Proafrikana
New Member
- Apr 4, 2011
- 4
- 2
CHADEMA Kimejipambanua kwa vitendo kama Chama cha Watu na kinachojali Watanzania. Kwa muongo mmoja tumeshuhudia kuzaliwa na kukuwa kwa demokrasia ya vyama vingi ikiwa ni pamoja na CHADEMA. Muuendelezo huu umekuja na mapinduzi katika siasa za Tanzania na Mategemeo ya wanasiasa wetu. Waasisi wetu walikuwa watumishi wetu (servants of the people) na maslai yao yote yalikuwa kutumikia umma.. Sasa tunaona viongozi ambao wamekuwa mabwana (masters) wakiweka mbele vipaumbele vyao binafsi. Tumeshuhudia tuhuma za ufisadi na usaliti ndani ya vyama vyenye mamilioni ya wafuasi. Hawa ni wafuasi ambao wamejenga na wameweka matumaini yao katika vyama (vikundi hivi) na hawa ndiyo wenye Vyama vyao. Tumeshuhudia msemo wa vyama vya msimu labda kwa sababu msimu wa kulima watu hutafuta umaarufu halafu huvuna kwa kuuza mwisho wa msimu na huu ndio mwisho wa vyama vingi (vioongozi kuuza) Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 tulishuhudia Mh. ZZK akiwaambia wananchi wa Kigoma Kaskazini kuwa atagombea ubunge Kwa tikiti nyingine yoyote na alisikika akizungumzia majimbo kadhaa likiwepo moja la mkoa wa Mwanza. Amesahau kuwa Waha ndio waliombeba hadi akaonekana na sasa amekuwa Dume la shoka linaloweza kugombea jimbo lolote. Huu ni udhaifu mkubwa na usaliti kwa wananchi wa Kigoma Kaskazini. ZZK na Dr Mkumbo mmekuwa mfano wa vijana na wasomi ambao mmepata umaarufu wa kuonyesha nafasi ya kada hizi katika siasa. Umaarufu wote mliopata ni kwa kuwa katika nafasi hizi na jamii kuwapa heshima hiyo. Tunayoyasikia kutoka CHADEMA ni mwendelezo ule ule wa wa 2010 prematurity (kukosa ukomavu). Kwa umaarufu huu kibindoni tupo tayari kwa uenyekiti wa chama hata Uraisi Wa Tanzania, Je mko tayari pia kusema ZZK akikosa anachotaka basi tukose wote? Mko tayari kuvunja matumaini ya Watanzania kwa ajili ya personal intrest? personal intrest ni pamoja na ego siyo pesa. No mata how popular we may become or how powerful we may become, in this game we are not masters but servant of the people! Ask yourself first, what is it that you seek peoples glory or your own?