Waraka wa Profesa Anna Tibaijuka kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Kagera. "Kagera Twafa"

Mkoa wa Kagera unapaswa kuwa moja ya mikoa tajiri sana kwani upo katika eneo nyeti (strategic position) kwa kupakana na Uganda na Rwanda. Kinachotakiwa ni kufungua mipaka na kufanya biashara bila vikwazo.

Kwa sasa mkoa umefungwa kwa kisingizio cha usalama na wakimbizi. Viongozi na hasa wana Kagera wanapaswa kupigania uhuru zaidi wa kufanya biashara kwa kuuza na kununua toka kwa majirani.
si rahisi wa watu wa kagera kubadilika.kwanza wanatakiwa kubadili mindset zao kibiashara.wengi wa wenyeji wa mkoa huu si waaminifu kibiashra.wao kila kitu ni ujanja ujanja.taasisi nyingi za fedha zilizopo kagera zinalalamika huwa wakiwezeshwa fedha za mikopo hawalipi na wengine huwa wanahama makazi kabisa pia bado wanatabia za kudhulumu wakipewa mchongo.wao kwa wao kwanza hawaaminiani hata kidogo.pia kwa asili wao si watu wa kujituma hawana traits za ujasiriamali wao kila kitu huenda shortcuts.hawapendi kuvuja jasho bali wanapenda biashara za magumashi hivyo kwao ni kazi kubwa kutoboa.kuna mambo mengi wanatakiwa wabadilike na nawashangaa wanapowalinganisha na wachaga wkt kuna mikoa kibao tu imewaacha mbali.kama mkoa ni wa 25 sasa unawalinganisha na mkoa gani kimaendeleo?mikoa inayofanya vzr ndo mikoa iliweza kutumia elimu zao ktk biashara na ujasiriamali.Prf analalamika anataka asaidiwe wakati yy ameshika nyadhifa nyingi lkn aliusahau mkoa wake.alikuwa busy kuhodhi ardhi ambayo nayo mpaka sasa wala haiendelezwi si angeitoa hiyo ardhi akawapa wazalishaji ili kipato cha mkoa kiongezeke?inabidi mkoa ujitathimini wenyewe unakoelekea sababu hata wageni wanashindwa kuwasaidia sababu ya unafiki na ubinafsi.
 
1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.

2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.

3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.

4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.

Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.

5. Sababu nyingine ni historical disruptions za

(a) Vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda, Murongo, lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.

(b) Pili, ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera. Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.

(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.

Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU (1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.

Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya, Mwanza, Moshi, Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
Umeandika as if wew ndo professor [emoji123]

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Waraka unaosemekana umeandikwa na Prof Msomi wa kihaya Anna Tibaijuka ukionesha Dunia jinsi mkoa wa Kagera unavyorudi nyumba kimaendeleo ni waraka ambao umebeba ujumbe ambao haukustaili kuandikwa na Anna Tibaijuka, au mtu kama Wilsoni Masilingi.

Watu hawa wekuwa viongozi wa wakubwa katika serikali za awamu tofauti, mathalani mtu kama Prof amekuwa mbunge wa huko huko mkoani kagera lakini unaambiwa hakuna Alichokifanya zaidi ya kusambaza maji pale Muleba.

Ukienda kwa ta Mwami Wilsoni Masilingi aliishia kuchonga ndevu na kupaka piko bungeni hakuna aliro lifanya ,leo hii wapo nje ya mfumo wanaanza kuropoka ovyo pasipo kuja na suluhisho.

Mali alizo Nazo Tibaijuka nusu na robo ya Mali zake ziko mikoa mingine kwa nininl hakuwekeza kwao? Ze same bushit to Masilingi na ndevu zake kama kamshungu shungu leo hii wako nje ya mfumo wanaona mkoa ukidorola wanaanza kelele.

