Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Waraka wa Bernard Membe kwa Askofu Mwamakula: Sitishiki, sitakaa kimya na kamwe sitaabudu mtu wala miungu wengine

Baba Magu yuko powa...
Msukuma hatishiwi na taarabu [emoji3][emoji3]
Waraka huu lazima umtoe povu yule mshamba na limbukeni. Lazima atafyatuka tu.

Utangulizi wa kachero mbobezi nimeupenda sana pia, ameanza kwa maneno 2 tu "NIGUSE NINUKE".

Nami namuonya limbukeni, asithubutu kumgusa kachero mbobezi.

Patamu hapo
 
Ndio tunataka watu wenye misimamo ya aina hii tuwape uongozi siyo Wapiga magoti, kazi na bata Membe twende kazi, mtu tumchague halafu anajimwambafy.
 
C&P......ujumbe alioujibu bernard membe ni huu hapa.

UJUMBE MAHSUSI KWA MHESHIMIWA BERNARD MEMBE.
Mheshimiwa Bernard Membe!
Pokea salaam za upendo kutoka kwangu mimi niliye mdogo sana miongoni mwa Maaskofu wa Kanisa la Mungu hapa duniani nisimamaye katika zamu yangu sasa! Nimekuwa nikifuatilia kwa makini na kusikia mengi juu yako katika siku za hivi karibuni. Ninatambua kuwa wewe ni mwanasiasa na siasa ni uwanja wa hoja.
Hata hivyo, kwa mazingira yalivyo tumeshuhudia kauli nyingi kukuzunguka wewe ambazo wakati mwingine zinatia hofu na mashaka. Kauli zinazoashiria kuwa siasa za Tanzania zimeanza kuonyesha dalili za watu kuanza kukosa kuvumiliana hasa pale watu wengine wanapoonyesha muono tofauti wa mambo.
Ninapenda nikuhakikishie kuwa pamoja na ukimya wao, Maaskofu walio wengi katika Nchi hii wanafuatilia kwa karibu sana mambo yanayohusu nchi hii ambayo Mungu amewaweka kuwa watumishi na mawakili wa siri zake. Pengine utatiwa moyo kusikia kuwa mimi pamoja na Maaskofu, Wachungaji, na watu wengine wengi usiowajua tunakuombea na kulitaja jina lako mbele za Mungu wetu.
Tunapenda ifahamike kuwa kukuombea kwetu hakutufanyi sisi kuwa lazima tukubaliane na muono wako wa mambo kuhusiana na siasa za Nchi hii, la hasha! Bali tunakuombea kutokana na ukweli kuwa kwa mazingira yaliyopo sasa baadhi yetu tunahisi kuwa unaweza kujikuta unaishi katika maisha ya hofu na wasiwasi mkubwa.
Tunamuomba Mungu ili akupe utulivu moyoni na pia akupe ulinzi dhidi ya watu ambao wanaweza kutaka kukudhuru kutokana na wao kutokupenda misimamo na mitazamo yako. Kwa kuwa na washindani wako na wao pia watausoma ujumbe huu, tunawasihi sana wasije wakaingia katika mtego wa kugusa uhai wako. Lakini pia, na wewe uepuke kuingia katika mtego wa kutaka kuwadhuru washindani wako. Mungu wetu atahusika na mtu ye yote anayejipanga kumwaga damu ya mtu mwingine iwe yeye mwenyewe au kuwatumia watu wengine.
Tunapenda wanasiasa wote wafahamu kuwa Mungu anapotoa kibali kwa mtu, kibari hicho hakiwezi kuondolewa na mtu au mamlaka ye yote ya kidunia. Kupambana na mtu aliyepata kibali kwa Mungu ni sawa na kupambana na Mungu mwenyewe. Tunapenda ifahamike kuwa kama wapo watu ambao Mungu amewapa kibali, wewe ukipambana nao utakuwa unajisumbua bure. Lakini pia, kama wewe utakuwa umepata kibali kutoka kwa Mungu, basi wale watakaoinuka kupambana na wewe na wao watakuwa wanafukuza upepo!
Tunakemea mambo yote ya kutishana na kunyamazishana na hata kutaka kupotezana miongoni mwa wanasiasa iwe ni katika Vyama vya Upinzani au ndani ya Chama Tawala. Kiongozi ye yote atakayeasisi au kushiriki katika vikao au mikakati ya kutaka kumuua mtu mwingine kwa sababu za kisiasa na mambo mengine nje ya mfumo na mchakato wa ki-Mahakama atakuwa anajitoa mwenyewe katika kibari cha Mungu kwa kuwa damu ya mtu haiwezi kumwagika bure pasipo kupiga kelele!
Ninaomba ukipata nafasi uweze kutafakari kwa kina Zaburi 35.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Kadri unavyomzingua paka ndivyo anavyozidi kunyanyua mkia huyu kiumbe anadhani kwa kuwatia hofu,kuwatesa,kuwaua, kuwabambia kesi, na kuminya kila aina ya uhuru watu ndio watanyamaza
 
Yeye anaongea tu! Awami ya tano ni vitendo tu. Sasa nani kiboko?

JMK amenukuu maneno ya Nyerere,

watawala kuwa na unyenyekevu na kufuata Katiba, sheria, taratibu na kanuni.

BKM kanukuu ya Mwamakula.

Hayo yote KIUHALISIA
yanausema utawala wa awamu ya TANO.

AWAMU HII, IKIRI, ITUBU NA KUANZA UPYA.

Watanzania hawana makuu, watasamehe.

mfano:- eti,
Nikitoka sgr, rufiji, flyover hazitajengwa.

ndege bombardier hazitanunuliwa.

Mbona awamu zilizopita hawakuyafanya?


KAMWAMBIE MUMEO, DIWANI WAKO NA MBUNGE WAKO.

EE, MUNGU SHUSHA ROHO YA TOBA NA WOGA HAPA TANZANIA.
 
Back
Top Bottom