Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Habari zenu enyi makampuni ya huduma za mawasiliano. Nakuja kwenu kwa lengo la kuwapa wazo la kibiashara ambalo litaweza kuboresha huduma zenu kwa wateja, haswa kwa upande wa intaneti. Changamoto ambayo nyie makampuni mnayo ni urasimu haswa linapokuja suala la mtu mwenye nia ya kufanya kazi na nyie. Inafahamika mnaogopa sana suala la hakimiliki na kesi zinazohusiana na kipengele hicho kwa kuwa tayari mmeshapata sana changamoto maeneo hayo. Lakini tayari mnao wanasheria na sijui wanafanya kazi gani kuhakikisha maslahi yenu hayapati shida. Au ndio wanawashauri muweke urasimu kiasi hicho?
Kwa njia hiyo mtakosa sana ideas mpya katika soko hata kama mna wadau/agents mnaofanya nao kazi. Nao pia wana limitations zao kama hawatapata mawazo mapya, mradi tu wasiweke nao urasimu kama nyie. Nitawapatia wazo hapa na kama litakuwa muafaka kwenu ni vyema mkanitafuta inbox kwa ajili ya kujua tunayajenga vipi. Hii nayo itasaidia sana kuondoa usumbufu ambao mnaukimbia pale ambapo hapatakuwa na makubaliano rasmi.
Here is the Deal!
UTANGULIZI
Kumekuwepo na uhitaji wa matumizi ya intaneti kwenye simu janja kwa kiasi kikubwa kwa miaka ya karibuni. Hii kwa kiasi kikubwa imechangiwa na kampuni za simu kuboresha vifurushi vyao vya intaneti. Pili ni kutokana na watu wengi kumiliki simu janja. Kadhalika ni kutokana na kuwepo kwa watengenezaji maudhui wengi kuona fursa iliyopo kupitia mitandao mbalimbali Pamoja na application mbalimbali kama Tiktok, facebook, Instagram, WhatsApp, X, n.k. yote haya pamoja na mengine yamefanya matumizi ya intaneti kuongozeka.
Sambamba na matumizi hayo kuongezeka, kumekuwa na changamoto moja ambapo sio kila mmoja anaweza kumudu kununua bando ambalo litamtosha kutumia na kukamilisha mahitaji yake ya kimtandao. Hivyo wakati wa matumizi, mteja hujikuta anaishiwa bando na pengine asiwe na kiasi cha hela ambacho angeweza kununua bando kwa wakati huo. Wakati huo huo wapo watu ambao wana uwezo wa kuwa na bando la kutosha na ziada juu. Ndipo wazo la kumpunguzia mteja mwingine bando la intaneti likaja. Wazo tuliite NIBANDIKE TAFADHALI.
UHAMISHAJI WA SALIO LA KIFURUSHI CHA INTANETI KWENYE SIMU
Kwa sasa mteja anapoishiwa kifurushi cha intaneti, atamwomba mtu wake wa karibu amuunganishe kwa njia ya tethering, na mlengwa atapata huduma hiyo kwa muda huo na kwa eneo hilo alipo kutegemea na uwezo wa wi-fi. Changamoto ya njia hii ni kwamba mhitaji ni lazima awe Jirani sana na msaidizi wake. Lakini kwa huduma ya NIBANDIKE, ujumbe utatumwa kama wa kawaida kwenye huduma zingine na mhitaji atapunguziwa kiasi cha bando aliloomba bila kujali yuko wapi.
NINI KIFANYIKE
Kwa mara nyingine mteja anapoishiwa bando la intaneti atatuma ujumbe kwa mtu wake wa karibu kuomba ampunguzie kiasi cha data ili akamilishe hitaji lake. Ili zoezi zima lisiathiri biashara ya kampuni na pia kuleta usumbufu kwa msaidizi, ni lazima pawepo na taratibu zitakazopaswa kufuatwa, kwa maana ya vigezo na masharti kuzingatiwa. Hii ni kama ifuatavyo;
Mpango huu utaleta faida kwa kampuni kama ifuatavyo;
HASARA
Hakuna hasara.
HITIMISHO
Wateja wana michango yao katika kuboresha huduma za biashara za makampuni ambayo wanapata huduma na bidhaa. Ni wakati sasa wa kuyaangalia mahitaji ya wateja katika kona hii ili kuweza kuwaboreshea huduma zao, hasa katika matumizi ya intaneti pale ambapo wamefikwa na uhitaji sana na hawana suluhisho la haraka.
Pale mtakapoona wazo hili ni bora na linafaa kufanyiwa kazi, msisite kufanya hivyo, pakiwepo na makubaliano ya pande mbili kwenye utekelezaji wa wazo hili.
©2024

WAZO LA KIMKAKATI
HUDUMA YA KUMPUNGUZIA MTEJA BANDO LA INTANETI KATIKA MITANDAO YA SIMU

19/10/2024

- Kiasi cha juu cha mteja kuomba kupunguziwa bando kisizidi MB 1000
- Muombaji ataomba mara moja kwa siku.
- Ili pia kampuni iweze kufaidika na zoezi hili, itaweza kutoza kiasi kidogo cha gharama ya hamisho la bando.
- Njia zingine ambazo kampuni inaweza kuona ni sahihi katika kuboresha huduma hii.
Mpango huu utaleta faida kwa kampuni kama ifuatavyo;
- Pale ambapo wateja wataona kampuni imewajali katika hali zao na kuwawezesha kutatua shida zao za matumizi ya intaneti kwa muda huo bila kujali umbali.
- Kuiongezea kampuni kipato kupitia tozo za hamisho la bando
- Kuongeza matumizi ya intaneti ambapo itapelekea kuongezeka kwa ununuzi wa bando za intaneti
- Faida zingine ambazo kampuni inaweza kuziona kupitia mpango huu.