Anna Tibaijuka akiwa mbunge alishindwa hata kuomba barabara ya lami leo hii barabara zinajengwa anaona wivu yeye aliishia kuongea lugha za ajabu ajabu bungeni mfano ile ya KUPANUA na nyingine atulie hata afanyeje Samia hawezi enda na kizee kama yeye apambane na Hali yake.
Sababu kama hizi ndizo zinazotusukuma wenyeji wa Ngara kutaka mkoa mpya wa Chato, huu wa sasa ni uendelezaji tu wa historia na ukoloni.

Mawazo mapya yanatusukuma kutaka mkoa mpya wa Chato, utakaokuwa mdogo na wenye kufikika kila mahali.
 
Anayepinga hoja za prof yuko kisiasa na ana upeo mdogo. Uchambuz wa mama tibaijuka ni wa kisayansi, huyu analeta porojo. Utafit hupingwa kwa utafiti! Cha muhim tujue tunatokaje tulipo.
 
Kumuongelea iddi amini miaka 45 iliyopita kuwa amewarudisha nyuma ni ujinga sana
Pale Kenya Kuna report inaitwa TJRC,truth justice and reconciliation commission,hiyo report imeeleza political and economic injustice and crime ambazo jamii zingine zilifanyiwa na serikali,madhara yake yapo mpaka leo,hiyo report serikali imeshindwa kuifanyia kazi,maana Kuna waliofsidika na dhuruma hizo.
Kusema imepita miaka 45 kwahiyo madhara ya vita ysmeisha kimiujiza?wakati miundo mbinu inaharibiwa kagera,mikoa mingine iliacha maendeleo mpaka vita iishe?
Pale Kenya Kuna makabila matatu yalifaidika na utawala,Kikuyu,kalenjin,Ruo,kamba,luhya,watu wa makabila haya waliofsidika na rasilimali za nchi,walipewa Elimu sana,tangu uhuru mwaka 1963,leo hii miaka 55+baadae uwekezaji uliofsnyika kwenye jamii hizi,umezipa ukwasi wa kutisha,na nguvu ya kiuchumi kubwa,wafanyabiashara wakubwa ni kutoka hizi jamii.
Wakati makabila mengine yamebaki fukara sana,muda sio ishu,bila juhudi za makusudi hata ipite miaka mingspi,kama mbegu ya madhara ilipandwa itsonekana tu
 
Magufuri alitaka kuifufua Kagera!lakini safari imekatika!,
Meli alizaka kujenga, na mazao ya kimkakati vingeweza kufufua uchumi wa Kagera!,
Bei ya sukari mpaka ikapangiwe Mwanza au Dar!
 
si rahisi wa watu wa kagera kubadilika.kwanza wanatakiwa kubadili mindset zao kibiashara.wengi wa wenyeji wa mkoa huu si waaminifu kibiashra.wao kila kitu ni ujanja ujanja.taasisi nyingi za fedha zilizopo kagera zinalalamika huwa wakiwezeshwa fedha za mikopo hawalipi na wengine huwa wanahama makazi kabisa pia bado wanatabia za kudhulumu wakipewa mchongo.wao kwa wao kwanza hawaaminiani hata kidogo.pia kwa asili wao si watu wa kujituma hawana traits za ujasiriamali wao kila kitu huenda shortcuts.hawapendi kuvuja jasho bali wanapenda biashara za magumashi hivyo kwao ni kazi kubwa kutoboa.kuna mambo mengi wanatakiwa wabadilike na nawashangaa wanapowalinganisha na wachaga wkt kuna mikoa kibao tu imewaacha mbali.kama mkoa ni wa 25 sasa unawalinganisha na mkoa gani kimaendeleo?mikoa inayofanya vzr ndo mikoa iliweza kutumia elimu zao ktk biashara na ujasiriamali.Prf analalamika anataka asaidiwe wakati yy ameshika nyadhifa nyingi lkn aliusahau mkoa wake.alikuwa busy kuhodhi ardhi ambayo nayo mpaka sasa wala haiendelezwi si angeitoa hiyo ardhi akawapa wazalishaji ili kipato cha mkoa kiongezeke?inabidi mkoa ujitathimini wenyewe unakoelekea sababu hata wageni wanashindwa kuwasaidia sababu ya unafiki na ubinafsi.
Hizi hisia za kichaga zitakuua bure, muhaya mali yake ni ya halali hana pesa na utajiri wa damu wa kuuwa watu na ndugu zenu, nyinyi mmewekeza kwenye biashara, sisi elimu na familia zote zenye wasomi uhayani zina maisha bora, sasa nyinyi mkifika bk mjini mnaanza maneno, kazi ya kujenga soko na barabara ni ya serikali, sisi wananchi tushachangia kodi, kama serikali haitajenga hiyo miundombinu sisi hatuna habari tutaendelea kufanya maendelea kwenye familia zetu, mkija mkakuta nyanya imepangwa chini nunueni, hamtaki rudini kwenu penye maendeleo.
 
