Mimi nadhani Dr ajibiwe kwa hoja.ameongea hayo ni kama ameanzisha jambo fulani fikirishi ili kila mmoja alete ufahamu wake kwanini uchumi uko hapo. Naona ana hoja za msingi.
Nadhani kama wananchi wametengwa iwe rai sasa kwa wanakagera wenyewe kupambana kama ambavyo kilimanjaro ilipambana. Serikali si ya kuitegemea sana. Tanga imeharibiwa na hawahawa. Tungeweza kuwa na bandari kadhaa tu eg dsm, bagamoyo, mtwara na tanga zikioperate kwa ukubwa lakini policies zilizowekwa zinadiscourage sana. Hizi bandari zingeweza kusave kutokana na ukanda ila ndo hivyo remote iko dsm.
Nakumbuka Rombo ilitengwaga na lami. Lami imewekwaga juzi tu hapo. Barabara ilikua mbaya sana. Na hata leo hii hakuna stendi ya kusema ni stendi kule. Huko boarder ni mateso th ndo maana wengi walikua wakipiga magendo wanakwepa kodi mpakani kwa kupitia njia za panya enzi hizo. Sema soko kubwa la mbao lililokuwepo Tarakea, viazi vya west na kilimo cha mahindi na maharagwe na alizeti viliweza changamsha. Watu walikua wanapambana vibaya mno despite ya kukosa barabara. Hawakujali sana huduma za kiserikali. Na hawa ni wale ambal hawakua na Elimu. Kagera Elimu waliipa kipajmbele sana lkn kiutendaji sijui tatizo ni nn. Naamini iko siku serikali itajileta yenyewe na magoti. Iko siku wataleta wenyewe huduma.
Pamoja na hayo, ndugu zetu wahaya, mumejawa na ubinafsi baina yenu wenyewe kwa wenyewe. Mtu hataki mwenzake ampite mwenzake. Iko policy moja naiaminigi, ukieainua watu kadhaa leo kesho ukaangula angalau hata wawili watatu watakuinua tena. Ukiwafungia vioo watu siku ukianguka ndo basi tena. Wivu, majivuno, utapeli unawaangusha sana. Ujanja ujanja haufai.
Mkoa wa kagera ni mzuri sana katika ardhi na ardhi mnayo kubwa sana. Kilimanjaro ardhi ni ndogo sana. Mupate wasaa na vjongozi wenu waache ubinafsi ziwekwe sera sahihi. Haya mambo ya kufunga boarder na jeshi unalo ni kurudishana nyuma. Tibaijuka asibezwe.
Sent from my SM-G960U using
JamiiForums mobile app