbalimbali ya vyakula vya baharini, supu ya boga na samaki, ambavyo viko tayari ajili ya wateja. Chini ya maelekezo ya Wachina Pala Pala pia anaweza kuandaa nyama nya ng’ombe ya pilipili na mboga za majani, na anapakua vizuri kwenye sahani za chakula kwa ajili ya wageni kuonja. Mpishi huyu mchangamfu anasema amevutiwa na vyakula vya Kichina, ambavyo vina lishe nyingi.

Jesse Obara ni mpishi mwingine aliyeshiriki kwenye shindano hilo, na anaangalia nyama ya ng’ombe inayochemka ambayo imechanganywa na viungo vya kijani, anaigeuza kwa utaratibu ndani ya sufuria na hatimaye kuiweka kwenye sahani ya kupakulia. Akiwa ameboresha ujuzi wake wa mapishi kwa miaka mitatu katika migahawa mbalimbali jijini Nairobi, kijana huyo wa miaka 25 anaonekana akiwa mchangamfu na tayari kushiriki kwenye shindano hilo kwa mara ya kwanza. Anasema shindano hilo litamsaidia kukua katika taaluma na safari ya mapishi na wenzao wa Kichina.

Kenya imeandaa Shindano la Mapishi ya Kichina, likiwa ni shindano la kwanza la aina hiyo barani Afrika, na kuvutia timu 40 za washindani kutoka China, nchi kadhaa za Afrika, Australia na Marekani.

Kama sehemu ya Msimu wa mwaka 2025 wa Utalii na Utamaduni wa China na Kenya, tukio hilo la siku moja liliandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Dunia la Mapishi ya Kichina, Shirikisho la Mapishi ya Kenya na China na Utamaduni, na Chuo cha Utalii cha Kenya.
 
Hii habari ingefaa kuwepo kwenye jukwaa la mapishi. Vipi hao wapishi wameweza kupika konokono, nyoka, mende, majongoo na vyakula vingine vya ajabuajabu vya kichina?
 
Back
Top Bottom