Suala la yeye Prof. kuhodhi ardhi halihusiani na maendeleo ya wana Kagera kwa ujumla wake. Kitu cha msingi ulicho point out hapa ni desturi ya kutokujituma, ulaghai na utapeli, uvivu na unafiki walionao wana Kagera.

Aidha tusimlaumu kwa kutowaendeleza wananchi wenzake kwa kigezo cha nyadhifa alizowahi kushika bali tumuunge mkono katika harakati za kubadilisha mind set za wana Kagera.
 
Hizi hisia za kichaga zitakuua bure, muhaya mali yake ni ya halali hana pesa na utajiri wa damu wa kuuwa watu na ndugu zenu, nyinyi mmewekeza kwenye biashara, sisi elimu na familia zote zenye wasomi uhayani zina maisha bora, sasa nyinyi mkifika bk mjini mnaanza maneno, kazi ya kujenga soko na barabara ni ya serikali, sisi wananchi tushachangia kodi, kama serikali haitajenga hiyo miundombinu sisi hatuna habari tutaendelea kufanya maendelea kwenye familia zetu, mkija mkakuta nyanya imepangwa chini nunueni, hamtaki rudini kwenu penye maendeleo.
Futa mapovu yako hapa! Hakuna anayezungumzia Bukoba mjini, wala soko hapa tunajadili maendeleo ya mkoa wa Kagera!
 
Siwezi kufuta kwa zwazwa moja la kichaga linaloishi kwa mali za damu kwa kuuwaua watu na ndugu zake. Nyinyi ndiyo janja janja tu, mnaishi kwa kubebwa bebwa kama mlidhubutu kuiba BOT, nani asiyejua mali zenu za wizi na damu.
 
Pale Kenya Kuna report inaitwa TJRC,truth justice and reconciliation commission,hiyo report imeeleza political and economic injustice and crime ambazo jamii zingine zilifanyiwa na serikali,madhara yake yapo mpaka leo,hiyo report serikali imeshindwa kuifanyia kazi,maana Kuna waliofsidika na dhuruma hizo.
Kusema imepita miaka 45 kwahiyo madhara ya vita ysmeisha kimiujiza?wakati miundo mbinu inaharibiwa kagera,mikoa mingine iliacha maendeleo mpaka vita iishe?
Pale Kenya Kuna makabila matatu yalifaidika na utawala,Kikuyu,kalenjin,Ruo,kamba,luhya,watu wa makabila haya waliofsidika na rasilimali za nchi,walipewa Elimu sana,tangu uhuru mwaka 1963,leo hii miaka 55+baadae uwekezaji uliofsnyika kwenye jamii hizi,umezipa ukwasi wa kutisha,na nguvu ya kiuchumi kubwa,wafanyabiashara wakubwa ni kutoka hizi jamii.
Wakati makabila mengine yamebaki fukara sana,muda sio ishu,bila juhudi za makusudi hata ipite miaka mingspi,kama mbegu ya madhara ilipandwa itsonekana tu
Nakuelewa ndugu ila kwa hili idi amini tunamsingizia,mimi nimefika bukoba,kyaka,mtukura,misenyi,ngara,karagwe.sijaona madhara ya iddi amini,iddi amini alitia hasara taifa kwa kuua wanajeshi na kutumia bajeti kubwa kumfurusha ila wahaya na wanyambo walioathirika na vita moja kwa moja ni kidogo sana,mi nadhani zao ka kahawa kukosa bei nzuri,na mnyauko wa migomba,wahaya kutopenda fursa zingine zaidi ya kusoma,kutowekeza bukoba mjini,ubinafsi,ubaguzi na egoism ndio sumu ya maendeleo ya wana bukoba
 
