Wapo wapi Neema Diwani, Flora Nducha na Misanya Dismas Bingi?

Wapo wapi Neema Diwani, Flora Nducha na Misanya Dismas Bingi?

Kipindi cha misanya Bingi nilikuwa siwezi sikiliza nikiwa na wazazi wangu ni aibu tupu matusi kejeli na kudharauliana .Bora alivyopotelea mbali nilifurahi sana alikuwa anajiona mjanja kumbe mjinga tu
 
Aaah ! Umenikumbusha mbali aisee ! Flora Nducha na Deo Mshigeni nilisota nao hapo Oljoro JKT (833 KJ) Tukiwa pamoja kombania G mwaka 1993. Mimi na
Deo tulikuwa mabwana shamba wa Bustani ya kombania. Siku yeye na Flora wanatoroka kwenda kufanya interview ITV nakumbuka aliniaga nikatunza siri.Namkumbuka SG Alex Mwambuluma, Copol Akioo, Sir major Busongo Bufumba , Major Mirudy na wengine. Jitokezeni basis tuliosota pamoja , Akina Mabara,Slivia Ndekana, Leopordina Sailo, Lazia Mwawanga, pritash Topiwala, Mazahil, Kara, Magina Sabaha, John simon na wengine.
 
Ma legendary hao, zamani hizo daaah
 
Ni kweli kabisa Dull
A yupo Kibo fm anakula shavu


Pia Dulla ndiye alikuwa meneja mwanzilishi wa Kili Fm, ilipopata umaarufu, akaenda kuwa meneja mwanzilishi wa Moshi Fm, then akaenda Kibo Fm, zote za Moshi
 
Back
Top Bottom