Hahahahahaha! M2 na M3 kiboko! eti wapewe 2 milioni waanzishe kimradi! hivi Toyo zinauzwa bei gani? Siasa bana :smile-big:
Duh Zitto na Dr Kitila wanajua spinning kwa hali ya juu , yaani wamekaa wakataka kupre empty taarifa ya waraka kwa umma wamemwaga kwenye mitandao waraka feki wanachotaka kusoma hali ya wananchi wanasemeje aibu Dr Kitilla heshima yote uliyojijengea nchi hii kumbe ni feki you are too local
Anakutisha wewe na MA------ yako...
kidoogo!!!! naanza kuliona na mimi hili , yangekuwa mabomu wangeenda haraka kutoa ufafanuzi , lakini kwa hili la ZZK , midomo mizitoDr. Slaa mnafiki sana. Yeye ndio mchochezi wa vurugu zote hizi lakini leo anajifanya kamuachia Tundu Lissu ndio atoe taarifa kwa waandishi.
Dr. Slaa ni mwanasiasa mlaghai...
Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.
Wafukuzwe tu, na mimi nasema wafukuzwe. Kitila, Zitto, M2, etc. wameikuta CHADEMA na wataiacha CHADEMA ikiwa na nguvu ile ile.
Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.
Ngoja hili liripuke;
hapana alifikisha 60 yrs,akaomba contract akanyimwa
Hii itakuwa fedha ya visima ya Mzee Sabodo:
Sangara,
Kama hayo yangekuwwepo na kama ni makosa yangeidhinishwa kwenye sababu za kuwafukuza. Majungu utayajua tu maana yanaandikwa kwa muelekeo wa kumchafua mtu.
Jadili hoja ya Dr. Kitila inayosema kuwa, wakati umefika kumuondoa Mbowe na kuwa na uongozi wa wasomi.
Kwenye Swala la Usomi Kitila Kajiexpose? Mapungufu yaliyokwenye waraka husika yanavua nguo qualify ya elimu yake. He has disgraced himself.
Kivipi, hebu tuelezee alichoandika kinachoondoa degree zake 3.
Kaonyesha namna uwelewa wake wa dhana ya Democrasia ulivyo mdogo, achilia mbali mazingira yote ya kwamba anachokipigania sio hoja bali madaraka, lakini kathibitisha kwamba hana uwezo wa kuoanisha mahusiano ya democrasia na uhuru wa maoni/mawazo na uwazi.
Mtu yeyote anayefanya mambo kwa siri katika jina la democrasia ama ni mtu asiyeelewa maana pana ya democrasia au la anaelewa lakini ameamua kupindisha ufahamu wake ili kutimiza malengo yake binafsi.
Mtu wa namna hiyo hastahili kuendelea kutambulika kwenye jamii kama mtu aliyebobea kwenye tasnia ya sayansi ya Siasa, ni ni wazi, narudia tena, kama hakusukumwa na maslahi binafsi, basi hana uwezo wa kufundisha vijana wetu sayansi ya siasa ambayo katika dunia ya sasa imejikita kwenye democratic politics.
Hiyo ni kwa ufupi tu, au la pitia nyuzi za wadau humu ndani uone anavyochanwa. He has disgraced himself.
Wewe Sangara ndio usiojua maana ya demokrasia.
Chadema haitasonga mbele kama kitakuwa chama cha Mbowe na wale wanaokubaliana naye tu kwa kuogopa kufukuzwa. Maoni tofauti ndio yatakayoboresha chama na sio ubabe na udikiteta.
- Kupigania madaraka ni sehemu kuu ya demokrasia yenyewe sawa sawa na uwezo wa kuchagua umtakaye. Mbowe hataki kuwe na ushindani maana anataka aendelee kutawala bila kupingwa licha ya uwezo wake na elimu yake ndogo.
- Kufanya mikakati ya kuteuana/kuchaguliwa kisiri siri sio kosa, hii inamaanisha tu kuwa wahusika hawataki kila mtu ajue wanachokifanya mpaka hapo wakati muafaka utakapowadia. Demokrasia inaruhusu watu/vikundi mbali mbali kuwa na mipango yao binafsi ilimradi tu hawavunji sheria. Kujadili mabadiliko ya uongozi kihalali ndani ya chama ni siasa na sio kosa la uhaini.
- Dr. Kitila hahitaji uhakiki wa mtu asiye na elimu ya kiwango chake (Ph.D) ili kuamuliwa ubora wa elimu yake. Ni wazi kuwa, Dr. Kitila, yuko juu sana kielimu ukilinganisha na elimu pungufu ya sekondari ya Mbowe ambayo pia hakufaulu.
Waraka ule umetaja mapungufu ya viongozi na uongozi wa CHADEMA, DR Kitila alikuwa anaingia kwenye vikao vya juu kabisa vya CHADEMA hakuna records zinazoonyesha kwamba aliwahi kutaja mapungufu hayo katika vikao husika, sio muwazi au ni Muoga au hajiamini. Hii inamaanisha kwamba ama alishindwa kutumia fursa ya chama chake kujitambulisha kama cha kidemocrasia kuchukua hatua za kidemocrasia katika kuweka wazi mapungufu hayo (Sio Muwazi)
Au, la alikosa ujasiri wa kutoa hoja hizo (Muoga), au la CHADEMA sio chama cha kidemocrasia kama kinavyodai, hivyo KITILA angepaswa kujitoa siku nyingi sababu yeye anajiita ni Muumini wa Democrasia, kung'ang'ania kwenye chama ambacho unasema sio cha kidemocrasia wakati wewe ni muumini wa democrasia nayo inamaana zake mbaya, ama haelewi democrasia ni nini au ana maslahi binafsi, analipwa kuwa apo ili kukivuruga chama.
SIRI, Kapitie waraka uone walivyokuwa wanapanga kutanua pyramid ya usaliti wao mikoani, yaani waende mikoani na hoja zilizo kwenye waraka, za malalamiko mwanzo mwisho, nia ilikuwa ni kuvunja morali ya wanachama mikoni na au la kuvunja chama.
Elimu yake, ni questionable.likely ni mkaririji fulani hivi.
Kutowa 'muwazi' au kuwa 'muoga' havina uhusiano wowote na elimu ya Dr. Mkumbo Kitila, B.A, M.A, Ph.D. Yeye ni msomi na anatambulika hivyo, utake au usitake. Aliye kubwa jinga ni Mbowe aliyeishia sekondari tu. Kama wewe umeuona huo waraka basi ubandike tuusome na usiendelee kuunukuu bila kuthibitisha. Zaidi ya hapo, ni tokea lini 'uwazi' na 'uoga' vikawa ni vigezo vya kuwafukuzisha viongozi wa siku nyingi chamani?