Waraka wa Maaskofu unabagua mambo

Waraka wa Maaskofu unabagua mambo

Nyerere alipewa waraka kwaajili gani?
Nilimaanisha hata wakati wa Mwalimu Nyerere TEC walikuwa wakitoa nyaraka za kichungaji. Nyaraka haziandikwi kumlenga kiongozi wa kitaifa, "addressees" wa nyaraka ni wanakanisa na mahitaji ya kanisa na ndiyo maana husomwa kanisani kwa waumini.
 
Unachanganya mambo. Labda kwa sasa ungejikita kwa hicho TEC walichokisema na wewe ulete utetezi wako. Hapo ndipo ungeeleweka. By the way, unadhani TEC haina wanasheria?
wanasheria uchwara? Kama mahakama imetoa ruling kwa mwanasheria makini anajua maana yake ni nini? ukiona mwanasheria anapingana na maamuzi ya mahakama mitaani ujue hapo kuna tatizo tayari. Kama hajaridhika akate rufaa kwenye mahakama za mbele badala ya kutafuta sympathy ya waumini makanisani na mitaani. Atavunjwa kichwa bure na asipate wa kumtetea.
 
Tuna bahati kumpata huyu Rais kimiujiza, amenyooka kama rula, hana magenge, ana hofu ya Mungu, hana ndugu maskini sana, hana njaa, na anafahamu kuwa wanawake wote wanapimwa kupitia yeye.
😂😂😂😂😂🛩️ 📌🔨
 
Unajichanganya sana kwenye kujenga hoja zako.
Mwaka 1992 nani alikuwa raisi? Alikuwa wa kutokea upande gani kiimani?
Kama hao TEC lengo la nyaraka zao kupinga viongozi wa upande 'huo' mbona hawakumpinga Mwinyi 1992?
Nyie watu nila kukicha ni malalamiko tu na kutopenda kukosolewa munapo haribu mambo serikalini au kwenye jamii.
Labda kama hukuwepo wakati huo wa 1992. Aliyelazimisha kuwepo kwa vyama vingi alikuwa Mwl Nyerere ingawa hakuwa Rais.
 
Labda kama hukuwepo wakati huo wa 1992. Aliyelazimisha kuwepo kwa vyama vingi alikuwa Mwl Nyerere ingawa hakuwa Rais.
Nilikuwepo, nani alikuwa na mamlaka makubwa?
Mbona Nyerere alipinga kubinafsisha bank ya NBC na hukusikilizwa?
Mwinyi angefanya alichoona sahihi bila kujali Nyerere anataka nini kama vile Mkapa alivyofanya kuhusu NBC.
 
jana Gerson Msigwa kushatangaza Serikali inaendelea na Mkataba wa ukodishaji wa Bandari

kuna watu hawaamini maana walidhan utulivu wa Serikali hii ni ishara ya kuwaogopa

inanikumbusha ile mijadala na nyaraka za mahafidhina ya Kikomunist machawa ya Nyerere yaliyokuwa University of Dar es salaam miaka ya mwisho ya 1980s yaliyopinga kwa nguvu zote kuupiga chini Ujamaa, kile kimya cha Ally Hassan Mwinyi yakatafsiri anawaogopa na watambabaisha, hata Nyerere mwenyewe alikuja kujua kupitia gazeti la Mfanyakazi na uhuru aliishia kupiga makelele na kutukana kupitia kitabu chake maarufu cha Hatima yetu na Siasa za Tanzania
Watajua hawajui na waraka wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanasheria uchwara? Kama mahakama imetoa ruling kwa mwanasheria makini anajua maana yake ni nini? ukiona mwanasheria anapingana na maamuzi ya mahakama mitaani ujue hapo kuna tatizo tayari. Kama hajaridhika akate rufaa kwenye mahakama za mbele badala ya kutafuta sympathy ya waumini makanisani na mitaani. Atavunjwa kichwa bure na asipate wa kumtetea.
Kuna sheria inayosema ruling ya mahakama ikishatoka mtu haruhusiwi kutoa maoni au kueleza mawazo yake? Kwa nini huwa kuna rufaa kama ruling maana yake ni watu wasiwe na maoni na mawazo juu ya jambo fulani linalowahusu? Watu wako huru kutoa maoni na kueleza mawazo yao juu ya jambo lolote linalohusu maisha yao na hakuna sheria inayosema hukumu ya mahakama itawafunga watu kutoa maoni yao. Kama ipo ilete humu tuione. Kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2005) "kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza mawazo yake". Ngoja nisubiri hiyo sheria au case law inayozuia watu kutoa maoni na kueleza mawazo yao kwa jambo lolote linalowahusu.
 
Wakati wa Magufuli hukuona waraka wowote toka TEC? Umejaa huku JF.

Tatizo lenu mnaendeshwa na mahaba ya dini yenu, hamtaki mama yenu aguswe hata akikosea wazi, hilo haliwezekani, sio kwa Tanganyika hii ya leo.