1. Nimesoma andiko la Prof. Anna Tibaijuka juu ya hali tete Mkoa wa Kagera tunapojikuta tuko mwisho kwa vigezo vya kiuchumi hususan GDP.

2. Ningeomba atupe namba ya mkoa katika quality of life/happiness index kutokana na household survey. Ni kwa kutazama vyote viwili ndio tunaweza kusema kama tupoteze imani kabisa au tupendekeze mikakati ya kutupandisha chati katika kipindi cha miaka 5 hadi 10.

3. Huko nyuma nimeshandika sababu ambazo zinaelezea kuanguka kwa uchumi wa Mkoa wa West Lake/ Kagera katika miaka 60 kutoka wa 2 hadi wa 26; kama mtu ambaye ameona haya yote yakitokea.

4. Sababu ya kwanza ni demographic na nategemea Prof. aielezee hii point. Kupiga hatua katika elimu bila kukua kwa viwanda au estate agriculture kuweza kuwaajiri wasomi wake huko kumesabaisha brain drain ya watu wetu walio kwenye productive age kuajiriwa nje ya mkoa wetu na kwa hiyo kuchangia kuendeleza mikoa mingine ya Tanzania.

Tumeacha watoto na wazee ambao mchango wao katika uzalishaji ni haba wakibaki kulima mashamba ya migomba na mibuni iliyopandwa miaka 100 iliyopia. Wachache walio na uwezo wa kuzalisha wamezembea kuhamia mahala ambako wangejiongeza kiuzalishaji na kuendekeza land fragmentation; mojawapo ya sababu ikiwa kuishi kwa invisible earnings kutoka kwenye mishahara ya jamaa zao walioko nje ya mkoa.

5. Sababu nyingine ni historical disruptions za

(a) Vita ya Tanzania na Uganda au na Idi Amin. Wengi huiona kama athari katika miaka ya 1978 mpaka 1980;
wanasahau kwamba uhusiano na Uganda ulififia kwa miaka zaidi ya 10 kuanzia 1971. Mathalan uwekezaji wa Serikali/NAFCO katika shamba la Ngano Kibanda, Murongo, lililokuwa mechanised ukiwa na matrekta hadi combine harvestor, ulisitishwa kwa kuhofia Amin asipate target ya kupiga mabomu. Prof. atafiti agundue kwa nini Serikali haikuendelea nao baada ya vita.

(b) Pili, ni Vita ya Kiuchumi ya Sokoine ambapo tofauti na mikoa mingine, wafanyabiashara wote muhimu katika mkoa waliswekwa ndani, na malori zaidi ya 400 yalikamatwa na kuteketea Kaitaba Stadium. Prof. na wasomi wengine watupe kiwango cha economic disruption iliyotokana na vita hiyo na fidia ambayo haikutolewa. Sheria maalumu kutaifisha malori yasiyozidi miaka 5 ambayo ilihusu Kagera tu ilikuwa ya kibaguzi na fidia ilikuwa kiduchu,ambayo kutokana na inflation,hawakuweza kununua lori nyingine. Nilishangaa sifa alizopewa Nsa Kaisi miaka ya karibuni, bila watu kukumbuka ukatili(sadism) alioufanyia mkoa wa Kagera. Serikali na CCM walipaswa kutengeneza Marshall Plan ya kuwekeza katika mkoa kuurudisha kwenye maendeleo iliyokuwa nayo.

