Watanzania wenzangu, tuwe makini sana na watu kama akina Mtikila hasa kipindi kama hiki, ccm wana mbinu nyingi sana za kuhakikisha kuwa, mchakato wa kuipata katiba mpya unavunjika, mpaka hapa tulipofikia kuipata rasimu ya pili ya katiba, ccm wameshikwa pabaya, ndio maana tunaona wapeleka mambo ya kitoto kama vile kura wazi, na mambo hayo yamekuwa hayakubaliki ndani ya bunge la katiba na kuishia kugeukana wao kwa wao, kuna watu watakuja na hoja tamu sana ambazo zinakubalika kama alivyofanya Mtikila, tukadanganyika na kuwasapoti, kumbe lengo lao ni kuharibu mchakato, ili tusipate katiba mpya, hawa watu wanatumika na ccm, Mtikila na wajumbe wengine, wanapaswa kuungana na kupinga kwa nguvu zote, namna yoyote ya kutukwamisha tusipate tusipate katiba inayotakiwa, na siyo kuturudisha nyuma eti tuanze upya, huo ni uhuni, kama ni elimu ya uraia, CHADEMA walizunguka nchi nzima kutuelimisha, tukaelewa na kutoa maoni yetu, japo serikali ya ccm haikupenda.