Responded Waraka wa Katibu Mkuu kuhusu MUDA WA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA UHAMISHO KUPITIA MODULI YA e-UHAMISHO

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
A

Anonymous

Guest
Huu ni Waraka kutoka kwa katibu mkuu.

Hii iwaendee Supervisors Maafisa utumishi HR na Wakurugenzi malalamiko yetu watumishi ya kucheleweshwa kwa maombi ya uhamisho sasa yamemfikia mh.

KATIBU MKUU na amejibu kwa ufasaha kabisa!

======

MUDA WA KUSHUGHULIKIA MAOMBI YA UHAMISHO KUPITIA MODULI YA e-UHAMISHO NGAZI YA MWAJIRI

Waajiri wote katika Utumishi wa Umma mnafahamishwa kwamba Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maboresho kwenye Moduli ya Uhamisho Kielektroniki (e-Transfer Module) iliyopo kwenye Mfumo wa e-Watumishi.

Kupitia Maboresho hayo, maombi ya uhamisho kupitia Moduli ya e-Uhamisho yamewekewa Muda Maalumu wa kukaa na kushughulikiwa na Viongozi mbalimbali ngazi ya Mwajiri.

Baada ya muda tajwa kufika, ombi husika litaendelea hatua inayofuata kwa dhana (Assumption) kwamba ombi hilo limeridhiwa katika ngazi husika. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha maombi ya uhamisho ya Watumishi yanashughulikiwa na kuhitimishwa kwa wakati.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni C.17 (2) ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za Mwaka 2009, Muda Maalum kwa Viongozi ngazi ya Mwajiri kutoa maoni yao kwenye Maombi ya Uhamisho kupitia Module ya e-Uhamisho kuanzia tarehe 17 Mei, 2026 ni kama ifuatavyo:-

I. Msimamizi wa Kazi (Supervisor), siku tatu (3) kuanzia siku ya kupokelewa kwa ombi hilo;

II. Mkuu wa Kitengo/Idara anayofanyia kazi Mtumishi, siku nne (4) kuanzia siku ya kupokea ombi kutoka kwa Msimamizi wa Kazi;

III. Mkuu wa Kitengo/ldara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, siku nne (4) kuanzia tarehe ya kupokea ombi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo/ldara; na

IV. Mwajiri (Accounting Officer), siku kumi (10) kuanzia siku ombi ilipomfikia kutoka kwa Mkuu wa Kitengo/ldara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu.

Ninawashukuru kwa ushirikiano wenu.
SACP. Ibrahim B. Mahumi
21/05/2026 Kny: KATIBU MKUU (UTUMISHI)

=======

Kwa Sasa maombi yakikaa kwa mhusika zaidi ya sku zilizoanishwa na Mh. KATIBU MKUU huyo mhusika ajue anaenda kinyume na miongozo ya utumishi wa umma kwasasa mambo ni mazuri ngoja tuone utekelezaji wake kwa wale walio omba tutapata feedback kupitia kwenye group letu

Share ujumbe huu kwa watumishi wote TZ waweze kupata habari hii njema✅
 
naona ni habari njema kwa wale wote wenye vilio vya kucheleweshewa uhamisho wao
 
Mwezi wa nne(4) ombi langu bado lipo kwa karibu mkuu yaani PO- PSMGG nasubiri approved jamaa yangu miezi Tisa anasubiri
 
Kwenu waajiriwa..
Mke wangu katoka masomoni, hajapandishwa cheo (sasa ni mwaka umepita) alikuwa na diploma ya utabibu, akaenda kuchukua degree, kisa anaambiwa hakujaza PEPMIS(kama sijakosea)
Je akifanikiwa kuhama hali ya kuwa hajapandishwa cheo na kurekebishiwa mshahara haitampa tabu huko mbele ya safari?
Maana hiki ndio kitu anaogopa kuanza mchakato wa uhamisho.
 
Transfer request au ulianza na vacancy request
Kaka nimefuata taratibu zote nilianza vacancy (hii ni kwajili ya kuomba nafasi kule uendako mfano taasisi,wizarara nk) kwa hiyo nikajibiwa nkaendelea hatua nyingine ,ambapo ikanipeleka kwenye Transfer request( hii ni baadaya ya kukubaliwa nafasi kwenye vacancy request unaendele na hatua nyingine amabayo inapitq kwa mkuu wa idara yako then unaenda kwa mkurugenzi aki approve Moja kwa Moja inaenda UTUMISHI HQ) kwa hiyo mtu wa mwisho ku approve hapa ni katibu mkuu.
NB hatua zote nimetumia mfumo
 
KWa namna hiyo itakuwa vyema,japo hajasema maombi kwa katibu mkuu yata kaa kwa muda gani.
 
Kaka nimefuata taratibu zote nilianza vacancy (hii ni kwajili ya kuomba nafasi kule uendako mfano taasisi,wizarara nk) kwa hiyo nikajibiwa nkaendelea hatua nyingine ,ambapo ikanipeleka kwenye Transfer request( hii ni baadaya ya kukubaliwa nafasi kwenye vacancy request unaendele na hatua nyingine amabayo inapitq kwa mkuu wa idara yako then unaenda kwa mkurugenzi aki approve Moja kwa Moja inaenda UTUMISHI HQ) kwa hiyo mtu wa mwisho ku approve hapa ni katibu mkuu.
NB hatua zote nimetumia mfumo
Mkuu sorry!!!naomba nipate ufafanuzi kidogo ,hv upande wa attachment kule kwenye vacancy request je unaattach CV tu au ni pamoja na barua ya maombi ya kuomba kuhamia uko unakotaka kwenda??
 
Mkuu kulingana na huo waraka, kama mtu kanzisha ombi la uhamisho kupitia dirisha la Vacancy transfer na ombi likifika kwa Destination institution linachukuwa siku 10 au 21. Maana Kuna maombi yamefika siku 10 Bado hayajaenda mbele
Mkuu sorry!!!naomba nipate ufafanuzi kidogo ,hv upande wa attachment kule kwenye vacancy request je unaattach CV tu au ni pamoja na barua ya maombi ya kuomba kuhamia uko unakotaka kwenda??
 
Ni jambo jema sasa shida itaanzia kule HQ maana wao kupitisha ombi la mtumishi wanaona n kama dhambi hv
 
Jamani nyie suala la vacancy not budgeted mnafanyagaje,au kuna namna nyingine naombeni tafadhali,,,maana yake nakoomba kote ndio navyo jibiwa,,,
 
Back
Top Bottom