(c) Mathalan,mwaka 1967 serikali ilipotaifisha mabenki na Viwanda, kampuni ya West Lake Bus Service iliyokuwa na mabasi ya routes zote mkoani ilifilisiwa na wamiliki wa Kihindi na kukomba hela yote na kumwacha Mzee Daniel K Rwiza, mtu aliyedhamini watu kujenga nyumba za bati Karagwe, kubaki masikini. Shida zote za usafiri mkoani tangu hapo mpaka miaka ya 1990s zinaanzia hapo,na ziliathiri mkoa sana.

Nadhani nimempa Prof. Anna na wapenda maendeleo wa Mkoa wa Kagera nafasi ya kuanzia. Sijataja athari za kuhujumu BCU,kuleta Mamlaka ya Kahawa na kuanzisha BCU (1990) Ltd na KDCU bila mali za Union zote kupatikana nyingine zikichukuliwa na RTC na CCM kuchukua kiwanja cha Union ambako kumejengwa makao makuu ya CCM ambayo ni gofu ambalo halikwisha na halitaisha.

Wakati yote hayo yanatokea viwanda vinajengwa Mbeya, Mwanza, Moshi, Arusha tulikuwa na viongozi wazawa. Nani tumlaumu?
Nitakuwa nimekosea nikiandika kwamba jamaa zangu ninyi mna kitu ile inaitwa "selfishness" ??!! Ukishapata wewe you don't give a damn about others !! Au nasema uongo ?
 
Siwezi kufuta kwa zwazwa moja la kichaga linaloishi kwa mali za damu kwa kuuwaua watu na ndugu zake. Nyinyi ndiyo janja janja tu, mnaishi kwa kubebwa bebwa kama mlidhubuti kuiba BOT, nani asiyejua mali zenu za wizi na damu.
Kaka inawezekana ni kweli baadhi yao wako hivo! Lakini kubali ukatae wachaga ni wachapakazi na wabunifu ila nyinyi hamna kila kitu mna roho mbaya na mnampenda sifa! Pili kuna jirani zenu hapo wasukuma mlikuwa mnawadharau sana lakini saizi wameshawapiga gepu kubwa tu! Hata ukiangalia sekta ya usafitishaji wa abiria Wasukuma na wachaga ndo wanamagari ya kwenda huko kwenu! Nyamazeni miaka inakuja mtapoteana sana tu! Zamani mlikuwa mnahesabika malegend wa taifa hili saizi hata top ten hampo!
 
Huyu mama nakumbuka wakati bado anafanya kazi huko umoja wa mataifa, alikuja Tz akawa anahojiwa na waandishi wa habari kuhusu mikataba ya madini ilivyokuwa inainyonya nchi, akasema huko umoja wa mataifa kipo kitengo ambacho huzisaidia nchi zilizoingia mikataba ya kinyonyaji ili hiyo mikataba irekebishwe, nikamuona huyu mama ni MTU mzuri mzalendo kweli kweli duh! Siku ya pili yake tu alipohojiwa tena aliruka maili mia kama vile Jana hakuwa yeye !! Nilishangaa nikasema kweli wahenga walisemaga DUNIA HADAA ULIMWENGU SHUJAA !!! Ila naamini huwa hawapati peace of mind kwa sababu ya tamaa zao , KARMA IS REAL !
Zimbabwe hawataki kumsikia huyu mama jinsi alivyoungana na mabeberu kuisagia kunguni nchi yao ipigwe sanctions.
Wazungu wenyewe wakasema ripoti tumepewa na mwafrika mwenzenu Tena kutoka nchi ambayo ni maswahiba wenu Wala hakuna mzungu alieshiriki hiyo ripoti.
Mama nuksi huyu.
Yeye pia kwanini hajawekeza hata shule zake huko Kagera?
 
Back
Top Bottom