Waraka wa Elimu kuhusu Adhabu ya Viboko kwa Shule za Tanzania Bara

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, washika dau pamoja na wananchi wote kuwa mnamo mwaka 2002, Serikali ya JMT kupitia Wizara ya Elimu ilitoa Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko na kuweka utaratibu mahususi wa utolewaji wa adhabu ya viboko. Adhabu hiyo inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa ya jinai yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima. Waraka huu pia unaongeza kuwa adhabu ya viboko itakayotolewa sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Nani mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwanafunzi kwa viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko umeweka bayana kuwa ni Mwalimu Mkuu wa shule husika ama mwalimu mwingine atakayeteuliwa na mwalimu mkuu kwa maandishi, kila mara kosa linalostahili adhabu hii linapotendeka. Aidha, waraka huu unaonya kuwa mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike.

Waraka umeweka wazi kuwa kila mara adhabu ya viboko inapotolewa sharti iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, la kujaza taarifa zihusuzo adhabu husika, hii ikiwa ni pamoja na jina la mwanafunzi aliyepewa adhabu, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo. Kwa kuwa waraka unamtambua Mwalimu Mkuu kama mtu mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi husika basi unamtaka pia atie saini yake katika kitabu hicho maalum kila adhabu ya viboko inapotolewa.

Waraka unasemaje pale mwanafunzi / mzazi anapokataa adhabu ya viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko unasema mwanafunzi anapokataa adhabu ya viboko sharti asimamishwe shule ili kupisha hatua zingine za kinidhamu juu ya kosa lake.

Mwisho kabisa waraka huu unawaonya waalimu kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atakiuka utaratibu ulioidhinisha na waraka huu. Kwamba kupitia Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko ni marufuku kwa mwalimu yeyote kuonekana na fimbo mkononi kwa lengo la kumuadhibu mwanafunzi.

Wizara ya Elimu Tanzania
 
Wizara yangu ya Elimu, futa hii corporal punishment, huu ni ukatili kwa watoto wetu na unatuletea kizazi chenye chuki na hasira, kulikua na uzi humu juzi kati wa kuwakunbuka waalimu, wachangiaji karibu wote wamechangia kuhusu ukatili wa viboko kwa wanafunzi, shame!!,waalimu wakati nchi Ina heshima na adabu, ilikuwa huwezi kuwa mwalimu kama huna ile EDUCATION, zaidi ya taaluma yako, Leo kutokana na viajira kuwa uchwara, graduate wa BSc naye eti anakwenda kuwa mwalimu!,
 
Waraka unasemaje kuhusu.

Idadi ya viboko ndani ya muda husika ipi ?

Viboko vipigwe wapi, mkononi au shingoni ?

Wanafunzi wanajulishwa na nani kuhusu kuzitambua adhabu stahiki ?

Viboko viwe vya fimbo za aina gani na za uzito upi ?

Mwanafunzi akipigwa kinyume na waraka achukue hatua gani ?

(Naomba majibu haya kwanza ili niendelee kuuliza mengine)
 
Mkuu hapa ni kufutilia mbali ukatili huu, adhabu ya viboko ipigwe marufuku nchini, adhabu mbadala zipo nyingi tu, adhabu za kumjenga mtoto ili aje kuwa raia mwema,ona humu kuna members wana ukatili wa hali ya juu na imesababishwa kulelewa bila upendo, baba akirudi watoto hawafurahii, wote wanakimbilia chini ya uvungu wa vitanda na ukimya unatawala!!,vyote hivi ni tabia fake, pretending ,mfanye mtoto wako akuone mzazi kama best friend
 
Kaka sio Kwa Tanzania hii hata vikifutwa watachapwa tu!
Walimu wa bongo tuna shida Mahala

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Sawa mkuu shida ipo wapi?,mie pia ni mwalimu ila kwa Muda mfupi niliofundisha hii adhabu sikuipenda kabisa na hata wale niliotumia nipo tayari to apologize to them, mwalimu aliyesoma ile Education (methodology),kutumia adhabu hii inakupa ukakasi sana, kipindi nipo chuo principal alianzisha hii copral punishment kwa waalimu watarajiwa, ila alikumbana na push 🔙 iliyomfanya arudi kwao in a body bag, hii inaonyesha waalimu watarajiwa hawa waliiona hii adhabu ni ushenzi wa hali ya juu, ninahakika intakes ile sidhani walitumia adhabu hii ya viboko, ni ukatili sana kwa wanafunzi
 