Kama hamtaki aguswe, muondoeni ikulu muende nae Makunduchi halafu muone kama yupo atakayehangaika nae.
Wakati wa Mkapa na Magufuli TEC walikuwa wanapiga kwa LESO, ... wanapoingia walengwa hakuna silaha inayoachwa!
BAJAMENI HEBU LOGENI USIKU, ... MCHANA MTAYABHURA! 😅
 
Watajua hawajui na waraka wao

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hiyo inazuia watu kutoa maoni na kueleza mawazo yao? Mbona mnashindwa kutofautisha vitu. Watu wanatoa maoni, serikali inasikiliza na inaweza kuzingatia maoni ya wananchi au kuyapuuza. Lakini watu wataendelea kutoa maoni na kueleza mawazo yao. Hivyo, ni useless kudhani serikali ikiendelea na mpango wake wa uwekezaji wa bandari then imewafunga watu mdomo kuwa na maoni au mawazo tofauti kuhusu uwekezaji bandarini. Kuna mambo Mwalimu Nyerere alishauri yafanyike baada kuwa amestaafu - kuna baadhi ya yale aliyoshauri yalifanyiwa kazi na kuna aliyoshauri na hayakufanyiwa kazi. Na hiyo haina maana kwamba kama alichoshauri hakikufanyiwa kazi basi akome kutoa maoni au ushauri. Kutoa maoni au ushauri si lazima ukubaliwe. Kwa hiyo, muwe mnatofautisha mambo kuliko kuweka tu maneno pamoja na kudhani yana'make' sense. Hapana.
 
Nilikuwepo, nani alikuwa na mamlaka makubwa?
Mbona Nyerere alipinga kubinafsisha bank ya NBC na hukusikilizwa?
Mwingi angefanya alichoona sahihi bila kujali Nyerere anataka nini kama vile Mkapa alivyofanya kuhusu NBC.
Nyerere alikuwa bado mwenyekiti wa CCM
 
jana Gerson Msigwa kushatangaza Serikali inaendelea na Mkataba wa ukodishaji wa Bandari

kuna watu hawaamini maana walidhan utulivu wa Serikali hii ni ishara ya kuwaogopa

inanikumbusha ile mijadala na nyaraka za mahafidhina ya Kikomunist machawa ya Nyerere yaliyokuwa University of Dar es salaam miaka ya mwisho ya 1980s yaliyopinga kwa nguvu zote kuupiga chini Ujamaa, kile kimya cha Ally Hassan Mwinyi yakatafsiri anawaogopa na watambabaisha, hata Nyerere mwenyewe alikuja kujua kupitia gazeti la Mfanyakazi na uhuru aliishia kupiga makelele na kutukana kupitia kitabu chake maarufu cha Hatima yetu na Siasa za Tanzania
Saa ya UKOMBOZI ikifika Mungu huifanya mioyo ya Watawala kuwa migumu na anguko hufuata. Farao/Firauni aliwekewa kiburi ndani ya moyo wake na kukaidi kila alichoambiwa na Nabii Mussa, kilichofuata ni anguko. CCM kwa hili la bandari, shupazeni shingo zenu, saa ya UKOMBOZI imeletwa na DP World.
 
Kuna sheria inayosema ruling ya mahakama ikishatoka mtu haruhusiwi kutoa maoni au kueleza mawazo yake? Kwa nini huwa kuna rufaa kama ruling maana yake ni watu wasiwe na maoni na mawazo juu ya jambo fulani linalowahusu? Watu wako huru kutoa maoni na kueleza mawazo yao juu ya jambo lolote linalohusu maisha yao na hakuna sheria inayosema hukumu ya mahakama itawafunga watu kutoa maoni yao. Kama ipo ilete humu tuione. Kwa mujibu wa Ibara ya 18(a) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kama ilivyofanyiwa marekebisho hadi 2005) "kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kueleza mawazo yake". Ngoja nisubiri hiyo sheria au case law inayozuia watu kutoa maoni na kueleza mawazo yao kwa jambo lolote linalowahusu.
kila mtu ana uhuru wake binafsi, lakini sio uhuru wa kushawishi, kulaghai, kuchochea na kulazimisha wengine ili wakubaliane na mawazo yako , utashi wako, maslahi yako binafsi na kundi lako ili wakusaidie kupinga serikali.
 
Of course, unachofanya wewe ndicho hicho unachokisema. Unafanya kitu ambacho kwenye psychology kinaitwa "projection" - yaani weakness yako mwenyewe unai'project' kwa wengine ili ujione kama wewe huna shida. Unajisumbua bure. Waraka umeshatoka na umeshasomwa na watu wengi duniani, sasa sijui utafanya nini? Pole sana!
 
Saa ya UKOMBOZI ikifika Mungu huifanya mioyo ya Watawala kuwa migumu na anguko hufuata. Farao/Firauni aliwekewa kiburi ndani ya moyo wake na kukaidi kila alichoambiwa na Nabii Mussa, kilichofuata ni anguko. CCM kwa hili la bandari, shupazeni shingo zenu, saa ya UKOMBOZI imeletwa na DP World.
Iko siku kila kofi litapigwa na kila mtu siku ambayo bandari itakapokuwa inatema pesa nyingi kutokana na uwekezaji huu. Hii ni phobia tu of unknown origin na resistance of change. Kuna watu wanaogopa change/mabadiliko kwa sababu au bila sababu. Lakini simuoni mtu mwenye uwezo wa kuuza bandari hapa akafanikiwa.
 
Kama kuna vipiengele kwenye mkataba vina changamoto kwa maslahi ya taifa, virekebishwe, mambo yaendelee.

Ni bora maji ya kunywa kwa wote kuliko mvinyo kwa watu wachache.
 
Back
Top Bottom