Tanzania bado tuko nyuma sana kimaendeleo. Huwezi amini mpaka sasa watoto wanalazimishwa kwenda shule. Huku vijijini kuna msako wa nyumba kwa nyumba kutafuta waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, wengi hawajaripoti
 
Nawaza tu siku nikija kuwa Rais walimu washenzi Kama wale wa kyerwa watapumulia wapi. Nawaza tu
Mpaka hapo umeshaharibu 😂😂😂 malengo adimu kama aya hayaongelewi hata kwa ndugu mkuu
 
Kuvunjwa mikono, kuachwa na makovu mwilini pamoja na athari hasi za kiwango kikubwa zaidi kwa maana ya vifo ni matukio mbalimbali yaliyotendwa na yanayoendelea kutendwa dhidi ya wanafunzi mashuleni huku sababu kubwa ikihusisha adhabu ya viboko. Jambo la kusikitisha zaidi ni kuwa, utolewaji wa adhabu hizo haufuati taratibu, kanuni pamoja na miongozo husika iliyowekwa.

Tunapenda kuwakumbusha wazazi, wanafunzi, walimu, washika dau pamoja na wananchi wote kuwa mnamo mwaka 2002, Serikali ya JMT kupitia Wizara ya Elimu ilitoa Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko na kuweka utaratibu mahususi wa utolewaji wa adhabu ya viboko. Adhabu hiyo inaweza kutolewa endapo kutatokea utovu wa nidhamu uliokithiri ama kwa makosa ya jinai yaliyotendeka ndani ama nje ya shule yenye muelekeo wa kuishushia shule heshima. Waraka huu pia unaongeza kuwa adhabu ya viboko itakayotolewa sharti izingatie ukubwa wa kosa, umri, jinsi na afya ya mtoto na isizidi viboko vinne kwa wakati mmoja.

Nani mwenye mamlaka ya kumuadhibu mwanafunzi kwa viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko umeweka bayana kuwa ni Mwalimu Mkuu wa shule husika ama mwalimu mwingine atakayeteuliwa na mwalimu mkuu kwa maandishi, kila mara kosa linalostahili adhabu hii linapotendeka. Aidha, waraka huu unaonya kuwa mwanafunzi wa kike anapaswa kupewa adhabu ya viboko na mwalimu wa kike tu isipokuwa isipokuwa kama shule haina mwalimu wa kike.

Waraka umeweka wazi kuwa kila mara adhabu ya viboko inapotolewa sharti iorodheshwe katika kitabu kilichotengwa kwa kusudi hili, la kujaza taarifa zihusuzo adhabu husika, hii ikiwa ni pamoja na jina la mwanafunzi aliyepewa adhabu, kosa alilotenda, idadi ya viboko na jina la mwalimu aliyetoa adhabu hiyo. Kwa kuwa waraka unamtambua Mwalimu Mkuu kama mtu mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi husika basi unamtaka pia atie saini yake katika kitabu hicho maalum kila adhabu ya viboko inapotolewa.

Waraka unasemaje pale mwanafunzi / mzazi anapokataa adhabu ya viboko? Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko unasema mwanafunzi anapokataa adhabu ya viboko sharti asimamishwe shule ili kupisha hatua zingine za kinidhamu juu ya kosa lake.

Mwisho kabisa waraka huu unawaonya waalimu kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambaye atakiuka utaratibu ulioidhinisha na waraka huu. Kwamba kupitia Waraka wa Elimu (Na.24) Kuhusu Adhabu ya Viboko ni marufuku kwa mwalimu yeyote kuonekana na fimbo mkononi kwa lengo la kumuadhibu mwanafunzi.

Wizara ya Elimu Tanzania
Ukimpiga mwanangu nakuvizia nakuua, final! haya manyaraka hayasaidii ni mzazi kukabiliana na wafidhuli hawa. Ukimpiga mwanangu nakupiga au nakuua usiku na sitafahamika!
 
Sasa mbona mnaujadili warska kwa maneno matupu na hakuna hata mmoja ameuleta softcppy yake.
 
HAWa watoto wanaokazana darasani mchana kweupe au kuna wengine. Haumjui kilichopo hizi shule za leo hasa sekondari mtu kajikosesha asiende sekondari laki anajikuta kafaulishwa kinguvu
 
Back
Top Bottom